Sina tatizo lolote lakini nakosa furaha na amani

Asante sana. Mimi pia. Nahisi baadae ntapata madhara
 
Mama Pole na msongo wa Mawazo.. Nakushauri kama Ni Mucha Mungu basi Sali Sana tena Sana pia usipende kujitenga na watu wako wa Karibu mara nyingine Upweke hupelekea hofu ya Kuishi.. Ongea na Mungu Akuepushie Hofu ya Mauti.

Mungu akubariki
Asante sana. Na Amen kwa yote
 
Nalala tu mda wa kawaida. Siku zote. Saa now. Na kuamka saa kumi na mbili
Ni jambo jema kama usingizi unaupata na unapumzika vya kutosha.
Jaribu kufuatilia ulichokuwa unafanya wiki 3 nyuma na unachofanya sasa hivi, ni nini kimeongezeka au kupungua.
Iwe kwenye vyakula, Dawa, mazingira yanayokuzunguka na watu pia.
Je tarehe ndani ya hizi wiki 3, zinakumbushia mambo yaliyotokea miaka ya nyuma yakakuumiza?
Pole sana.


Asante. Ila sijui kufanya meditation
 
Nashukuru sana. Ngoja nifatilie
 

Usuwe na hofu hali kama hiyo inawatokea watu wengi unaweza kuimanage kwa njia ya mazoezi uwa yanaongeza feel good hormones na vile vile kwa kutumia imani yako ongeza muda wa kusali na kumuomba Mungu kamwe usitumie pombe kwani utakuwa unaongeza matatizo na kupoteza pesa zako
 
Asante sana. Uzuri situmii pombe
 
Mimi pia huwa inanitokeagaa ila huwa natokewa na hiyo hali nikifikiriaga jambo bayaa...
Km niliwahi kufikiria kipindi marehemu bibi yangu alivyokuwa hai tulivyokuwa tukipendanaa basi hapo hapo nakosa raha, sina amanii

Kwahiyo nsvyohisi utakuwa unamawazo unawaza vitu vibaya
 
Kuna mda nawaza vibaya. Ila siwazi sanaaa
 
umeota ndoto gani?, huzuni mara nyingi hujulisha tukio lisilo jema lijalo, au tukio baya ulilotenda na uhahitaji toba, au unahitaji utulivu ilikuskia kitu toka kwa MUNGU, kama wewe ni Mcha MUNGU ni vizuri kuomba angalau mara tatu kwa siku, ukiomba toba na kumsihi MUNGU nini kipo mbele ya huzuni hiyo
 

Pole sana ila tunae mfalme wa amani naye ni Mungu wetu muombe Mungu amani atakupa maana ameshakwisha kudhibitisha kuwa yy ni mfalme wa Amani najua atakupa amani maana amesema Amani utupayo sisi sio kama vile ulimwengu utoavyo yohana 14:27 nakutakia amani na furaha katika jina la Yesu be happy mdada
 
Mi nikihisi sijielewi elewi. Stress n.k naimagine 'system yangu' imejam so narefresh. Narefresh aje sasa?
*let go off social medias.
*Nalala mapemaaa for a better next day.
*nabadili ulaji, unywaji na uvutaji.
*nakaa mwenyew tu.
Baada ya siku 1,2 tu za utulivu huo kama ni tatizo ntakuwa nshajua..nasolve nasonga mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…