Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Januari 30, 2025, Mwanachama huyo alisema hali ni mbaya sana hasa msimu huu wa mvua ambapo Watoto wanaenda shule kwa tabu kutokana na maji na matope ya kutosha huku mabasi ya Shule na magari ya binafsi yakipata changamoto kupita.
Alisema kuwa ahadi zimekuwa nyingi bila utekelezaji hivyo akaomba Mamlaka zinazohusika kushughulikia changamoto hiyo.
Jana Februari 2, 2025 Greda lilionekana likipita na kukwangua Barabara hiyo, likafukia mashimo, kunyoosha sehemu zilizokuwa na changamoto na kuondoa visiki kadhaa.
Ilivyokuwa awali, soma hapa ~ Singida: Wakazi wa Unyakumi tunateseka na ubovu wa barabara. Ahadi zimekuwa nyingi bila utekelezaji