Singida Black Stars Yamuachisha kazi kocha wake Patrick Aussems na Msaidizi Denis Kitambi

Singida Black Stars Yamuachisha kazi kocha wake Patrick Aussems na Msaidizi Denis Kitambi

Ubaya Ubwela

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2024
Posts
1,353
Reaction score
3,060
Patrick Aussems na Denis Kitambi Waliwa kichwa
IMG-20241125-WA0028.jpg
 
Klabu ya Singida Black Stars imemfuta kazi Kocha Mkuu, Patrick Aussems, kutokana na matokeo yasiyoridhisha. Hadi kufikia hatua hii, timu hiyo imecheza mechi 11 za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ikishinda mechi 7, kutoka sare 3, na kupoteza mechi 1.
IMG_0922.jpeg

Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji, alijiunga na Singida Black Stars kabla ya kuanza kwa msimu wa 2024/2025, akilenga kuipa timu hiyo mafanikio makubwa. Hata hivyo, licha ya rekodi ya ushindi katika mechi nyingi, uongozi wa klabu umeamua kumaliza mkataba wake kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa timu.

Kabla ya kujiunga na Singida Black Stars, Aussems aliwahi kuifundisha Simba SC na AFC Leopards ya Kenya. Alipokuwa Simba, alifanikiwa kuiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
 
Kocha gani duniani ambaye timu yake huwa haifungwi ni kushinda tu? Pamba jiji wamchukue ausems haraka sana atawasaidia
Kuna namna yanga na wafuasi wake wanajiwekea guarantee ya kutofungwa na hasa kwa kutoheshimu mpira.
Inafika wakati wanatumia mbinu za nje ya uwanja ili mradi tu washinde.
Yanga na vitimu shikizi vyake ni wahuni tu walioiminiwa kuongoza timu
 
Back
Top Bottom