Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni

Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni

Tanzania kuna wachezaji wengi wazuri, tumekosa mfumo wa kuwatambua na kuwaendeleza.
Hatuna uhaba na hili la kuwapa uraia ni kuthibitisha ubutu wetu.
Hatuna wachezaji,ukiondoa wa Simba na Yanga unabakia na hamna .
Hawa Simba na Yanga kwasababu wanakutana na watu wenye uwezo zaidi yao katika vilabu vyao
 
Singida Black Stars imewabadilisha uraia wachezaji wake wanne wa kigeni na kuwa raia wa Tanzania, Singida imefanya hivyo ili kukidhi kanuni ya kuwa na wachezaji 12 wa kigeni.

Wachezaji hao ambao wamebadili uraia ni Emmanuel Keyekeh, Arthur Bada, Damaro Mohamedi na Golikipa Amas Obasogie.

Josaphat Arthur Bada (22) ni kiungo raia wa Côte d'Ivoire amewahi kuichezea klabu ya ASEC Mimosas na timu ya taifa Ivory Coast chini ya miaka 23
View attachment 3210353
Emmanuel Keyekeh (27) kiungo mkabaji raia wa Ghana alijiunga na Singida Big Stars akitokea FC Samartex ya ligi kuu ya nchini kwao.
View attachment 3210354
Pamoja na Mohamed Damaro (22), kiungo mkabaji raia wa Guinea ambaye pia ni mchezaji wazamani wa timu ya taifa chini ya miaka 18.
View attachment 3210380

==

View attachment 3210345
View attachment 3210383
Tunaomba picha ya Victoria Adebayo, tutakuwa tunamuita "Viki"😅😅😅
 
Hii nchi imeshakuwa ya watu wachache. Najua imekuwa hivyo kwa muda sasa ila imefika wakati hawafichi tena.

Wanangu tutafute pesa kwa njia yoyote ile.....pata pesa, pata mamlaka halafu pata heshima.
 
Bongo bwana🙆‍♂️
Yaani watu wanapata uraia kiurahisi rahisi
Hao walitakiwa wapate work visa,
next permanent resident visa kwa miaka kama mitano hivi then waaply huo uraia
Sasa hawa sidhani kama wamemaliza miaka 8 ndani ya nchi yetu
Anyway labda katiba inaruhusu
 
Ili kukidhi takwa la kikanuni la kuwa na wachezaji 12 wa kigeni watakaotumika ligi kuu Tanzania bara
Singida Black Star wamelazimika kuwapambania wachezaji wanne wa kigeni ili wapate uraia wa TANZANIA na kupata hadhi ya idadi ya kutumika katika ligi kuu

Tukumbuke pia Kibu Denis ambaye alikuwa raia wa Burundi alipewa uraia ili atumike Simba Sports club

Wachezaji hao ni
1. Emmanuel Keyekeh- Ghana

2. Josephat Arthur Banda- Ivory Coast

3. Mohamed Damaro - Guinea

4. Marouf Tchakei - Togo

Tukumbuke Kuna mechi Singida Black Star walichezesha wachezaji wote wa kigeni isipokuwa goal keeper Mnata, hapa wadau wa soka tulijiuliza kuhusu kanuni ya wachezaji wa kigeni hatukuwa na majibu
Labda hawa wachezaji walipatiwa uraia kimya kimya na nyaraka zipo tFF

Uraia wa TANZANIA umekuwa rahisi kupatikana namna hii,
Yaani sijui walipima vigezo Gani kuwapa wachezaji uraia na kazi Yao ni ya muda mfupi
Kibu kabla ya kuja kucheza Simba alishachezea timu mbili tofauti, alipokuja Simba ndio swala lake la uraia likaibuka. Wakati huo alikuwa ameitwa timu ya taifa kwa hiyo maswala hayafanani.
 
Back
Top Bottom