Singida BS kuzindua uwanja wao kwa mechi ya kirafiki na Yanga

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Klabu ya Singida Black Stars imetangaza rasmi uzinduzi wa uwanja wao mpya wa kisasa unaoitwa Airtel Stadium, uliopo katika eneo la Mtipa, mkoani Singida.

IMG_3522.jpeg
Uzinduzi wa uwanja huo mpya wa klabu hiyo utafanyika Machi 24, 2025, mkoani Singida, ambapo watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Wananchi, Yanga SC.

"Airtel Stadium ni sehemu ya dhamira ya Singida Black Stars ya kuwekeza katika maendeleo ya michezo kwa kutoa mazingira bora kwa wachezaji, mashabiki, na jamii kwa ujumla. Uwanja huu umejengwa kwa viwango vya kimataifa na unatarajiwa kuwa kitovu cha mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa," imeeleza taarifa ya klabu hiyo.

TAARIFA YA SINGIDA BS

IMG_3521.jpeg
 
Klabu ya Singida Black Stars imetangaza rasmi uzinduzi wa uwanja wao mpya wa kisasa unaoitwa Airtel Stadium, uliopo katika eneo la Mtipa, mkoani Singida.

View attachment 3272415
Uzinduzi wa uwanja huo mpya wa klabu hiyo utafanyika Machi 24, 2025, mkoani Singida, ambapo watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Wananchi, Yanga SC.

"Airtel Stadium ni sehemu ya dhamira ya Singida Black Stars ya kuwekeza katika maendeleo ya michezo kwa kutoa mazingira bora kwa wachezaji, mashabiki, na jamii kwa ujumla. Uwanja huu umejengwa kwa viwango vya kimataifa na unatarajiwa kuwa kitovu cha mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa," imeeleza taarifa ya klabu hiyo.

TAARIFA YA SINGIDA BS

View attachment 3272413
Vilabu vidogo vinapata pesa za kujenga viwanja halafu Simba na Yanga ni kupiga madomo tu.
 
Binafsi naona kama hivi vilabu vinafanyiwa figisu ili visije kujitegemea na waendelee kuvitumia kwa manufaa yao ya kisiasa. Ila pia hao SBS siyo mfano mzuri, kuna viashiria visivyo visafi kuhusiana na hii timu.
 
Mawazo yako yako sahihi kabisa! Kuna kitu kiko nyuma ya pazia ambacho wengi yawezekana hatukijui.
 
Unajenga uwanja wa mpira wa viwango vya kimataifa katika mji ambao hamna hata uwanja wa ndege wa kupokea ndege kubwa hata za safari za ndani. Tanzania tumebarikiwa vingi ila tumenyimwa viongozi.
Sema kuna watu mnapenda sana mikoani kuendelee kubaki vile vile miaka na miaka. Maendeleo yanaanza na hatua moja.
 
Haujanielewa. Ningekuwa na mtazamo huo nisingepinga uamuzi wa kujenga uwanja Arusha ambao binafsi naamini ulitakiwa upelekwe Mwanza, Mbeya au hata Morogoro.

Arusha imeendelea zaidi ya mikoa hiyo ila kuna vigezo vingine ambavyo vinavibeba mikoa hii kupata uwanja mpya wa kisasa kabla ya Arusha.
 
Vilabu vidogo vinapata pesa za kujenga viwanja halafu Simba na Yanga ni kupiga madomo tu.
Singida BS ni mali ya Mwigulu Nchemba. Na Mwigulu Nchemba ni Waziri wa Fedha. Na Waziri wa fedha ndio mlinzi wa Hazina yetu. Pia SBS na Airtel ndio wameshirikiana kujenga uwanja.
Katika Kila GB 1 mkipigwa MB 50 au 70 hamuwezi kushtuka na hata mkishtuka Waziri wa fedha anaweza kuzima kelele ndogo ndogo lakini hizo MB 50 mara kadhaa zinaingiza ngapi Katika kapu la maokoto ya kujenga uwanja?
Tunapigwa!
 
Haujanielewa. Ningekuwa na mtazamo huo nisingepinga uamuzi wa kujenga uwanja Arusha ambao binafsi naamini ulitakiwa upelekwe Mwanza, Mbeya au hata Morogoro.

Arusha imeendelea zaidi ya mikoa hiyo ila kuna vigezo vingine ambavyo vinavibeba mikoa hii kupata uwanja mpya wa kisasa kabla ya Arusha.
Jitahidi wakati mwingine kuwa mpole. SBS makao yake yapo Singida! Na mmiliki wake anafahamika. Sasa ulitaka wajenge uwanja wao Morogoro, Mbeya, nk kwa utaratibu upi?
 
Eleweni hili:
Waliohusika kujenga uwanja huo ni
1. Kampuni ya Airtel
2. Mo Dewji ( MeTL Group)
3. GSM

That is a fact!
 
Jitahidi wakati mwingine kuwa mpole. SBS makao yake yapo Singida! Na mmiliki wake anafahamika. Sasa ulitaka wajenge uwanja wao Morogoro, Mbeya, nk kwa utaratibu upi?
Nazungumzia uwanja wa Arusha unaojengwa na Serikali. Nimetoa maelezo hayo kumuelezea huyo aliyesema wengine tunataka mikoa ibaki ilivyo. Ukisoma vizuri utaelewa msingi wa maelezo yangu.

Ni wazi SBS kama taasisi binafsi ina uhuru wa kufanya chochote wanachotaka ila bado ni sahihi kuhoji kujenga uwanja wa kimataifa sehemu ambapo huduma muhimu hazipatikani.
 
Back
Top Bottom