Singida BS kuzindua uwanja wao kwa mechi ya kirafiki na Yanga

Klabu ya Singida Black Stars imetangaza rasmi uzinduzi wa uwanja wao mpya wa kisasa unaoitwa Airtel Stadium, uliopo katika eneo la Mtipa, mkoani Singida.

Uzinduzi wa uwanja huo mpya wa klabu hiyo utafanyika Machi 24, 2025, mkoani Singida, ambapo watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Wananchi, Yanga SC.

"Airtel Stadium ni sehemu ya dhamira ya Singida Black Stars ya kuwekeza katika maendeleo ya michezo kwa kutoa mazingira bora kwa wachezaji, mashabiki, na jamii kwa ujumla. Uwanja huu umejengwa kwa viwango vya kimataifa na unatarajiwa kuwa kitovu cha mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa," imeeleza taarifa ya klabu hiyo.

TAARIFA YA SINGIDA BS

Jambo jema yanga wahamishie mechi zao huko na inawezekana pia wakapewa hongera sana mwigulu!
 
Sasa kwa mfano tu Singida utailinganisha na Mtwara ambako ndege zinakwenda?
Mimi nimesema Singida hakuna uwanja unaopokea ndege kubwa hata za ndani, umekuja kuniambia sina exposure ila wakati huo huo unakubaliana na mimi kuwa ni kweli Singida inapokea ndege ndogo tu.

Sasa unachonipinga ni nini hasa?
 
Ndege kubwa za nini Singida?

Dom to Sgd ni KM kama 246 kwa bus ni three hours timu zitashuka Dom na watapanda bus.

Tanga kinaboreshwa kiwanja cha mpira kuwa cha kisasa sana na nadhani April wanazindua kuna airport ya ndege kubwa?

Learn sababu za ndege kupelekwa mahari kwa ajabu kama Mtwara na haziendi SGD au ndege kwenda Bukoba na haziendi Njombe
 
Unajua vigezo vya uwanja wa mpira kukubalika kutumika kwa mechi za kimataifa?
 
Eleweni hili:
Waliohusika kujenga uwanja huo ni
1. Kampuni ya Airtel
2. Mo Dewji ( MeTL Group)
3. GSM

That is a fact!
Nimeona sehemu pia kuhusu hili suala. Mo nadhani kashiriki sababu Singida ni kwao ingawa yule mdogo wake Fatma dewj yupo katika bodi ya SBS.
 
Klabu ya Singida Black Stars imetangaza rasmi uzinduzi wa uwanja wao mpya wa kisasa unaoitwa Airtel Stadium, uliopo katika eneo la Mtipa, mkoani Singida.

Uzinduzi wa uwanja huo mpya wa klabu hiyo utafanyika Machi 24, 2025, mkoani Singida, ambapo watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Wananchi, Yanga SC.

"Airtel Stadium ni sehemu ya dhamira ya Singida Black Stars ya kuwekeza katika maendeleo ya michezo kwa kutoa mazingira bora kwa wachezaji, mashabiki, na jamii kwa ujumla. Uwanja huu umejengwa kwa viwango vya kimataifa na unatarajiwa kuwa kitovu cha mashindano makubwa ya kitaifa na kimataifa," imeeleza taarifa ya klabu hiyo.

TAARIFA YA SINGIDA BS

Uwanja mpaa sasa hamna mwenye picha yake.
 
Wakuu
Timu ya Singida black stars inatarajia kuzindua uwanja wake wa nyumbani mkoani Singida ambao kwa mujibu wa makubaliano na kampuni ya Airtel Tanzania,utaitwa jina la Airtel stadium kwa muda wa msimu mmoja wa mashindano.

Uwanja huu ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuingiza na kuketisha watu elfu 15,na kwa sasa utaweza kuingiza mashabiki elfu 5,

Singida watacheza na klabu ya Young African SC na viingilio ni Tsh5,000.

Karibu Airtel Stadium Singida kutazama mchezo huo.
 
Back
Top Bottom