Singida: DC Iramba apongeza utengaji wa maeneo ya uwekezaji

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MHE MWENDA AENDELEA NA ZIARA YA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO, APONGEZA UTENGAJI WA MAENEO YA UWEKEZAJI
Mkuu wa wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda ameupongeza uongozi wa kata ya Ulemo kwa kutenga maeneo ya uwekezaji. Mhe Mwenda ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kujitambulisha na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara iliyofanyika katika eneo la Misigiri ofisi ya Kijiji.

Akitoa taarifa ya mpango mkakati wa kata ya Ulemo, diwani wa kata hiyo Mhe Peter John Peter amemuhakikishia Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe Suleiman Yusuph Mwenda kuwa kata yake imeandaa eneo kwa ajili ya kuwapatia Jeshi la zimamoto kwa ajili ya ujenzi wa ofisi. Ninaomba nikuhakikishie kiongozi tuna maeneo kwa ajili ya ujenzi wa benki na hata vyuo.

Akiongea na wananchi waliojitokeza kumsikiliza, Mkuu wa wilaya Iramba Mhe Mwenda amewataka viongozi wa kata nyingine kutenga maneno maalumu kwa ajili ya uwekezaji. "Wilaya yetu ina fursa nyingi za uwekezaji na ninawaomba tuendelee kutumia fursa zinazopatikana katika wilaya yetu kwa ajili ya kukuza uchumi wa wilaya yetu na wananchi kwa ujumla." alisema DC Mwenda.

#IrambaKaziInaendelea







 
Huko iramba ndio mtu akawekeze kuchinja punda n kuku,huko ndio watatoka wajinga waliotukuka mwigulu,dk gwajima,kitila mkumbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…