Pre GE2025 Singida: DED azuia Mkutano wa Hadhara wa Tundu Lissu, Mwenyewe apinga asema lazima Ufanyike au la Patachimbika

Pre GE2025 Singida: DED azuia Mkutano wa Hadhara wa Tundu Lissu, Mwenyewe apinga asema lazima Ufanyike au la Patachimbika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Taarifa ikufikie Popote ulipo kwamba, Huko Singida Mjini kumepangwa kufanyika Mkutano wa Hadhara wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu 8/6/2024, kwenye viwanja vya Stendi ya Zamani.

Taratibu zote zimekamilishwa na kwamba Polisi wameahidi kutoa ulinzi , lakini cha ajabu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Mjini amejitokeza jioni hii kutoa Tangazo la kusitisha Mkutano huo kinyume cha Sheria za nchi, bila sababu yoyote zaidi ya ile ya "MNANIJUA MIMI NANI"

Hata hivyo Tundu Lissu amepinga vikali Upuuzi huo wa DED na kuamuru Magari ya matangazo kuendelea na kazi, huku akiwaomba wananchi kuhudhuria kwa wingi bila uoga wowote ule maana uwanja wa Stendi ya zamani ni mali ya umma, huku akisisitiza kuwa wako tayari kwa lolote.

Screenshot_2024-06-07-21-43-45-1.png
 
Huo ndio mkwara alioutoa makamu Mwenyekiti wa chadema Mh Tundu Lisu jioni ya Leo

Lisu anasema wamefanya taratibu zote ikiwemo kutoa taarifa Polisi tangu Jumanne na Polisi wamewakubalia na kuahidi kutoa ulinzi

Lakini ghafla manispaa ya Singida wametuzuia kutumia Uwanja huo

Lisu anasema Chadema hawatakubali uonevu huo na kesho mkutano utafanyika kama ilivyopangwa hata kama watasombwa na kwenda kulala mahabusu

Taarifa imetolewa na Chadema tz Ukurasani X

Mlale Unono 😀😀

Mtanikumbuka 😂😂🌟
 
Huo ndio mkwara alioutoa makamu Mwenyekiti wa chadema Mh Tundu Lisu jioni ya Leo

Lisu anasema wamefanya taratibu zote ikiwemo kutoa taarifa Polisi tangu Jumanne na Polisi wamewakubalia na kuahidi kutoa ulinzi
Kama taratibu zote zimefatwa na Polisi wametoa Go ahead shida ni nini?

Hii ccm kuna siku itasababisha vita
 
Mkuu wa mkoa Singida Mh. Halima Dendego asikubali 4R za mheshimiwa rais Dr. Samia Hassan ahujumiwe waziwazi na DED wa halmashauri ya Singida mjini
1717791626030.png

Picha maktaba: RC Halima Dendego akitoa nasaha ktk shughuli ya kimkoa 6 June 2024.
 
Wafitini wa kupinga 4R wakiwa kazini, Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Amos Makalla akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Jesh Lupembe na Mkurugenzi wa Singida DC, Ester Chaula wakiwa ktk mikakati.

1717792085939.png

na wataalum wengine kutoka Halmashuri tofauti za Singida wakisikiliza kero za wananchi katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi ambaye leo amezungumza na wananchi wa Manispaa ya Singida.
 
View attachment 3011491
na wataalum wengine kutoka Halmashuri tofauti za Singida wakisikiliza kero za wananchi katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi ambaye leo amezungumza na wananchi wa Manispaa ya Singida.
😆😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom