SI KWELI Singida Fountain Gate FC yaituhumu TFF na Bodi ya Ligi mchezo dhidi ya Simba SC

SI KWELI Singida Fountain Gate FC yaituhumu TFF na Bodi ya Ligi mchezo dhidi ya Simba SC

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Baada ya Singida Fountain Gate FC kupoteza mchezo wao wa Ligi ya NBC Premier League wakiwa nyumbani dhidi ya Simba, kupitia mitandao ya kijamii walitoa malalamiko yao wakiituhumu TFF na Ligi ya Bodi kuwapangia refa kwenye michezo wanayokutana na Simba ambaye amekuwa akiibeba timu ya Simba SC baada ya kupewa maelekezo maalum ya kuwabeba Simba.

Singida FG wamedai kuwa katika michezo ambayo refa huyo amekuwa akichezesha dhidi ya Simba basi yeye ndiye huibuka Man Of The Match, hivyo wamezitaka taasisi hizo zinazosimamia ustawi wa mpira wa miguu nchini kutolea ufafanuzi.

Singida.jpg
 
Tunachokijua
Klabu ya Singida Fountain Gate ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa ni timu ya wafanyakazi wa Benki ya DTB ikifahamika kwa jina la DTB Football Club kabla ya kubadilishwa jina. DTB FC baadae ilipata hamasa kubwa baada ya kushiriki mabonanza ya mabenki nchini na kufanya vizuri, hivyo kupelekea uongozi wa DTB kuwekeza kwenye timu na kuipeleka kushiriki michuano ya mashindano hadi kushiriki Ligi Daraja la Kwanza (Championship).

Baada ya kufanya vizuri kwenye championship na kufanikiwa kupanda daraja kwenda Ligi Kuu mwaka 2022, Benki ya DTB iliamua kutoendelea kumiliki timu ya mpira ili kubaki katika kazi zake za msingi za kibenki. Hii ilitoa fursa kwa wadau kutoka mkoani Singida kuinunua timu hiyo na kuibadilisha jina kutoka DTB FC kwenda Singida Big Stars.

Mwaka 2022/2023, Klabu ya Singida Big Stars ilianza kushiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na kufanikiwa kufanya vizuri kutokana na mkakati wake wa kusajili wachezaji wa kimataifa wenye ubora wa hali ya juu na wale waliocheza vilabu vikubwa vya Tanzania vikiwemo Simba, Yanga na Azam.

Baada ya kumalizika msimu wa 2022/23 kwa mafanikio makubwa, Klabu ya Singida Big Stars ilipata ofa nzuri kutoka kwa mwekezaji Fountain Gate Academy ambae aliinunua kwa lengo la kuiboresha zaidi na kuiendesha kisasa.

Baada ya kununuliwa, Singida Big Stars ikatengeneza muunganiko na Fountain Gate Academy hatimaye kupata jina lake jipya la Singida Fountain Gate FC.

Tuhuma za Singida Fountain Gate FC
Oktoba 8, 2023, Singida Fountain Gate FC ilishuka dimbani kumenyana na timu ya Simba kwenye mchezo uliofanyika mkoani Singida katika uwanja wa CCM Liti. Katika mchezo huo, timu ya simba iliibuka na ushindi wa 2-1.

Baada ya kumalizika kwa mchezo ule, walaka unaodaiwa kutolewa na Singida Fountain Gate FC ukiituhumu TFF na Bodi ya Ligi ulianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua mjadala mkubwa.

Katika kufahamu ukweli wake, JamiiForums imezungumza na Hussein Massanza, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano (Msemaji) wa Singida Fountain Gate FC aliyeikana barua hiyo na kuutaka umma wa watanzania waipuuze kama alivyonukuliwa hapa chini;

Ndugu WanaJF,

Kwanza niwashukuru kwa maoni na mjadala huu, hata hivyo nasikitika kuona kuna kurasa feki zinatumia jina la timu yetu kuchapisha taarifa za upotoshaji na kusababisha taharuki. Kwa mfano ukurasa huu wa Facebook sio wetu na hatuutambui, hivyo ni taarifa potofu, IPUUZENI.

Kuhusu mechi yetu dhidi ya Simba SC ambayo tulipoteza 1-2 katika uwanja wa nyumbani, klabu bado haijatoa tamko lolote kwa njia yoyote. Endapo kuna malalamiko au hoja za kuwasilisha, basi tutafanya hivyo kwa kufuata kanuni za Bodi ya Ligi Kuu na sio kulalamika mitandaoni.

Niwatakie wakati mwema na niwape pole kwa usumbufu wowote uliojitokeza.


Aidha, Oktoba 9, 2023, ikiwa ni siku moja pekee tangu waraka huo uanze kusambaa, akaunti rasmi ya Singida Fountain Gate FC kwenye mtandao wa X ikinanusha kuhusika nayo, na kwamba ukurasa huo wa Mtandao wa Facebook uliotoa taarifa ulikuwa haumilikiwi na klabu hiyo.

fake-4-jpg.2779981

Ufuatiliaji wa JamiiForums umebaini kuwa barua (waraka) hiyo haijatolewa na Uongozi wa timu ya Singida Fountain Gate FC hivyo inapaswa kupuuzwa.
Mtalalamika Sana msimu huu utopolokwinyo, huo ni mwanzo tuu
 
Hawa dawau wa singinda ni kinanani? au ni miongoni mwawale wajube wa utopolo
 
Back
Top Bottom