Chakushangaza mada kama hizi kuna shabiki andazi linakuja kutukana badala ajikite kwenye uhalisia au kama unashindwa kaa kimya. Kuliko kuja na commrent za ajabu kama vile kilichotokea ni sawa kwakua imekua favor kwa timu yako. Idiots
Duh hili bandiko limefika hadi huku? Nimechelewa kuona.
Ndugu WanaJF,
Kwanza niwashukuru kwa maoni na mjadala huu, hata hivyo nasikitika kuona kuna kurasa feki zinatumia jina la timu yetu kuchapisha taarifa za upotoshaji na kusababisha taharuki. Kwa mfano ukurasa huu wa Facebook sio wetu na hatuutambui, hivyo ni taarifa potofu, IPUUZENI.
Kuhusu mechi yetu dhidi ya Simba SC ambayo tulipoteza 1-2 katika uwanja wa nyumbani, klabu bado haijatoa tamko lolote kwa njia yoyote. Endapo kuna malalamiko au hoja za kuwasilisha, basi tutafanya hivyo kwa kufuata kanuni za Bodi ya Ligi Kuu na sio kulalamika mitandaoni.
Niwatakie wakati mwema na niwape pole kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
Hussein Massanza,
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano (Msemaji)
Singida Fountain Gate FC.