Singida: Godbless Lema afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, asomewa mashtaka 15

Singida: Godbless Lema afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, asomewa mashtaka 15

Kilichomfikisha mahakamani kipo Sawa kabisa na Wala hakina uonevu,

Hata Mimi kwangu binafs mtu akisema kwamba Mimi ni muuwaji na nimeuwa watu na jamaa anasema ushahidi anao, kinachonipasa ni kwenda mahakamani na nispokwenda kumshitaki maana yake Mimi ni muuwaji kweli na badala yake huyo mtu anapaswa anipeleke mahakamani mimi

Na hata Mh Lema, Endapo serikali wasingempeleka mahakani yeye alipaswa awashitaki Kwa ushahidi huo alokuwa nao
 
CHADEMA wangekuwa na makambi ya kufunza na kutayarishi wanachama wake kuwa viongozi bora na wanaofuata siasa Safi kama ilivyo kwa CCM, matatizo haya ya mashtaka ya Mara kwa Mara kwa wapinzani yangekwisha. Ni mtazamo wangu.
Siasa safi za CCM..? Hizi za kina Kangi lugola kwenda kusaini mikataba ya kifisadi nje ya nchi.
 
CHADEMA wangekuwa na makambi ya kufunza na kutayarishi wanachama wake kuwa viongozi bora na wanaofuata siasa Safi kama ilivyo kwa CCM, matatizo haya ya mashtaka ya Mara kwa Mara kwa wapinzani yangekwisha. Ni mtazamo wangu.
Ni kama walivyo memba wao humu, hawajui siasa safi
 
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless J Lema amefikishwa Mahakamani Singida leo Tarehe 25/03/2020 na kusomewa Mashitaka Kumi na Tano (15).
===


View attachment 1398910
​
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Singida na kusomewa mashtaka 15 yanayomkabili.

Kati ya mashtaka hayo moja ni la kusababisha taharuki kwa jamii na 14 ya kupotosha jamii.

Amesomewa mashtaka hayo leo Jumatano Machi 25, 2020 na mawakili wa Serikali, Monica Mbogo, Rose Cholongola, Michael Ng’hoboko na Caren Malando mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Consolata Singano.

Imeelezwa kuwa Lema alitenda kosa hilo Februari 29, 2020 mjini Manyoni mkoani Singida katika mazishi ya kiongozi wa Chadema.

Anadaiwa siku hiyo na katika mitandao ya kijamii alisambaza taarifa za uongo kwa nia ya kupotosha jamii kuwa watu 14 wameuawa kwa kupigwa mkoani Singida.

Lema alikana mashtaka yote yanayomkabili na shauri hilo kuahirishwa hadi Aprili 15, 2020 huku mbunge huyo akiachiwa kwa dhamana.

Pia soma >
Lema: Nimepewa orodha ya viongozi wa CHADEMA waliouliwa Manyoni na Polisi kutofanya uchunguzi

DPP Biswalo Mganga: Lema kuchukuliwa hatua kwa kupotosha vifo vya watu 14 Manyoni
Ipo siku ccm nao watakuwa hawaashi kwenda mahakamani kama wanavyowafanyia chadema
 
Kilichomfikisha mahakamani kipo Sawa kabisa na Wala hakina uonevu,

Hata Mimi kwangu binafs mtu akisema kwamba Mimi ni muuwaji na nimeuwa watu na jamaa anasema ushahidi anao, kinachonipasa ni kwenda mahakamani na nispokwenda kumshitaki maana yake Mimi ni muuwaji kweli na badala yake huyo mtu anapaswa anipeleke mahakamani mimi

Na hata Mh Lema, Endapo serikali wasingempeleka mahakani yeye alipaswa awashitaki Kwa ushahidi huo alokuwa nao
Nimekuelewa vizuri Sana.
Wewe ndiyo umetoa mwanga kuwa,maneno yaliyosemwa na watu kuwa serikali inapoteza watu,inateka na kumpiga risasi Lissu NI kweli serikali imekubali Hilo kwakuwa haikuwasaka,kuwatia nguvuni na kuwashitaki waliosema hayo!!!! Mungu akubariki sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHADEMA wangekuwa na makambi ya kufunza na kutayarishi wanachama wake kuwa viongozi bora na wanaofuata siasa Safi kama ilivyo kwa CCM, matatizo haya ya mashtaka ya Mara kwa Mara kwa wapinzani yangekwisha. Ni mtazamo wangu.
Umenena kweli maana tunaona hayo makambi yenu yametuzalishia kina Makonda
 
Swali la msingi ni kweli ama siyo ukweli hicho alichoitaarifu jamii. Kama alisikia sikia tuu na hana uthibitisho apewe adhabu hata ya kunyukwa viboko (faru) 12 akiwa na kanga pekee iliyoloana maji ya pilipili na chumvi na video irushwe mtandaoni ili kukomesha uongo mambo ya kufungana ni msongamano
Na kama ni kweli utatakiwa wewe upewe adhabu kama hiyo
 
Nimekuelewa vizuri Sana.
Wewe ndiyo umetoa mwanga kuwa,maneno yaliyosemwa na watu kuwa serikali inapoteza watu,inateka na kumpiga risasi Lissu NI kweli serikali imekubali Hilo kwakuwa haikuwasaka,kuwatia nguvuni na kuwashitaki waliosema hayo!!!! Mungu akubariki sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, iko hivyo, nilikomalizia ndio inapaswa sasa watu kama wanaoushahidi wa kutosha kuhusu hayo sijui ya Lisu na wengine wengi ni kuiburuza serikali mahakamani

Je sasa ushahidi upo??
 
Natamani sana kuona hati ya mashitaka hayo 15! Nasikia walibishana sana kuchomeka shitaka la kutakatisha, hoja kwamba aliwashawi aliowapanga kumpa taarifa kwa fedha haramu alizopokea toka kwa mabeberu, hongera DPP.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akiwa mahakamani anajifanya kuweka uso wa huruma halafu akienda Instagram utamsikia oh siogopi kufa sijui nini.
 
CHADEMA wangekuwa na makambi ya kufunza na kutayarishi wanachama wake kuwa viongozi bora na wanaofuata siasa Safi kama ilivyo kwa CCM, matatizo haya ya mashtaka ya Mara kwa Mara kwa wapinzani yangekwisha. Ni mtazamo wangu.
Pole pole ndiyo ana siasa safi?
 
Back
Top Bottom