Singida: Godbless Lema afikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, asomewa mashtaka 15

Mashtaka yote hayo, haya yametengenezwa Na DPP kwa ajili ya kukomoa watu
 
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless J Lema amefikishwa Mahakamani Singida leo Tarehe 25/03/2020 na kusomewa Mashitaka Kumi na Tano (15).
===

View attachment 1398910
​
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Singida na kusomewa mashtaka 15 yanayomkabili.

Kati ya mashtaka hayo moja ni la kusababisha taharuki kwa jamii na 14 ya kupotosha jamii.

Amesomewa mashtaka hayo leo Jumatano Machi 25, 2020 na mawakili wa Serikali, Monica Mbogo, Rose Cholongola, Michael Ng’hoboko na Caren Malando mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Consolata Singano.

Imeelezwa kuwa Lema alitenda kosa hilo Februari 29, 2020 mjini Manyoni mkoani Singida katika mazishi ya kiongozi wa Chadema.

Anadaiwa siku hiyo na katika mitandao ya kijamii alisambaza taarifa za uongo kwa nia ya kupotosha jamii kuwa watu 14 wameuawa kwa kupigwa mkoani Singida.

Lema alikana mashtaka yote yanayomkabili na shauri hilo kuahirishwa hadi Aprili 15, 2020 huku mbunge huyo akiachiwa kwa dhamana.

Pia soma >
Lema: Nimepewa orodha ya viongozi wa CHADEMA waliouliwa Manyoni na Polisi kutofanya uchunguzi

DPP Biswalo Mganga: Lema kuchukuliwa hatua kwa kupotosha vifo vya watu 14 Manyoni
huyo mbwiga katoa tuhuma. Serikali kwa kutumia vyombo vyake vya uchunguzi. Kama si za kweli, apuuzwe.
 
Hapo japo moja litamlaza ndani, 15 ? This is a joke right?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom