Singida: Jela miaka 30 kumbaka mtoto wake wa kumzaa

Singida: Jela miaka 30 kumbaka mtoto wake wa kumzaa

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Singida, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mkazi wa Mtaa wa Kimpungua, Manispaa ya Singida, Hamisi Mtanda (37) kwa kosa la ubakaji.

jela (1).jpg

Mtanda amehukumiwa kifungo hicho baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa la kufanya mapenzi na mtoto wake wa kike, mwenye umri wa miaka 11.

Ilidaiwa na Mwanasheria wa Serikali, Elizabeth Barabara, kwamba mshtakiwa alianza kufanya mapenzi na mtoto wake huyo (jina linahifadhiwa) kuanzia Julai, mwaka jana, kwa kumchokonoa kwa vidole baada ya kutengana na mama wa mtoto huyo.

Mwanasheria huyo alidai kuwa mshtakiwa alitengana na mke wake, ambaye ni mama mzazi wa mtoto, Modesta Mshana na hivi sasa anaishi mkoani Dar-es-Salaam na alikwenda kumchukua mtoto huyo akiwa na umri wa miaka sita na kuanza kuishi naye.

Barabara alidai kuwa katika kipindi chote hicho, mshtakiwa huyo kabla ya kuanza kumwingilia kimwili mtoto ambaye ni mwanafunzi (jina la shule linahifadhiwa), alikuwa akimnyemelea usiku akiwa amelala.

Alidai kuwa mshtakiwa baada ya kuona sehemu za siri za mtoto zimetanuka, ndipo alipoanza kumwingilia kimwili na wakati akifanya unyama huo, mtoto alikuwa akipiga kelele za kuomba msaada bila mafanikio kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata.

Mwanasheria huyo alidai kuwa, kutokana na mshtakiwa kukana shtaka la kutenda kosa hilo, upande wa Jamuhuri ulipeleka mashahidi sita, akiwamo daktari ambaye alithibitisha bila kuacha shaka yoyote kwamba mshtakiwa ndiye aliyemwingilia mtoto huyo.

Kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, mahakama ilijiridhisha bila kuacha shaka yoyote kuwa mshtakiwa huyo ndiye aliyemfanyia unyama huo mtoto wa kumzaa mwenyewe.

Kabla ya kutolewa adhabu, mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea kwa kudai kuwa hakufanya unyama huo bali mtoto huyo alikuwa amefanya vitendo vya ngono na mwalimu, bila kumtaja ni mwalimu yupi.

Akitoa hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi Robert Oguda, alisema anamhukumu mshtakiwa kifungo cha miaka 30 jela, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama za mshtakiwa huyo.
 
Mimi napenda sana pumpuu,siwezi kabisa kuamka asubuhi kwenda kufanya shughuli bila kupiga bao hata kama ni la kuku,hata kama wife hayupo ntabeba mchepuko tu.Kitu nisichoelewa kuhusu baadhi ya wanaume wenzangu hivi mtoto wa miaka 11 tena uliyemzaa mwenyewe anakuvutia nini?
 
Ni upuuzi wa baadhi ya wanaume yaani tena afungwe maisha
 
mpaka hapo mi naona kesi imetengenezwa kama mama wa mtoto walitenganga basi hio imekua ni kukomoana mimi haya mambo ya kutengana nayajua sana hasa pale mwanaume unapokua na maisha ya kubadilisha mboga halafu mwanamke mliyetengana anaona unakula na wanawake wengine lazima kesi isukwe isukike uende na maji...

ila tumuachie Mungu ndiye anajua ukweli uko wapi maana tumeona watoto wengi wakishakua wakubwa wa kujitambua wengine hua wanakili kabisa walipangwa na wanajutia walichokifanya...
 
Watu kama hawa ni wa kuhasiwa tu
Kuna jimbo moja la Kaduna nchini Naigeria wamepitisha sheria hiyo ya kuhasi watuhumiwa wanaopatikana na hatia ya kubaka wasichana chini ya umri wa mtu mzima.

Kuna wakati niliwasikia wabunge wetu wikizungumzia hii, nadhani baadaye waliipuuza!

Ingelikuwa mhalifu akithibitishwa kafanya, pmb zinakwenda na maji anabakia na bomba lisilokuwa na kazi ili kumkata ngebe, makosa aina hiyo yangelipungua ama kwisha kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
toka lini mahakama ikatenda haki ???

wakati anabaka mahakama ilikuwepo au mahakama inafuata kilochoandikwa kwenye makaratasi ?
Kwa jambo lililofanywa mafichoni unategemea kuupataje ukweli?

Ukiachana na mambo ya rushwa, mahakama ndiyo chombo cha kuchambua ukweli na kutoa haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi napenda sana pumpuu,siwezi kabisa kuamka asubuhi kwenda kufanya shughuli bila kupiga bao hata kama ni la kuku,hata kama wife hayupo ntabeba mchepuko tu.Kitu nisichoelewa kuhusu baadhi ya wanaume wenzangu hivi mtoto wa miaka 11 tena uliyemzaa mwenyewe anakuvutia nini?
Huyu ni mtia nia, wajumbe wakafanya yao, Sasa babu kampa nae kutekeleza vigezo na masharti
 
Kwa jambo lililofanywa mafichoni unategemea kuupataje ukweli?

Ukiachana na mambo ya rushwa, mahakama ndiyo chombo cha kuchambua ukweli na kutoa haki.

Sent using Jamii Forums mobile app

hujui ulisemalo ambao tulishafikishwa mahakamani ndio tunaju kua mahakama inatenda haki au la !

ila hata hivo mi siilaumu sana kwa sababu sikua eneo la tukio
 
mpaka hapo mi naona kesi imetengenezwa kama mama wa mtoto walitenganga basi hio imekua ni kukomoana mimi haya mambo ya kutengana nayajua sana hasa pale mwanaume unapokua na maisha ya kubadilisha mboga halafu mwanamke mliyetengana anaona unakula na wanawake wengine lazima kesi isukwe isukike uende na maji...

ila tumuachie Mungu ndiye anajua ukweli uko wapi maana tumeona watoto wengi wakishakua wakubwa wa kujitambua wengine hua wanakili kabisa walipangwa na wanajutia walichokifanya...
Mkuu hizi kesi zipo nimewahi kukutana nayo moja, mke alilazwa hospital akamwacha mtoto na baba yake. Huku nyumbani jamaa akawa anamwingilia kimwili mwanae
 
Kuna jimbo moja la Kaduna nchini Naigeria wamepitisha sheria hiyo ya kuhasi watuhumiwa wanaopatikana na hatia ya kubaka wasichana chini ya umri wa mtu mzima.

Kuna wakati niliwasikia wabunge wetu wikizungumzia hii, nadhani baadaye waliipuuza!

Ingelikuwa mhalifu akithibitishwa kafanya, pmb zinakwenda na maji anabakia na bomba lisilokuwa na kazi ili kumkata ngebe, makosa aina hiyo yangelipungua ama kwisha kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeisikia pia,maana hata mwanamke mbakaji anakatwa Falliopian tubes pia,ila mwanaume akibaki na bomba si anasimamisha kama kawaida au inakuwaje?
 
Mkuu hizi kesi zipo nimewahi kukutana nayo moja, mke alilazwa hospital akamwacha mtoto na baba yake. Huku nyumbani jamaa akawa anamwingilia kimwili mwanae

inawezekana ila asilimia kubwa hizi kesi hua zinahusisha ugomvi wa baba na mama
 
Nimeisikia pia,maana hata mwanamke mbakaji anakatwa Falliopian tubes pia,ila mwanaume akibaki na bomba si anasimamisha kama kawaida au inakuwaje?
Mkuu korodani zikitoka, ndiyo mwisho wako utabaki ka'zezeta, maana hata hasira unakuwa hauna!

Hauonagi maksai wale ngombe wa kulima wanavyokuwa?

Huwa ule muungurumo wao wa kidume (kuhiga) unawatoka, hawawezi kupigana tena.

Pmb zimebeba takribani hormone zote za kiume.

Adhabu hiyo ikiidhinishwa yaweza kuwa kamkomoeni zaidi hata ya hicho kufungo cha miaka 30.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom