Singida: Serikali yakiri Kijiji cha Dominiki kina changamoto ya maji, yaelezea mipango

Singida: Serikali yakiri Kijiji cha Dominiki kina changamoto ya maji, yaelezea mipango

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Siku chache baada ya Wananchi wa Kata ya Mwangeza, Wilaya ya Mkalama mkoani Singida kulalamikia kuchota dumu sita hadi 12 ili wapatiwe huduma ya afya katika Zahanati ya Dominiki ikiwemo kwa Wanawake wanaotaka kujifungua kutokana na changamoto ya maji, Mamlaka husika imekiri uwepo wa changamoto ya maji na kueleza imeshatenga bajeti ya ili kutatua changamoto hiyo.

Kusoma malalamiko ya Wananchi, bofya hapa ~ Singida: Wanawake wanachota maji kwenda nayo Zahanati wakati wa kujifungua katika Kijiji cha Dominiki

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) - Singida, Mhandisi Lucas Saidi amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama hali ya upatikanaji wa maji kwa sasa ni asilimia 70.7

Amesema tayari Serikali katika bajeti ya Mwaka 2024/25 imetenga jumla ya shilingi milioni 150 ili kukabiliana na changamoto hiyo katika vijiji kadhaa ikiwemo Asanja, Singa, Mwangeza, Kinto na Dominiki.

Ikumbukwe Februari 3, 2025, Wanawake katika Kijiji cha Dominiki, Kata ya Mwangeza, Wilaya ya Mkalama walidai wanalazimika kuchota maji dumu 6 hadi 12 kwa ajili ya kutumia wakati wa kupata Huduma ya Matibabu katika Zahanati ya Dominiki ikiyopo kwenye kata hiyo.

Wamesema hali ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho ni changamoto kubwa na wanalazimika kuamka Saa Tisa Usiku ili kuyatafuta
 
Siku chache baada ya Wananchi wa Kata ya Mwangeza, Wilaya ya Mkalama mkoani Singida kulalamikia kuchota dumu sita hadi 12 ili wapatiwe huduma ya afya katika Zahanati ya Dominiki kutokana na changamoto ya maji, Mamlaka husika imekiri uwepo wa changamoto ya maji na kueleza imeshatenga bajeti ya ili kutatua changamoto hiyo.

Meneja wa RUWASA - Singida, Mhandisi Lucas Saidi amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama hali ya upatikanaji wa maji kwa sasa ni asilimia 70.7

Amesema tayari Serikali katika bajeti ya Mwaka 2024/25 imetenga jumla ya shilingi milioni 150 ili kukabiliana na changamoto hiyo katika vijiji kadhaa ikiwemo Asanja, Singa, Mwangeza, Kinto na Dominiki.

Ikumbukwe Februari 3, 2025, Wanawake katika Kijiji cha Dominiki, Kata ya Mwangeza, Wilaya ya Mkalama walidai wanalazimika kuchota maji dumu 6 hadi 12 kwa ajili ya kutumia wakati wa kupata Huduma ya Matibabu katika Zahanati ya Dominiki ikiyopo kwenye kata hiyo.

Wamesema hali ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho ni changamoto kubwa na wanalazimika kuamka Saa Tisa Usiku ili kuyatafuta
 
Attachments

  • IMG-20250209-WA0004.jpg
    IMG-20250209-WA0004.jpg
    183.7 KB · Views: 3
Back
Top Bottom