Singida: Watu 6 wafariki kwa ajali ya gari

Singida: Watu 6 wafariki kwa ajali ya gari

Gari ndogo hizi ni mbaya kwa safari ndefu, ipo siku ntakutafutia 4×4 moja Kali sana
Usiniumize wakati unajua natamani kuwa hata na nyumba ya vyumba viwili.Afu Siku zinavyozidi kwenda naiwazia sana nyumba kuliko mapenz.Soon nakuacha love😔
 
Acha ujinga wewe takwimu zinasoma katika afrika mashariki na kati Tanzania inaongoza kwakua na idadi kubwa ya fifo vya RAIA kwaajali kuliko nchi yeyote ile

Niwakati wetu madereva kujitambua uwapo na usafiri ufanye nn uwapo barabarani

Uchaguzi niwako ukimbie ili ufe au uwe mstarabu
 
Usiniumize wakati unajua natamani kuwa hata na nyumba ya vyumba viwili.Afu Siku zinavyozidi kwenda naiwazia sana nyumba kuliko mapenz.Soon nakuacha love[emoji17]
Usiniache, navyokupenda hivi ntapata shida sana. Kwenye nyumba hapo ndio uwanja wangu, mm ni contractor pia. Hebu tushauriane unataka ya aina ipi? Unataka iwe mbeya au dar?
 
Ajali mbaya iliyo husisha gari dogo aina ya Raum imetokea wilayani Mkalama katika mkoa wa Singida.

Chanzo cha ajali ni mwendo kasi.

Mzee Kinana nilikwambia kupitia uzi fulani hapa, kazi iendelee.

========

Watu sita wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Raum, kuacha njia na kupinduka katika eneo la Iguguno Ushamba Wilayani Mkalama Mkoani Singida, huku chanzo kikitajwa kuwa ni mwendokasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa, amesema tukio hilo limetokea jana na kusema Dereva wa gari hilo alikuwa anaendesha bila kuchukua tahadhari na ndipo gari hilo lilipohamia upande wa pili wa Barabara na kupinduka mara tatu.

Ajali hiyo imetokea kwenye Barabara Kuu ya Dar es Salaam - Mwanza wakati abiria wa gari hilo wakitokea Arusha kuelekea Mwanza ambapo Watu watano kati yao walipoteza maisha papohapo huku Dereva wa gari hilo akipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Singida.

Trafiki ee naona unatiririsha mada za lawama tu, kwani hizi ajali hazikuwepo hapo kabla!!
 
Kinana alikataza traffic kukaa barabarani, haya ndio matokeo yake
 
Haya ndio Kinana aliyataka. Watu wasafiri kwa uhuru. Maana yake watu wafe mapema.

Marekani ambako wana high ways za kueleweka, zimenyooka na kila aina ya miundombinu ya barabara bora trafiki hawakosekani halafu Kinana anataka barabara hizi wanazojenga ccm zenye matuta na mashimo barabarani watu waruhusiwe kutembea wanavyotaka.

Kinana anataka nchi ijiendeshe kisela kama enzi za kikwete, unregulated county. Haya ndio wanayataka.

Ni yale yale ya Samia alisema wafanyakazi walikua na nidhamu ya uoga, baadae akakiri kwamba nidhamu imeshuka zaidi.

Kinana anataka nchi iniendeshe kama autopilot kama Somalia(home).
Mzee kinana ni jambazi yule. Anataka urahisi wa kusafirisha magendo. Traffic wangekamata meno ya tembo sasa ameona watimuliwe ili aibe vizuri.
 
Usiniache, navyokupenda hivi ntapata shida sana. Kwenye nyumba hapo ndio uwanja wangu, mm ni contractor pia. Hebu tushauriane unataka ya aina ipi? Unataka iwe mbeya au dar?
Sawa nimeghairi to leave,so I stay with you forever.....Uendeshe vyema si umeona ajali zilivyonyingi sikuhiz love?! Take care!
 
Kinana alikataza traffic kukaa barabarani, haya ndio matokeo yake
Sidhani kama ndo sababu,mbona ajali zipo Kila Leo kabla hata ya katazo.Sema madereva nao inabidi wawe makin pia na uhuru waliopewa wasiutumie vibaya.
 
Sawa nimeghairi to leave,so I stay with you forever.....Uendeshe vyema si umeona ajali zilivyonyingi sikuhiz love?! Take care!
Ahsante sana, nipo makini na sijawahi kupata accident na naombea iendelee kuwa hivyo
 
Comrade Kinana asilaumiwe kila dereva akiwa na akili timamu anapaswa kutambua kuendesha gari bila ya tahadhari (reckless driving) kunauwa, hili halihitaji uangalizi wa Traffic.
 
Haya ndio Kinana aliyataka. Watu wasafiri kwa uhuru. Maana yake watu wafe mapema.
Huu ni ushamba wetu wa kutozoea barabara zilizonyooka ndiyo maana sisi madereva limbukeni tunaona tuendeshe kwa kasi.

Magari yenyewe asilimia kubwa second hand za miaka ishirini nyuma halafu tunajisifia barabarani.

Hata Kinana asingesema kitu hizo ajali zingeendelea kutokea tu.
 
Hata hiyo sio sawa, Raum ni 5 seats. Wawili mbele, watatu nyuma. Ila huwa tunaforce sana kuweka watu wanne nyuma, gari yenyewe wakiwa tu watatu nyuma tu inakuwa imechuchumaa.

Kwa route za gari kukaa wanne nyuma sio mbaya japo hairuhusiwi, Ila kwa route ndefu ni kutafuta shida tu
Labda kuna mama alibeba mtoto!
 
sikuona haja ya kinana kutoa ile kauli lkn ni kama mambo mengine mnambebesha bila kuwa na kumbukumbu sahihi.

sijui nyinyi watu hamna kumbukumbu au kibarua chenu mnaona kimeenda na nyasi.

mbona ajali zimekuwa nyingi kabla ya hata kauli ya kinana?

hebu pitieni related post hapo chini muangalie kabla ya kinana kuongea kulikuwa na ajali ngapi.
 
Ajali mbaya iliyo husisha gari dogo aina ya Raum imetokea wilayani Mkalama katika mkoa wa Singida.

Chanzo cha ajali ni mwendo kasi.

Mzee Kinana nilikwambia kupitia uzi fulani hapa, kazi iendelee.

========

Watu sita wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Raum, kuacha njia na kupinduka katika eneo la Iguguno Ushamba Wilayani Mkalama Mkoani Singida, huku chanzo kikitajwa kuwa ni mwendokasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa, amesema tukio hilo limetokea jana na kusema Dereva wa gari hilo alikuwa anaendesha bila kuchukua tahadhari na ndipo gari hilo lilipohamia upande wa pili wa Barabara na kupinduka mara tatu.

Ajali hiyo imetokea kwenye Barabara Kuu ya Dar es Salaam - Mwanza wakati abiria wa gari hilo wakitokea Arusha kuelekea Mwanza ambapo Watu watano kati yao walipoteza maisha papohapo huku Dereva wa gari hilo akipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Singida.
Yani umeripoti ajali na hapohapo unamlaumu kinana .
Kwani ajali haikuwepo ?
 
Back
Top Bottom