Single girl akiona hii lazima atukane

Single girl akiona hii lazima atukane

Kama haya yote mabaya yanafanyika, ni sababu ya kuzifumbia macho na kuzihalalisha?

Katika swala la kutoa mimba, ndiyo.

Kama itasaidia kupunguza vifo vya wanawake vinavyotokea katika kujaribu kutoa mimba kienyeji/kisiri.

Weka maswala ya dini na sayansi mbalimbali, au hutaweza kuelewa naandika nini. Itakuwa sawa na kubishana na jiwe.
 
Mke mwema anatoka kwa Bwana..
ukiangalia uzuri utakuja kujta mkuuuuuuuu....
stay down go in yo kneel you will have her.
 
You are a hypocrite!

Tofauti zetu kubwa zipo kwenye sheria. Mfano, kuoa jinsia moja kwa wao ni jambo la haki ya binadamu kama ilivyoamua makakama zao.
(Binafsi, naamini ndoa ni ya jinsia tofauti lakini naheshimu na sipendi kuingilia maisha ya mtu).

Tanzania kuna watu wengi tu wanazalisha na kusepa, wanawake wanatoa mimba kila siku, watoto wanalelewa bila baba, watoto wanabakwa na walimu na kuzaa nao, wanafunga ndoa za mikataba n.k. Hata wasagaji na makhanithi wapo wengi tu katika jamii zetu. Tunajitia hatuwaoni.

Jaribu Sweden au Marekani kummbaka mtoto au usilipe mahitaji ya mtoto uone moto wake.

Pia, mimba wanaitoa kiusalama zaidi huko kwa mama. Binafsi, ni muhimu zaidi kuliko kukataza na kuweka maisha ya wanawake katika hatari kwa kuitoa mimba kisirisiri au kienyeji.

Ifahamu jamii yako mwenyewe kabla ya kuishutumu nyingine.

Nyani haoni kundule.

Pia, uzilazimishe watu usiowajua kusoma biblia yako na kuishi kwa sheria zake. Wengine wanaishi kwa raha zaidi Kishinto au Kibudha au bila kuamini Mungu yoyote.

Una haki ya kuishi kivyako, huna haki ya kumpangia maisha mwenzio, awe yupo Sweden au Tanzania.
Wewe pumba kweli naona huijui jamii yako, jaamii ya afrika inautamaduni wake na inauheshimu, hakuna jamii inayoweza kuishi vizuri bila kuwa na utamaduni na sheria zake. Sisi huku kwetu mwanamke kuolewa au mwanaume kuoa ni heshima huko kwenu haituhusu na katika jamii hakuna mtu anaweza kutafuta furaha anavyopenda yeye. Hata obama aliambiwa na kinyata. Civilization inaweza ikaanzia africa.
 
Wewe pumba kweli naona huijui jamii yako, jaamii ya afrika inautamaduni wake na inauheshimu, hakuna jamii inayoweza kuishi vizuri bila kuwa na utamaduni na sheria zake. Sisi huku kwetu mwanamke kuolewa au mwanaume kuoa ni heshima huko kwenu haituhusu na katika jamii hakuna mtu anaweza kutafuta furaha anavyopenda yeye. Hata obama aliambiwa na kinyata. Civilization inaweza ikaanzia africa.

Mada ni ndoa KIUJUMLA, siyo ndoa za jamii ya Kiafrika.

Jifundishe kujipanga kabla ya kuwafundisha wachangiaji wengine.

Tunajadili ndoa siyo watu wa zamani waliokaa ndani ya majabali na mwituni wakiwinda uchi.

Halafu hutaki kujadili hoja kwa jicho la kidunia halafu upo haraka kumtaja Raisi wa nchi za magharibi kama kipimo chako cha mtu "muhimu" kuambiwa ustaarabu umeanza Afrika.

Kama umeandika kila nchi ina utamaduni wake, kwa nini unapinga tamaduni za nchi nyingine ambazo wanawake au wanaume hawataki kuoa na kusema "haituhusu"?

Kama umesoma sosholojia, utajua kuwa kila nchi ikitajirika, wanawake na wanaume wanachelewa kuoa au kuolewa. Na kuna nchi nyingine, ndoa inakuwa haina umuhimu wowote.

Hii si sababu za utamaduni, bali ni sababu za kiuchumi zaidi. Wajapani wapo tofauti sana kiutamaduni na watu wa nchi magharibi lakini hata wao wanawake wao hawataki kuolewa walipotajirika na ndoa kupungua.

Pia, utamaduni haugandi, unabadilika. Kama ungeganda, leo usingevaa nguo za katani bali ungejistiri na majani.

Kwa nini utamaduni wa Kiafrika uwe bora zaidi ya utamaduni mwingine? Umeupimaje?
 
Back
Top Bottom