You are a hypocrite!
Tofauti zetu kubwa zipo kwenye sheria. Mfano, kuoa jinsia moja kwa wao ni jambo la haki ya binadamu kama ilivyoamua makakama zao.
(Binafsi, naamini ndoa ni ya jinsia tofauti lakini naheshimu na sipendi kuingilia maisha ya mtu).
Tanzania kuna watu wengi tu wanazalisha na kusepa, wanawake wanatoa mimba kila siku, watoto wanalelewa bila baba, watoto wanabakwa na walimu na kuzaa nao, wanafunga ndoa za mikataba n.k. Hata wasagaji na makhanithi wapo wengi tu katika jamii zetu. Tunajitia hatuwaoni.
Jaribu Sweden au Marekani kummbaka mtoto au usilipe mahitaji ya mtoto uone moto wake.
Pia, mimba wanaitoa kiusalama zaidi huko kwa mama. Binafsi, ni muhimu zaidi kuliko kukataza na kuweka maisha ya wanawake katika hatari kwa kuitoa mimba kisirisiri au kienyeji.
Ifahamu jamii yako mwenyewe kabla ya kuishutumu nyingine.
Nyani haoni kundule.
Pia, uzilazimishe watu usiowajua kusoma biblia yako na kuishi kwa sheria zake. Wengine wanaishi kwa raha zaidi Kishinto au Kibudha au bila kuamini Mungu yoyote.
Una haki ya kuishi kivyako, huna haki ya kumpangia maisha mwenzio, awe yupo Sweden au Tanzania.