Single Moms njooni tuelimishane kitu hapa

Single Moms njooni tuelimishane kitu hapa

Mwenzenu huu usinglemom ulinikuta chap Kwa haraka...Yaan bila kutarajia...mtu niliyemwamini na niliyekuwa na malengo nae alinigeuka....nikisema iliingia Kwa bahati mbaya nitakuwa nadanganya...tulipanga Nami nilijiaminisha Kwa sababu Kuna hatua tulipitia ambazo nikajua yessss,nimelipata bwana!

We bwana wee...kumbe nimepatikana ...Yaan Ile kitu kutiki tu jamaa akasema "katoe mimba".....nyie wadada wenzangu mnaotupondea singlemoms...siyo Kwamba sikuweza kumeza P2 au miso-p au kwenda hospital kukwanguliwa...noo,ningeweza ila tu huyu kiumbe nakuwa na hatia.So mwishowe nikazaa huyu son wangu...jamaa alichoniambia ni kuwa...umezaa basi umejipanga kulea I mean haijawahi toa hata Senti kulea mwanangu then Leo hii anajitutumua anataka mwanaye.Teh!

Sasa point yangu ni ipi ya kuwakusanya wamama wenzangu...ni hivi...hatujaua,tumezaa,tunalea....na huenda tukawa tumebahatika kupata wanaume wema wanaotupenda siye na wanetu...sasa ninachokuuliza ..hivi wenzangu mnawezaje kuendelea kuwasiliana na mwanaume aliyeshindwa kukupa thamani ya kuweka ndani na akakuacha na mtoto....mnawezaje kuvua nguo tena Kwa mwanaume ambaye si mumeo Yaan Ex tena aliyekudharaulisha? Aisee,mwenzenu nimeshindwa....nilimwambia nitakuwahisha kunizoeašŸ˜–šŸ¤Ø

NB:sijawahi mjaza sumu mwanangu...hicho ndicho nilichoshinda....namwacha ajue yeye ndo atachambua magugu na ngano.Hongereni Kwa kupambana wanawake wenzangu kulea ni Kaz kweli.Nawapenda sanašŸ˜šŸ˜˜
Sheemeji leo umeniuzunisha sana 🤨🤨 Zulu man naomba uzibe pengo vyema mama wa watu bado moyo unavuja dam



Sema kuna wanaume jau sana na majeuri ole wake mwanaume wa hivi aje kwa dada yangu mwangu naua
 
Mimi ni Observer tu,
🤣🤣Wee,sema kweli!?
šŸ˜‡šŸ˜‡šŸ˜‡šŸ˜‡, siunajua observers wa uchaguzi hata kama kuna wizi wa kura, wao usema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Sema daah, mnapitia nyakati ngumu, kuna single mom of 2 daughters, anataka nimuoe, mimi huyu😳😳😳😳😳, hapana.
 
Mimi ni Observer tu,

šŸ˜‡šŸ˜‡šŸ˜‡šŸ˜‡, siunajua observers wa uchaguzi hata kama kuna wizi wa kura, wao usema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Sema daah, mnapitia nyakati ngumu, kuna single mom of 2 daughters, anataka nimuoe, mimi huyu😳😳😳😳😳, hapana.
Unakula tu,Wala hakuna shida mkuu
 
Back
Top Bottom