Single mothers waheshimiwe: Tuache mara moja kuwabeza

Single mothers waheshimiwe: Tuache mara moja kuwabeza

Siwezi kusimama mahala popote pale kutetea single mother never ever!!
Nitasimama mahala popote pale kuwa tetea na kutoa misaada kadiri ya uwezo wangu kwa wajane tu. hata biblia haijamuandika popote single mother kuwa atetewe wala kusaidiwa biblia inamjua mjane tu.

Kutetea single ni kutetea uovo 100% single mother hata awe dada yangu ama mtoto wangu lazima nikemee.Biblia yangu inaniambia mwanamke mpubavu huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe!

Masingle mother wengi kilicho waponza ni tamaa na kiburi chunguza vizuri utanielewa! kwenye mia wali lizwa na wanaume hawafiki hata15 walio baki tamaa,umalaya na kiburi niko hapa nimekaa.

Unaingia kwenye mahusiano na bint baada ya muda unagundua mpo wa3 mara nina mimba yako utakubali?

Acha kujipunguzia heshima hata jamii itakushangaa
 
Nikiwa nimejawa na jazba nawakemea watoto wa kiume na wavulana wote wanaodhihaki na kuwa kebehi single mothers.

Ieleweke kwamba, single mother ni mama yake mtu, ni kama alivyo mama yako. Aidha, wanawake hawa ni majasiri, wameamua kutunza uhai , kinyume chake wangetoa mimba na kuwa kama hayo majanamke mengine mauaji (slay queens) ambayo yanaua watoto kwa kutoa mimba na mnayashobokea.

Single mothers, wamefanya kazi ya Mungu, wamelea uhai miezi tisa tumboni na kuleta kiumbe duniani. Kwa kudra za Mwenye-Enzi- Mungu, kiumbe hicho kinaweza kuwa mtu muhimu na kutoa mchango mkubwa kwenye ujenzi wa taifa letu.

Kudhihaki single mothers ni sawa na kuchochea utoaji wa mimba, jambo hili likome mara moja. Waache wakina mama wanaopata mimba walete viumbe duniani. Mungu amesema nendeni duniani mkaijaze dunia, hongereni akina mama mlioamua kulea watoto wenu

Pamoja na hayo niliyoandika hapo juu, single mother ni reflection ya udhaifu wetu wanaume, yaani kuna mpuuzi mmoja ambaye anashindwa au anakataa kutimiza wajibu wake. Uwepo wa single mothers ni aibu kubwa kwetu wanaume, yaani hatufanyi wajibu wetu

Kwa kumalizia, single mothers wanapitia madhila mengi, haswa wale wasio na kipato cha kutosha na cha uhakika,. Hivyo ni rai yangu, kwa wale wababa wenye uwezo tuwatunze single mothers kwa manufaa mapana ya watoto na jamii nzima.

Kwa wale wenye changamoto za afya ya akili, uwanja ni wenu kuja kubisha na kupinga madini haya

Nimetoa uzi huu kama nilivyomuahaidi Demi
Bila kupima vinasaba, hata kama baba yupo na mnafanana, anaweza akawa ni baba mlezi bila yeye kijijua, so mama ni uhakika kuwa ni mzazi wako bila ya shaka
 
Kuna single maza mmoja hivi tuna heshimiana sana. Katika mazungumzo yetu aliwahi kunishi sana niwaepuke single mother mithiri ya swala aonaye Simba.
 
Back
Top Bottom