[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Samahani nimecheka.Pole kwake.
Akitafutiwa na asipompenda huyo mwanamke.???
Mimi mwenyewe sijui kawaza nini kichwani mwake, lkn hiii na wezekana,sababu tuna mwanatu alivyopata kazi ya kueleweka 2016,kamwambia baba yake amtafutie mke na si kwamba jamaa hajui kutongoza, kwani hata baadhi ya mademu zake na wajua.
Mzee wake akaenda Kibaha kamtafutia mke, jamaa akaoa 2016 mwezi 8 (ndoa za kislam zipo faster) mpaka sasa yupo na mke wake na wana mtoto mmoja. Huyu jamaa ni rafiki yetu may be nahisi ushauri atakuwa kaomba kwa huyu mwana.
Mfano ktk maisha yangu nishaattempt kuoa 2times ila mademu walinizingua. Wa kwanza alikuwa rafiki yangu mtaani kwa kifupi tumekuwa wote alivyo enda kusoma na mimi ni kaenda kusoma wakati na maliza 2013 nilikuwa nishapiga mahesabu ya kuoa mwakani 2014 ,ila huwezi amini 2013 mwezi wa saba narudi home nakutana na meseji fupi mimi na ww basi nishapata mwengine nilikuwa mpole bembeleza wapi wana nao wakanipa ushauri nikasema fresh yatapita.
Wa pili ni mdogo wa rafiki yangu,alikuwa black beauty mwenye shape yake, ila anapenda sana kuvaa mavazi vitenge ya heshima, nilitupia binti akanielewa. Nikawa na mahusiano naye ila ya siri kaka yake hakufahamu, yule demu kipindi hicho naunga unga na tempo lkn kila wiki naampa 50 na bado matatizo ya vocha sijui kusuka natoa hela, nilikuwa na mwamini na niliamini huyu ni mke wangu hata mtaani kwao wanamsifia kwa tabia njema.
Naye baada ya miezi sita 2017 mwezi 11 kama sikosi ilikuwa jumamosi mida ya saa tatu akaniandikia magazeti kama mawili yaliyo shiba mimi na ww basi nina mtu wangu ambaye nimetoka nae mbali, daaaaah mwanaume nilichoka ,nikasema hebu ngojea niisubirie simu ipoe, ile naingia whatsapp nataka kuongea nae, kwenye profile na status kaweka picha ya huyo jamaa ambaye ni jirani yake ,kuanzia hapo dada yangu mimi naamini mwanamke nitakayemuoa ataibuka.Huwezi amini huyo wa kwanza kazalishwa kaachwa yupo kwa mama yake, huyu wa pili baada ya miezi mitatu anaomba turudiane na huwezi amini tokea 2018 mpaka sasa bado anaomba turudiane amewatumia marafiki zangu mpaka mdogo wangu ila wapi sina time nae manake niliblock mwisho nimemwacha, anapiga simu hata sipokei.
Nina mwanangu mwengine demu wake wamotoka mbali tokea primary sasa hivi ni engineer kwenye kampuni ya simu, na kumbuka 2015 alikuwa anatupiga mikwala "vijana oeni, mimi mwakani naoa....",demu wake alipangiwa ualimu mkoa wa Dom, basi bwana mwana akamsuprise siku yake ya kuzaliwa.Sababu getho la huyo demu mwana analijua kila baada ya miezi kazaa alikuwa anamtembelea. Kudadadeki kufika hamadi anakuta demu ana mimba na kuna kidume kinazunguzunguka na taulo, mwana alibeba Laptop kama zawadi, mwana alichoka nahisi kilo tano zilikatika ghafla na kukonda juu. Jamaa mpaka sasa yupo single na huyo demu wake kazalishwa kaachwa.
Dada wanaume waoaji wapo ila wanawake tunaowaamini kwamba ni wake wema ndio wanaotukata maini.Hapo kuna wengine wamewaacha vijana wenzao wanahangaika na mababu/waume za watu kisa wana hela mwisho wa siku jua likizama kachuja wanapigwa chini ,anachukuliwa mwengine upweke huo akiwa single mother.