Otaigo1
New Member
- Sep 16, 2021
- 1
- 1
Serikali Imewekeza sana kwenye miundombinu ya sekta ya elimu kwa miaka sasa, uwekezaji huo unaanzia Elimu ya msingi, sekondari za kata, vyuo vya ufundi na vyuo vikuu na kumekuwa na ongekezo kubwa la idadi ya wanafunzi unaojiunga mashuleni na vyuoni.
Lakini elimu wanayoipata haiakisi uhalisia wa mabadiliko ya sayansi na technologia na wakati, hivyo kinachofundishwa hakimsaidii mwanafunzi na hivyo wahitimu wamekuwa wahanga wa mifumo ya Elimu. Kijana anahitimu lakini hana uwezo wa kufanyakazi aliyosomea. Hii hutokea kwa sababu ya mitahala mibovu ya Elimu inayoshindwa kumpa mwanafunzi ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira. Pia serikali imeshindwa kuja na vipaumble vya mahitaji halisi ya soko la ajira. Hivyo wanafunzi wengi kujisomea fani ambazo wakimaliza hazina ajira au hazitajiki sokoni (Skills Mismatch).
Kwa upande Mwingine uchumi wa Nchi unakuwa kwa kasi ndogo kwa kiwango ambacho kushindwa kuajiri wanahitimu wanaomaliza vyuo. Takwimu zinaonyesha serikali na taasisi binafsi zinatengeneza ajira 40,000 tu sawa na asilimia (5.6%) kwa mwaka wakati wahitimu wanaoingia katika soko la ajira kwa mwaka hufikia 900,000. Takwimu hizi zinaonyesha pia wahitimu wanashindwa kujiajiri kutokana na mfumo ya elimu ambayo haimuandai mwanafunzi kujiajiri.
Ushauri Kwa serikali

- Serikali iwe takwimu ya idadi ya watu na fani gani kwa mwaka inahitaji (twakimwi ya uhitaji wa serikali na sekta binafsi na aina ya fani inayohitajika) hii itatoa muongozo kwa wanafunzi wajielekeze kwenye fani zipi wakati wanachagua nini wanataka kusomea.
- Vyuo Vikuu vifanye utafiti kwenye sekta binafsi na serikali ijue uhitaji halisi wa watalaam na viandae mitahala inayoendana na uhitaji wa soko la ajira na mitahala inayojenga wanafunzi kwa vitendo na kujiajiri
- Kuwe na Mpango wa muda mrefu wa kwenye sekta ya Elimu na utengenezaji wa ajira (maono ya mbali ya utanuzi kwenye sekta za uchumi za nchini
- Usawa kwenye Nyanja ya elimu (mitahala ya elimu, vifaa,)
- Kuwe na mpango wa Kitaifa kwa wahitimu wanaotaka kujiajiri wapewe rasmali ikiwemo mikopo, ardhi hata serikali kuwawekeza dhamana iwapo watataka kuchukua mikopo kwa ajili ya biashara.
Upvote
1