Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Hilo hata mimi nimelioma jamaa angeachwa amgeansika story nzur lakini sasa analipua ili iishe kama wanavyotaka wenye haraka
 
Inaendelea.........

Wandugu habari mchana sasa tuendelee tulipoishia, ubalozini. Sasa maisha yakawa yamehamia ubalozini maisha yakawa changanyikeni maisha yakawa hayana thamani tena, wanaume wajasiri wakajitolea kukaa zamu kulinda geti la ubalozi, maji yakakata watu wanalala njee kwenye nyasi hakuna cha mume wala mke wa mtu kama una mkeka mnalala chini familia mbili, ile mandhari ya ubalozi ikageuka kuwa kama kambi ya wakimbizi majani ya kukauka yote, maua yakafaa vyoo vikaanza kuzidiwa maji hamna daaahhh watoto vilio usiku kucha, ukichanganya na milio ya risasi ya mara kwa mara ikawa ni kusubiri siku ifike tuone nini kitakachotokea .

Sasa kuna mambo yalikuwa yanaendelea huku tanzania, kulikuwa sijui kuna vikao vya mazungumzo sijui ya amani kati ya serikali ya rwanda na waasi kama sijakosea alikuja habyarimana mwenyewe na baadhi ya mawaziri wake na wakati tunasikiliza redio bbc jioni anatoka kwenye kikao kuna maneno Aliyatamka hakika kuanzia siku hiyo niliwachukia Wanyarwanda wote, mungu anisamehe.

Alisema hivi watanzania na wageni wote nchini rwanda wako salama wala hakuna lolote linaloendelea baya kwao na serikali inaendelea kuwalinda, na maneno kuwa nchi imeingiwa na machafuko ni propaganda za waasi wa Kagame kujaribu kuishawishi dunia ili imuunge mkono katika hatua yake ya kuivamia rwanda na apuuzwe. Na siku hiyo ndo ilikuwa mwisho wa kusikiliza redio maishani mwangu, utamaduni ambao nimeendelea nao hadi sasa huwa sisikilizi redio kabisa,yani nikija kwako kukutembelea ukitaka kunifukuza kwako washa redio naondoka hapo hapo.

Watu wakawa wengi chakula kikawa kimeisha.tukafanya mawasiliano na balozi,sasa kuna kitu kilikuwa kinaendelea ambacho tulikuwa hatujui. unawakumbuka wale jamaa saba alikuwepo moja kama mpemba hivi siku hiyo alikuja na balozi, pale akaangalia hali halisi wakaingia ndani walichoengea na balozi hatujui ila wakatoka wakaondoka hapo wote tukabaki tunatazamana hakuna anaejua nini kinaendelea.

Sasa ipo hivi hakuna watu wabaya kama wafanyabiashara lakini walikuwa na msaada mkubwa unajua kama sio wafanyabishara wa maroli tungekuwa tumeondoka mda mrefu ila kukawa na zuio kuwa maroli yote ya watanzania ambayo yalikuwa bandari kavu eneo la MAGERWA (tamka majerwa) lazima yarudi na madereva wake wote sasa ikawa kuna mengine yalikuwa hayajapakua ililazimu yapakue na, ndo walipokuwa wale manjemba saba waliokuja na defender nilikuja kuambiwa baadae na dereva moja hivi lakini nae alikuwa anawaona tu wanazungukazunguka mle ndani ya bandari ila wakiwa makini kweli kweli na mabegi yao.

Siku zikayoyoma ikawa kila siku lazima balozi awashe gari lake aende Majerwa( bandari kavu) Peke yake anapakia tambi, majani ya chai maziwa ya kopo, na mazagazaga mengine waliyokuwa wanashusha kwenye maroli ya watanzania analeta tunakula siku imeisha mlo moja tu hakuna cha mama anayenyonyesha wala wala mtoto ni mlo moja tu basiii.siku zikawa zinakwenda ikawa sasa inakaribia siku yenyewe sasa ambayo iliweka historia nchini rwanda....................

Mwanzo wa safari ya mateso, kutembea katika njia ya mauti, kushuhudia maiti zimezaga barabarani kama nzige ,unyama mbaya kuwahi kuushudia maishani mwangu.....

Itaendelea............. Leo leo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu hii stori ni nzuri, ila kuna kaujumbe Bossless anatufikishia, maana kila akiandika stori yake kuna mistari huwa anaweka na kuisisitiza mara kwa mara.

Ahsante mzee tunakuelewa, Mungu ibariki Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
hata mie nimemsoma vema kabisa....kuna ujumbe anajaribu kuufikisha kwetu sisi watanzania...soma kwenye mistari
 
Hii imekuwa fupi, unatuacha na uraibu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa heshima na tahadhima mkuu naomba usitumie kingereza, kiache tu kipumzike, ni hayo tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu na wewe ulikuwepo huko?
Hapana Mkuu, jamaa zangu ndiyo walikutana na mkasa huo mbaya,
Avatar yangu inaelezea mengi Mkuu,hapo ni makumbusho yalipowekwa mafuvu ya wahanga wa lile tukio baya kuwahi kutokea.

Mwenyezi Mungu awarehemu,wapumzike kwa amani Ameen..
 
Hapana Mkuu, jamaa zangu ndiyo walikutana na mkasa huo mbaya,
Avatar yangu inaelezea mengi Mkuu,hapo ni makumbusho yalipowekwa mafuvu ya wahanga wa lile tukio baya kuwahi kutokea.

Mwenyezi Mungu awarehemu,wapumzike kwa amani Ameen..
Dah pole ni wabongo au warwanda ?
 
Hapana Mkuu, jamaa zangu ndiyo walikutana na mkasa huo mbaya,
Avatar yangu inaelezea mengi Mkuu,hapo ni makumbusho yalipowekwa mafuvu ya wahanga wa lile tukio baya kuwahi kutokea.

Mwenyezi Mungu awarehemu,wapumzike kwa amani Ameen..
Na hakuna alorudi salama akakupa mkasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…