Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Mzee baba kama hautajali taja jina la balozi wetu aliyekuwa Rwanda wakati huo serikali ya Rwanda ilipofanya majaribio ya mauaji ya watutsi mwaka 1992 na baadae mauaji rasmi mwaka 1994. Sidhani kama jina la balozi yeyote katika nchi yoyote na kwa mwaka wowote ni siri yoyote kwa mtu yeyote yule. Hivyo sioni sababu kwa nini usitaje jina la huyo mwanadiplomasia wetu kwa wakati huo.
Google mzee au nenda wizara ya mambo ya nje kaulizie ila jua tu alikuwa mmama jina lake sitaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhalisia ndo ulikuwa huo ila vinena zinaacha zinaongoza chumvi nyingiiiii ila mauji ilikuwa kama tu po jahanamu vile.
Hii story kama sinema vile kila hatua inaleta hamu ya kujua ya mbeleni.

Kuna CD jina nimesahau inaelezea mauaji ya watutsi daah baba mmoja mhutu akapoteza mke na watoto kisa mke ni mtutsi

Wanafunzi wakachapwa risasi darasa zima kisa watutsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda alikuwa akiongea na mbobezi wa nchi ya Rwanda wa wakati huo yaani waziri wa mambo ya nchi za nje kumlalamikia kile wanachokifanya watu wake kwenye ubalozi wa Tanzania.
Baadae nilikuja gundua kuwa alikuwa anaongea na mkuu wa interahamwe ( jina lake nimelisahau jamaa babe liuaji hatari sijui kama bado lipo hai, kama bado yupo hai hajasakwa na kufikishwa ICC basi haina haja ya kuendelea kuwahukumu wengine) ila jamaa hilo ndo lilikuwa kama Li-mkuu la majeshi kigali nzima huyo ndo top akisema ua umekwisha akisema acha umepona, unajua mabalozi lazima wawe na koneksheni kubwa sanaa wakati mwingine kwa upande wa serikali, waasi (kama wapo) na wapinzani. Mtakufa wote lakini balozi atapona, atalindwa atasindikizwa na kuwekwa sehemu salama. Nyinyi mnahenyeka tuu na vipassport vyenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapo uliposema wadada wa kitutsi walivokimbilia ubalozi wetu nimekumbuka nilihadithiwa ubalozi pale ulipo tayari inatambulika kama vile ni sehemu ya ile nchi iko pale, hata inapotokea tatizo ukikimbilia pale basi umeingia nchi nyingine
 
umemaliza udbs wewe?
Inafikirisha sana ndiyo! Kwa maana ya kuitazama siasa yetu lakini ukitembea nje tu nyumba uliopo utagundua lifestyle ya watanzania ni tofauti sana na huko Rwanda, hakuna mtanzania mwenye munkari wa kushikiana mapanga achilia mbali ak47! Hata mambo ya kuchoma moto vibaka yamepungua sana.

Pengine wanasiasa ndo wangechochea vuguvugu za vijana kupigania ukombozi dhidi ya mkoloni mweusi! Wanasiasa hao wako wapi!!? Hao walozeekea kwenye vyeo vyao na sasa wanakwenda kugongeshana miguu na mkulu!? Hakuna anaependa vita ila na sisi tumelala mno.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana unachosema coz kuna watu hawapendi kusikia ukweli huu kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Humu kuna wasomali (anaebisha huwa hao wasomali wanaongea hadi hicho kisomali humu) ,kuna Warundi, Wanyarwanda etc mataifa yanayoongea kiswahili wamo humu

Kigoma wahutu ni wengi lazima wawatetee wahutu wenzao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Of all jf members wewe ndio nimekuspot direct Kama tiss employee directorate ya IT pale eagle wing maana huuu uzi Kuna infiltrators wawili wa kagame walioko umangani wanaufwatilia kila post na katika cloud chek ushawasiliana nao mwakajanadesembanakwenyejambolinalohusuuzihuunawewekwawikitatumweziuliopitaulikuwakigalibishanianike
Jifunze kuandika mkuu, mwandiko wako unatia aibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM iko wapi mkuu! Hii ambayo wamo kina Waitara, Mtatiro, Polepole, Kafurira, Mashinji, Dr. Slaa, Kabudi, Mgwira, Masha n.k? CCM ambayo imemtimulia mbali Membe na kumpa onyo Kinana! Tusikalili sana kuhusu neno CCM maana tayari wamechangamana na wapinzani waliopigania mabadiliko kwa kiasi kikubwa hapo awali. Kama hawawezi kuyaleta mabadiliko hayo wakiwa huko chamani, ni dhahiri unafiki wetu watanzania utakuwa ni wa kiwango cha kutisha.

Hivyo vikosi uchwara vya vyama havijaweza kuleta impact ya vita hapa nchini. Huko mitaani watu hata hawajali kabisa wapo kwenye harakati zao. Harakati za mnyukano wa kisiasa nchini hazizidi hata 5%, watu wapo bize na soka, kukanyaga mafuta, ubuyu wa instagram, kusaka noti... Hata CORONA tu hawana habari nayo.

Vita hapa kwetu si kesho wala mwaka kesho! Ni kama haipo forever. Watu wetu wengi, hata akina Seif Sharrif, Zitto, Mbatia wanaamini katika "Mwenye nguvu mpishe" na "Mpiga ngumi ukuta huumia mwenyewe"

Sent using Jamii Forums mobile app
Naungana na wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bossless,

We Muongo, ulienda mwezi WA sita hahahaha.

Vita imeanza mwezi WA nne imeisha mwezi WA Saba but wewe ulipata KAZI mwezi WA sita wakati serikali ya Rwanda imevurumishwa na Rpf na kukimbilia Gisenyi Kwa kina Haruna Niyonzima huku mapigano makali yakiendelea.

Anyways wakati unapata hiyo KAZI Rais wa Rwanda alikuwa anaitwa Nani?

Jibu huna Mpira uishie hapa.

" falsus in uno falsus in omnibus" false in one thing false in every thing.

@moderators futeni uzushi huu unachafua hadhi ya jf
Wahutu mpo wengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LIKUD,
Mbona inaonekana wewe ndiye una haraka? Wengi tunafahamu kwamba vita imeanza mwezi huo wa nne hadi wa saba tena mwaka 1994.

Yeye ameanza na mwaka aliomaliza masomo ya stashahada mwaka 1989 na kupata kazi kwenye ubalozi huko Rwanda. Bado anaendelea na background hajafikia kipindi vita imeanza.
Mhutu kama sio interahamwe huyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bossless usimalize story mapema maana kipindi hiki Cha Kwaresma tumeachana na uzi wa kula tunda kimasihara. Kipindi hicho ukiwa mkoa wa Kagera ndege zilipishana angani kama daladala. Baadae ilianzishwa kambi ya Burigi na mpaka leo bado watusi masalia wapo.
 
Habari zenu wakubwa kwa wadogo.

Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu.

Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu wakati naandika huu ushuhuda wangu binafsi ambayo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili nchini rwanda wakati wa vita ya kikabila ,wenyewe hupenda kuiita mauji ya halaiki.

Stori inaanza wakati ndo nimemaliza masomo yangu ya uhasibu ngazi ya stashahada mwaka 1989 (sintotaja chuo hicho) nikajaribu kuomba kazi wizara ya mambo ya njee mungu si Athumani nikapata kazi ubalozi lakini nikapaangiwa kituo changu cha kazi kigali-Rwanda, kama sijasahau ubalozi Tanzania ulikuwa maeneo yanaitwa KICHUKIRO ,kwa sasa sijui kama bado upo palepale au vipi sina uhakika.

basi mwezi wa sita baada ya kukamilisha taratibu zote nikaanza safari ya kwenda Rwanda kituo changu cha kazi kipya,ajira mpya na mara ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania... Safari ikaanza kwenda kuanza maisha mapya nchi ya watu ,mbali na ndugu jamaa na marafiki nikiwa sijui chochote kuhusu nchi hiyo..

Angalizo. naomba tuvulimiliane ni long stori kidogo na yanaweza jitokeza makosa ya kiundishi na kifasihi.... Ntaelezea mambo mengi sana ya kutisha ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ambayo hadi leo nimejitahidi kuyasahau lakini imeshindika kabisa.

Safari inaanza pale Mnazi moja nakumbuka enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya Booking. unawahi alfajiri na mapema unatafuta basi lako unapanda tu unasubiri safari ianze.

Basi nikiwa na mabegi yangu na shilingi za kitanzania 60 elfu(nilipewa kwa ajili safari na kujikimu na passport ) tu ,naianza safari ya kwenda Kahama, safari ikaanza midaa ya kama saa moja kamili asubuhi (jina la basi lile nimelisahau ila nakumbuka lilikuwa rayland) kipindi hicho barabara ni vumbi tupu changarawe la vumbi hadi linaingia kupitia madirishani, baada ya safari ya uchovu mwingi hatimae saa nane usiku tunaingia singida stand. Mimi mgeni sijui niende uelekeo gani ikumbukwe miaka ile nyumba za wageni zilikuwa za kuhesabu basi ikabidi tushuke pale stand tukawa tunakula mikate na chai na wengine chai na kahawa.

Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!

Tumefika Kahama stand tumepokelewa na wapiga debe enzi hizo wao ndo walikuwa kama mawakala wa magari makubwa anakubebea mzigo hadi kwenye gari unalipa nauli yeye anachukua chake mnaachana hapo hapo hapo ni usiku inabidi kupata gari ya kwenda boda ya Rwanda na Tanzania Rusumo hapo unavuka Mpaka, kuna mto mkubwa unaitwa mto Rusumo unapita kwenye daraja la chuma kama lile lile liloejengwa na wanajeshi pale njia panda Kawe unavuka ng'ambo ukagonga passport ,cha kuchekesha pale kulikuwa hakuna magari ya abiria makubwa.

Magari ya abiria kutoka boda hadi kigali mjini yalikuwa hakuna, ilikuwa inakubidi upande roli la mizigo au abiria mjichange kwa makundi mkodi magari madogo kama tax ila mnabananishwa humo hatari na mizigo juu, kutoka boda hadi kigali ilikuwa kama mwendo wa masaa nane hivi kuingia kigali mjini.
Hatimae baada ya kubadilisha fedha zetu kuwa mafaranga tukapata usafiri wa kutufikisha kigali nakumbuka kundi langu kwenye gari tulilokodi nilipanda na wazaire watupu hivyo kelele zilikuwa nyingi hadi tunaingia kigali wanaimba nakuongea sanaa ubishi mwingi mara mpira mara siasa ili mradi makelele tu.

Saa tisa mchana nikawa tumewasili kigali town enzi hizo sijui lolote kuhusu mji huo zaidi ya address na namba za simu ikabidi niangaze angalau kupata simu lakini wapi,aise kinyarwanda sijui na wao kiswahili kigumu kila nae mujliza ila kupata mawasiliano sikupata msaada ikabidi nikasogolea kwenye stand ya mabus madogo nikamuulize konda kuwa nataka kwenda ubalozi wa Tanzania akaishia kucheka tu niligundua hakunielewa lugha .

Nakumbuka nilikaa stand pale hadi saa kumi na mbili bila bila ikabidi niulizie sehemu pakulala hapo nikaeleweka nikaambiwa lazima upande bus nipelekwe sehemu inaitwa NYAMIRAMBO na nikaambiwa pia kuwa kuna waswahili wengi nikapanda bus hadi nyamirambo nikashushwa tu stand konda akanionyesha kuna hoteli moja ilikuwa imeandikwa nakumbuka inaitwa kama sijasahau ilikuwa inaitwa IMHALA ila nyamirambo ilichanganya kigodo naweza fananisha Magomeni enzi zile.


Nikaenda nikalipia chumba nikaomba kuelekezwa eneo la kula nikaelekezwa, nikaenda nikala halafu nikarudi kujilaza nikipanga namna ya kuingia kesho u abalozi wa Tanzania kuanza majukumu mapya .

Itaendelea...........





Sent using Jamii Forums mobile app
Inaendelea.....

Niwakumbushe tu kuwa tayari nimeshazitaja dalili mbili za kuingia kwenye machafuko rasmi sasa twende na dalili ya mwisho ambayo KUOGOPANA.

KUOGOPANA, hii maanake nini? Iko hivi ukiona yule jirani au majirani mnaanza kuogopana yani kila mtu yupo kivyake ujue sasa hali imefika mwisho kilichobaki ni kila mtu kumuwahi mwenzake ili abaki salama yeye hakuna namna.sasa hapo naomba nizungumzie jambo kabla sijaendelea.vita vya ukabila vikawa vimekufa rasmi ikaibuka vita nyingine mbaya ya njaa hapo tena ikawa haangaliwi mtusi au mhutu .ukiwa na chochote hata gunia la sembe la Kilo kumi watu wakajua utake usitake utatoa tu mgawane hapo ndo iliibuka dhana ya kuogapana yani ukija kwangu utajua na nini? Ukitoka unaenda kuwaambia wengine usiku mnanivamia mnachukua chakula ukileta ubishi mapanga ni halali yako.

Watu wakawa hawaaminiani tena siku zikawa inasonga kila mtu kivyake hakuna ujamaa wala undugu kila mtu la kwake ,maduka yakavunvwa wakapora vitu mji mzima chakula kikageuka kuwa almasi, watu wakaanza kuchunguzana kwa siri ukiwa na chakula upo hatarini kupotea au kuuawa kabisa tena na majirani hao njaaaa.....ikachukua nafasi si kwa wenyeji au wageni vita mipakani inaendelea unachinja kuku unamla siku 4 ,ana chacha wala husikii harufu ya kuchacha mambo yanazidi kuwa mabaya zaidi mpaka ikawa imefikia mwezi wa pili mwishoni 1994 sasa kila kitu kikawa wazi kuwa rwanda imebakia sekundi izame. propaganda zilipungua redioni wale wasemaji wasemaji wakawa hawasikiki tena mambo yanakwenda mrama(wameshakimbia) kigali inabaki tupu wale magwii wa siasa za propaganda wakapotea ghafla redio siku nzima inapiga muziki wa chama.

Watumishi wote tukaamriwa tureport ubarozini hakuna kutoka nilichukua begi langu hadi ubalozini nikawa sikumbuki tena mapenzi yangu na yule binti maanake nini tupo hatua mbaya na ya mwisho ya uharibifu hapo hakuna unachokifiria zaidi ya nafsi yako pekee unawaza unatoka aje salama hapo.

Kufika ubalozini nikakuta watu kibao (watanzania) waloikuwa rwanda aise watu wamejazana halafu eneo dogo ukiangalia wengine wamekuja na wake zao wakitisu kabisa na watoto wao Watusi pure aise
Nikajisemea leo balaa tusipouwa basi ,balozi akawa kama kapigwa na ganzi akiwaangalia wale watu ikawa ni kujieleza kila moja na watu wake hiyo ndo ikawa kazi yetu tunawahojimtu na mkewe. Daahh

Hesabu ikaonyesha kuwa watanzania tupo kiasi ila watoto na akina mama ambao ndo wengi halafu haiba yao ya kitusi pure ikaja tunafanya aje? Tuwafukuze au tufanyeje tukampa taarifa rasmi balozi yeye akawa yupo ofisini anaongea na watu kwa sauti ya chinichini sanaa tukawa hatuelewi tukawa tumekaa tu yeye yupo ofisini. Sasa angalia cha ajabu.

Kulikuwa kuna walinzi wawili pale getini wa kampuni ya pale pale kigali ghafla bila kutarajia jamaa wakayeyuka ghafla haijulikani walienda wapi? hiyo wasiwasi wangu walihofia ile hali sasa tukabaki hatuna ulinzi geti jeupeeeeee....yani unajiingilia tu.

Kufika midaa kama saa kumi na mbili ikaja landrover(defenda)nyeupe ikiwa na tinted full ikapaki getini ilionekana kama imetokea safari, balozi akatoka akawapokea hao jamaa, mapande ya majitu yaliyoshiba yamejazia vizuri kabisa walikuwa 7 wakashuka na maboksi flani hawakutaka mtu yeyote awasaidie kushusha wakawa wameingia ndani sasa kukawa kuna Mazungumzo yanaendelea hatukuja nini kinaendelea. Usiku ukafika tukalala kuamka asubuhi hatukiwaona tena hao jamaa ikawa sasa kila mtu na hisia zake, ila kuna mfanyakazi akawa anasema amesikia ndani wanaongea kiswahili. Sasa ntaelezea baadae ni akina nani hao na tulikutana tena boda ya burundi na rwanda wakiwa full ..........


Itaendelea..... Jioni.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Okay... Tukutane jioni mzee baba.
Imeishia patamu sana.
 
Back
Top Bottom