Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Wengi wao walikuwa wabeligi na wafaransa kuna siku wao kwa wao walichapana uwanja wa ndege wa Kigali waziri wa ulinzi wa Rwanda kipindi hicho ndo akaingilia kati kusuluhisha ugomvi wao.sasa walinzi gani hao eti UNAMIR.
Hawa askari wa UNAMIR walikuwa wametoka nchi za Ulaya au hata waafrika walikuepo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi wao walikuwa wabeligi na wafaransa kuna siku wao kwa wao walichapana uwanja wa ndege wa Kigali waziri wa ulinzi wa Rwanda kipindi hicho ndo akaingilia kati kusuluhisha ugomvi wao.sasa walinzi gani hao eti UNAMIR.

Sent using Jamii Forums mobile app
Walichapana kwa karate na judo au kwa silaha za moto mkuu? Wakauana?
 
Baadae nilikuja gundua kuwa alikuwa anaongea na mkuu wa interahamwe ( jina lake nimelisahau jamaa babe liuaji hatari sijui kama bado lipo hai, kama bado yupo hai hajasakwa na kufikishwa ICC basi haina haja ya kuendelea kuwahukumu wengine) ila jamaa hilo ndo lilikuwa kama Li-mkuu la majeshi kigali nzima huyo ndo top akisema ua umekwisha akisema acha umepona, unajua mabalozi lazima wawe na koneksheni kubwa sanaa wakati mwingine kwa upande wa serikali, waasi (kama wapo) na wapinzani. Mtakufa wote lakini balozi atapona, atalindwa atasindikizwa na kuwekwa sehemu salama. Nyinyi mnahenyeka tuu na vipassport vyenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wa interahamwe alikuwa mfanyabiashara .aliitwa georgers rutaganda.alifariki mwaka 2010.alikuwa na ma godown ambayo vitu vilivyoporwa na interahamwe vilihifadhiwa humo.na ndie mfadhili wa chakula na vinywaji kwa mgambo wa interahamwe
Screenshot_20200306-232612_Google.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hhahhaa kwa kukufungua akili tu ,iko hivi kuna watu wazito walikuwa Dar es salam,Kampala,Kinshasa,na Nairobi wanaendesha hii vita.ndo maana baada ya vita kuisha wengi walikimbilia maeneo hayo wazito wa Kampala wakawa wameshinda game.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kauli zake ndio zilimuondoa huyo Rais...

Embu shusha mambo, watu wajifunze, hasa hiki chama tawala maana kimeanza kutengeneza matabaka baina ya watanzania...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom