Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Duh, wanasafari ndefu banyarwanda, ila wahutu waliwafyeka wenzao,,lazma hii chuki izidi kuku. Ukifuatilia historia watusi ndo walianzisha uhasama kwa kujimwambafai ilhal wao ni wachache. Sasa wenzao wakamaindi waktaka kujikomboa na utumwa na umwinyi wa hao jamaa. All in all mtusi ni mtata....mhutu nae ni mkatili sasa...ndo unataka umfute mwezako ktk uso wa ardhi. Hahaahah duh, hao jamaa walijengewa makambi hko Ngara saivi ni wamefungua mashyle na mavyuo., ngara pale 40% ya wakazi ni wanyarwanda. Unamkuta kabisa anasikiliza redio rwanda...sasa unajiuliza huyu nimtz kweli?
Sio kweli aliyeharibu ni mbelgiji soma historia yako vizuri
 
Ukifika Rwanda utaona kama nchi yenye utulivu wa kutosha. Hata uhalifu mkubwa kama ujambazi na uporaji wa kutumia silaha umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa,iliyobakia ni udokozi mdogomdogo tu.

Lakini ukiangalia kwa undani utagundua kua Rwanda kuna tension ya hali ya juu sana miongoni mwa raia wake. Ule utulivu na amani ni kama vimeshikiliwa na kamba nyembamba. Unahisi kwenye nyoyo za watu kuna kutokuridhika flani hivi na kilichokuwepo ni kuogopa mkono fulani wa chuma

Kwa maoni yangu Rwanda ya baada ya Kagame lazima iwe handled very careful vinginevyo kitanuka tena! Nilisafiri kutoka Kigali kwenda Goma DRC kupitia Gisenyi na pote upitapo na kuonana na watu na kuongea nao unahisi ni watu wenye wasiwasi sana na hasira! Tuiombee Rwanda yasijirudie yaliyopita
Hata uombe vipi mkuu,bila kujisahihisha hakuna kitu. KG hajafanya juhudi zozote za kuliweka hilo Taifa pamoja. Badala yake amekweza wa kabila lake kwenye madaraka makubwa ya nchi,hawa wengine wamepewa mifupa ya nchi wana kinyongo.

Kuliponya hilo Taifa ilitakiwa kg awaite pamoja mpaka waasi akae nao wapange namna ya kuliweka pamoja hilo taifa. Kitendo cha kuwafuatilia huko waliko wapinzani na kuwafutilia mbali ni uoga wa kike wa muda tu. Maana hapo unazidi kuchochea moto,yeye anafikiri atadumu milele. Naamini hawa wanaonyanyaswa hawako kimya,lazima nao wana mipango hata iwe ya muda mrefu hawezi kuvumilia kuendelea kuwa chini. Hatuombei ila muda utaongea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji857][emoji857][emoji857] Bado naiona pesa kwenye hii thread.. Mkuu Mungu akijalia uzima .. Na mipango ikampendeza, na mwisho kama wewe hautojali siku moja nitakutafuta.. Unless uwe haupo interested.. Tu make hii kitu iende Amazon.. Naamini kabisa pesa ipo hapa.. Trust me or not [emoji857][emoji857][emoji857]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaendelea...........

EeeeMRND ......eeeeee...MRND..eeeee..MRND ....eeeeee...MRnd.. ishaka rya banyarwanda , eeeee...eeee
Eeee MRN ishaka ryubumng'e na mahoro na majambele ya rubanda tweshe turagushigikie ...eeeeMRNd ikomera.×2

Huo hapo ni wimbo wa kinyarwanda wa chama tawala Cha MRND nikaona kabla hatujamalizana na rwanda wote muujue huu wimbo ,Kama nilivyosema mwanzoni kipindi hicho ulikuwa unapigwa redioni masaa 24 kwa siku hakuna kupumzika .nachotaka kusema hapa ni kwamba wimbo huo ulipigwa maksudi ili kuwakaririsha watu waamini kuwa hakuna chama kingine Cha kuwaletea maendeleo zaidi ya chama cha MRND na hakuna mbadala ,huu wimbo ulipigwa redioni Hadi wazungu wakawa wanaujua achilia mbali watoto ukabadilika ukawa Kama wimbo wa taifa yani unaweza kukamatwa na interahamwe ukalazimishwa uimbe huo wimbo Kama ukishimdwa unakula vibao vya kufaa mtu ikalazimika Sasa lazima kila mtu aukariri uujue angalau beti hiyo moja huwa si usahau Hadi Leo (matumiz mabaya ya redio yakawa yameniathiri ) haijalishi we ni mwenyeji au mgeni.imbaaa

Haya Sasa tumalize na Rwanda.......

Tukawa tumelala pale boda usiku asubuhi tukawa tunasogea kwenye kidirisha Ila uongo mbaya sikumbuki sawasawa Kama siku ile nililala usingizi au vipi huwa sina kumbukumbu sawasawa nilistukia tu kumekucha watu Wana nawa nyuso nami nikaenda kunawa uso tukawa foleni kugonga passports zetu kuwahi kupanda maroli upande wa pili ,taratibu zikakamilika

Saa mbili kamili nikawa tumeiacha ardhi ya Rwanda rasmi tunaingia ardhi ya Burundi nikasema ASANTE MUNGU ,safari ikaanza kwenda bujumbura safari ikaanza huku tukiwa na baadhi ya warundi tukawa tunapiga stori kuhusu zile maiti za mtoni usiku Ila wao wakawa wanasema zile maiti zimetoka mbali Sanaa vijiji vya mbali Burundi bado Hali sio mbaya Sanaa japo kulikuwa na tension kubwa rais wao nae alikuwa kwenye ndege iliyomuua rais wa Rwanda Habyarimana. nikajiapiza kuwa kamwe haitotokea Mimi nikanyage ardhi ya Rwanda Tena hadi nakufa hata Kama Vita itaisha nikaambiwa nirudi kazini tena ,hata ningeteuliwa kuwa balozi kamili na ndo ingekuwa mwisho wa hiyo kazi siko hiyo .( Ila miaka ya 2000' ) nilitembelea Kigali tena zaidi ya Mara mbili kibiashara lakini mwenyewe.)

tukaingia Burundi MAROLI yakaenda kupaki eneo la Gitega Kama sijakosea Ila ise nako kulikuwa na kituko ambacho kiliniacha hoi yani niliona magari kadhaa yanapishana mjini yakiwa na matundu ya risasi na polisi hawana time nayo magari ya raia tu nikawa nawaza hapaNapo sipo.tukalala asubuhi safari ikaanza rasmi kuelekea boda ya Tanzania tukavuka boda nikawa ndani ya motherland nikavuta pumzi ndefuu nikasema uuuuaaahhhhhh Asante mungu.
Kuna kitu sitaki kumaliza bila kukisema baada ya kumaliza kuvuka boada ya tanzania Kuna kamwendo kakutoka boda Hadi kuna sehemu madereva huwa wanakula na Kama kupumzika kunaitwa kwa MAMA SHILINGI Sina uhakika Kama bado kupo Kuna mgahawa hivi Sasa pale watu tukawa tunashuka ili kula nikakosa sahani ya kulia ya kuwekea ubwabwa ikabidi yule mama muuzaji anipe kikombe cha chai ili nitumie Kama Sahank na kweli nikachotewa ubwabwa nikawekewa nikawa na kula huwa nikikumbuka nachekaa sanaAaaaa...ubwabwa kwenye kikombe duuuhhh.

Nafikiri Sasa nikawa ndani ya Tanzania ..rasmi ya Rwanda yakawa yameishia hapo.

Sasa kwakuwa niliahidi kuwaletea stori yangu hadi kufika Tanzania,kuacha kazi,kujiingiza katika biashara ya chuma chakavu huko Zambia ,kufungwa jera Ndola n.k Basi niwaombe Kwanza nitengeneze simu yangu kwanza ikiwa imepona Basi ntaiendeleza Kama sehemu ya pili ya maisha yangu kujifunza tu.

Mwisho naomba niwashukuru wote kwa kunifuatilia,kunikumbisha,hata wale mliinidhihaki lakini mkawa mnanifuatilia Kiaina,Asante Sanaa..

Stori hii naamini itakuwa imewavutia wengi sio mbaya kuipeleka kokote Kama sehemu ya kujifunza lakini usisahau kutoa credit kwa Bossless mwenyewe ambae ndo mmiliki wake halali.

Asante kwa viewers na comments za kutosha. USIKU MWEMA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shkamoo kwako mkuu...
 
Asee nakumbuka miaka hiyo mimi na familia yangu tulikuwa tunaishi lusumo magereza mama yangu alikuwa ananipa maandazi najwenda kuuza benako na nikiuza nilikuwa nabeba dagaa wale wa mwanza ni maisha ambayo niliyazieya,hiyo vita imepiganwa nimeshuhudia miili ikipita mtoni pale darajani, kiukweli nina mshukuru sana Mama yangu mzangu Mungu amjaalie huko alipo RIP MUM., sahv na watoto na maisha ya naendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma hii story nikapitiwa na usingizi nimeota naswakwa mtaani kisa nakata watu mapanga... mimi mwenyewe sikumbuki tukio la kukata mtu ila nimeona damu nyingi sana na jinsi watu wanavyoniogopa na kunisimulia navyotisha hata mimi mwenyewe namejiona adui.

Sasa kuna majamaa wakawa wananilia mingo wanikate na mimi nashukuru ndoto imeisha na usingizi umekata sasa niko hapa kusubiria toleo jingine. Ila sitasoma tena hii nightmare muda mchache kabla ya kulala
 
wewe nae unapumbazwa unaonekana zuzu unakubali tu.
hivi na akili zako timamu (japo zipo robo kilo) unaamini kwamba eti commando mmoja ni sawa na wanajeshi 100!!!

kwamba risasi ikimpiga kichwani hafi?
kwamba gari lao likitupiwa grumeti halilipuki?
Ni grenade mama sio grumeti. Grumeti ni mto upo Serengeti.
 
Uzi umenifikirisha sana!!upande wa mama yangu asili yao ni wanyankole wa uganda!!Kwa sasa ni Wanyambo wa kule kaisho karagwe!!!Kuna vitabia fulani vya Roho ngumu huwa naviona na kujisikia na maringo kwa hawa ndugu zangu wa upande wa mama!!!naona sasa nimeridhika kiuchunguzi kuhusu kabila lao!!!
 
Well spoken kiongozi. Na nikwambie kitu mara baada ya ndege ile kushambuliwa na kuuawa kwa marais hao mtutsi yeyote aliyekuwa ughaibuni alifanya sherehe kubwa au ndogo, kwa uwazi au kwa usiri kufurahia tukio hilo.

Wiki chache sana kabla ya tukio la ndege kutunguliwa kulikuwa na mkutano mkubwa sana pale jijini Mwanza uliowakutanisha watutsi wote kutoka kanda yote ya ziwa. Mkutano huo mkubwa na wa aina yake ulifanyika pale Vijana Social Hall jirani na uwanja wa mpira wa CCM Kirumba. Lango kuu kulikuwa na udhibiti mkubwa sana na walioruhusiwa kuingia ndani ni watutsi pekee yake.

Hata hivyo mimi nikiwa nje nilibahatika kuwaona watu fulani watutsi waliokuwa wakiishi Mwanza kipindi hicho kwa kivuli cha wafanyabiashara na wengine watumishi wa serikali waliokuwa na nyadhifa kubwa kubwa kwenye taasisi mbalimbali za serikali wakihudhuria mkutano huo ulioashiria kwamba kuna jambo kubwa walikuwa wanapanga kulitekeleza, wanataarifiwa au kuwekana sawa. Kiufupi hakuna mtutsi yeyote aliyekuwa na umri wa zaidi ya miaka 18 ambaye hakuhudhuria mkutano huo pasipokuwa na sababu maalumu maana kulikuwa na uhamasishaji sana ili wahudhurie bila kukosa.

Baada ya vifo vya marais hao wawili, mauaji ya kimbari yaliyofuatia na baadae watutsi wengi kurudi kwao Rwanda, wengi wa watu hao niliowafahamu waliokuwa katika mkutano huo walipata nyadhifa kubwa kubwa katika serikali ya Rwanda.

Hata baadhi ya watu nchini (watutsi) waliokamatwa kwa kudaiwa kufanya sherehe za waziwazi kutokana na furaha waliyokuwa nayo baada ya kuuawa kwa marais hao, baadae waliachiwa huru kwa amri kutoka mamlaka za juu. Ndiyo maana kuna speculations za hapa na pale kwamba hata TZ kuna upande ilikuwa ikipendelea kwenye yale majadiliano yaliyokuwa yakiendelea ili kuleta muafaka wa amani/kiuongozi.
Mkuu nilielezwa na chazo cha uhakika kwamba hata kupanda ndege moja kwa Marais wa Burundi na Rwanda walishawishiwa na mtu unaeza kumuita "EXTREMELY INFLUENTIAL". Mtu mwenyewe ni Mtanzania ambae mpaka sasa hivi hakuna anaemzungumzia kua alikua na mkono kwenye machafuko yale na hatimaye kuingia madarakani RPF, ngoja niishie hapa
 
Mkuu nilielezwa na chazo cha uhakika kwamba hata kupanda ndege moja kwa Marais wa Burundi na Rwanda walishawishiwa na mtu unaeza kumuita "EXTREMELY INFLUENTIAL". Mtu mwenyewe ni Mtanzania ambae mpaka sasa hivi hakuna anaemzungumzia kua alikua na mkono kwenye machafuko yale na hatimaye kuingia madarakani RPF, ngoja niishie hapa
Huyo kiumbe mbongo bado yupo bongo?!
 
Back
Top Bottom