Intarahamwe utawajua tu, Safar hii ni jino kwa jino hatucheki na kima kama wewe.
Hv unaweza kuanza hesabu maiti wakati upo kwenye tension maswali mengine hayana maana.Hizo maiti kibao ni kama ngapi na ilikuwa ni akinanani kwa mlivyo waona
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli aliyeharibu ni mbelgiji soma historia yako vizuriDuh, wanasafari ndefu banyarwanda, ila wahutu waliwafyeka wenzao,,lazma hii chuki izidi kuku. Ukifuatilia historia watusi ndo walianzisha uhasama kwa kujimwambafai ilhal wao ni wachache. Sasa wenzao wakamaindi waktaka kujikomboa na utumwa na umwinyi wa hao jamaa. All in all mtusi ni mtata....mhutu nae ni mkatili sasa...ndo unataka umfute mwezako ktk uso wa ardhi. Hahaahah duh, hao jamaa walijengewa makambi hko Ngara saivi ni wamefungua mashyle na mavyuo., ngara pale 40% ya wakazi ni wanyarwanda. Unamkuta kabisa anasikiliza redio rwanda...sasa unajiuliza huyu nimtz kweli?
Hata uombe vipi mkuu,bila kujisahihisha hakuna kitu. KG hajafanya juhudi zozote za kuliweka hilo Taifa pamoja. Badala yake amekweza wa kabila lake kwenye madaraka makubwa ya nchi,hawa wengine wamepewa mifupa ya nchi wana kinyongo.Ukifika Rwanda utaona kama nchi yenye utulivu wa kutosha. Hata uhalifu mkubwa kama ujambazi na uporaji wa kutumia silaha umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa,iliyobakia ni udokozi mdogomdogo tu.
Lakini ukiangalia kwa undani utagundua kua Rwanda kuna tension ya hali ya juu sana miongoni mwa raia wake. Ule utulivu na amani ni kama vimeshikiliwa na kamba nyembamba. Unahisi kwenye nyoyo za watu kuna kutokuridhika flani hivi na kilichokuwepo ni kuogopa mkono fulani wa chuma
Kwa maoni yangu Rwanda ya baada ya Kagame lazima iwe handled very careful vinginevyo kitanuka tena! Nilisafiri kutoka Kigali kwenda Goma DRC kupitia Gisenyi na pote upitapo na kuonana na watu na kuongea nao unahisi ni watu wenye wasiwasi sana na hasira! Tuiombee Rwanda yasijirudie yaliyopita
Shkamoo kwako mkuu...Inaendelea...........
EeeeMRND ......eeeeee...MRND..eeeee..MRND ....eeeeee...MRnd.. ishaka rya banyarwanda , eeeee...eeee
Eeee MRN ishaka ryubumng'e na mahoro na majambele ya rubanda tweshe turagushigikie ...eeeeMRNd ikomera.×2
Huo hapo ni wimbo wa kinyarwanda wa chama tawala Cha MRND nikaona kabla hatujamalizana na rwanda wote muujue huu wimbo ,Kama nilivyosema mwanzoni kipindi hicho ulikuwa unapigwa redioni masaa 24 kwa siku hakuna kupumzika .nachotaka kusema hapa ni kwamba wimbo huo ulipigwa maksudi ili kuwakaririsha watu waamini kuwa hakuna chama kingine Cha kuwaletea maendeleo zaidi ya chama cha MRND na hakuna mbadala ,huu wimbo ulipigwa redioni Hadi wazungu wakawa wanaujua achilia mbali watoto ukabadilika ukawa Kama wimbo wa taifa yani unaweza kukamatwa na interahamwe ukalazimishwa uimbe huo wimbo Kama ukishimdwa unakula vibao vya kufaa mtu ikalazimika Sasa lazima kila mtu aukariri uujue angalau beti hiyo moja huwa si usahau Hadi Leo (matumiz mabaya ya redio yakawa yameniathiri ) haijalishi we ni mwenyeji au mgeni.imbaaa
Haya Sasa tumalize na Rwanda.......
Tukawa tumelala pale boda usiku asubuhi tukawa tunasogea kwenye kidirisha Ila uongo mbaya sikumbuki sawasawa Kama siku ile nililala usingizi au vipi huwa sina kumbukumbu sawasawa nilistukia tu kumekucha watu Wana nawa nyuso nami nikaenda kunawa uso tukawa foleni kugonga passports zetu kuwahi kupanda maroli upande wa pili ,taratibu zikakamilika
Saa mbili kamili nikawa tumeiacha ardhi ya Rwanda rasmi tunaingia ardhi ya Burundi nikasema ASANTE MUNGU ,safari ikaanza kwenda bujumbura safari ikaanza huku tukiwa na baadhi ya warundi tukawa tunapiga stori kuhusu zile maiti za mtoni usiku Ila wao wakawa wanasema zile maiti zimetoka mbali Sanaa vijiji vya mbali Burundi bado Hali sio mbaya Sanaa japo kulikuwa na tension kubwa rais wao nae alikuwa kwenye ndege iliyomuua rais wa Rwanda Habyarimana. nikajiapiza kuwa kamwe haitotokea Mimi nikanyage ardhi ya Rwanda Tena hadi nakufa hata Kama Vita itaisha nikaambiwa nirudi kazini tena ,hata ningeteuliwa kuwa balozi kamili na ndo ingekuwa mwisho wa hiyo kazi siko hiyo .( Ila miaka ya 2000' ) nilitembelea Kigali tena zaidi ya Mara mbili kibiashara lakini mwenyewe.)
tukaingia Burundi MAROLI yakaenda kupaki eneo la Gitega Kama sijakosea Ila ise nako kulikuwa na kituko ambacho kiliniacha hoi yani niliona magari kadhaa yanapishana mjini yakiwa na matundu ya risasi na polisi hawana time nayo magari ya raia tu nikawa nawaza hapaNapo sipo.tukalala asubuhi safari ikaanza rasmi kuelekea boda ya Tanzania tukavuka boda nikawa ndani ya motherland nikavuta pumzi ndefuu nikasema uuuuaaahhhhhh Asante mungu.
Kuna kitu sitaki kumaliza bila kukisema baada ya kumaliza kuvuka boada ya tanzania Kuna kamwendo kakutoka boda Hadi kuna sehemu madereva huwa wanakula na Kama kupumzika kunaitwa kwa MAMA SHILINGI Sina uhakika Kama bado kupo Kuna mgahawa hivi Sasa pale watu tukawa tunashuka ili kula nikakosa sahani ya kulia ya kuwekea ubwabwa ikabidi yule mama muuzaji anipe kikombe cha chai ili nitumie Kama Sahank na kweli nikachotewa ubwabwa nikawekewa nikawa na kula huwa nikikumbuka nachekaa sanaAaaaa...ubwabwa kwenye kikombe duuuhhh.
Nafikiri Sasa nikawa ndani ya Tanzania ..rasmi ya Rwanda yakawa yameishia hapo.
Sasa kwakuwa niliahidi kuwaletea stori yangu hadi kufika Tanzania,kuacha kazi,kujiingiza katika biashara ya chuma chakavu huko Zambia ,kufungwa jera Ndola n.k Basi niwaombe Kwanza nitengeneze simu yangu kwanza ikiwa imepona Basi ntaiendeleza Kama sehemu ya pili ya maisha yangu kujifunza tu.
Mwisho naomba niwashukuru wote kwa kunifuatilia,kunikumbisha,hata wale mliinidhihaki lakini mkawa mnanifuatilia Kiaina,Asante Sanaa..
Stori hii naamini itakuwa imewavutia wengi sio mbaya kuipeleka kokote Kama sehemu ya kujifunza lakini usisahau kutoa credit kwa Bossless mwenyewe ambae ndo mmiliki wake halali.
Asante kwa viewers na comments za kutosha. USIKU MWEMA.
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23]we Dada weweUnaandika ma-paragraph mareeeefu hata hayana maana.
Kuwa kama wanawake wenzako basi.
Bossless naomba msaada wako wa kitu ambacho ni critical. Unasema ulikuwa unafanya kazi ubalozini. Unamaanisha Rais Mwinyi hakutuma kikosi cha kuwarejesha nyumbani raia wake?Kwa taarifa yako Sina taaluma yeyote ya uandisha mnisamehe kwa hilo
Sent using Jamii Forums mobile app
Sioni sababu ya kuweka "ni" katikati ya sentensi, inatia kichefuchefu.Ahaa, nashkuru mzee wangu. Basi mm nakwambia haitofika 2050 bomu hilo la rwanda halijalipuka.
Wahutu walio wengi ni wanatanga tanga nchi jirani wakikimbia mkono wa PK, ukiachilia mbali dhana ya wengi kuongozwa na wachache.
Wewe ungali ni mtoto.
Ni grenade mama sio grumeti. Grumeti ni mto upo Serengeti.wewe nae unapumbazwa unaonekana zuzu unakubali tu.
hivi na akili zako timamu (japo zipo robo kilo) unaamini kwamba eti commando mmoja ni sawa na wanajeshi 100!!!
kwamba risasi ikimpiga kichwani hafi?
kwamba gari lao likitupiwa grumeti halilipuki?
Hujasema story mzee, kwa ile difenda ilikua na mapambo ndanBossless naomba msaada wako wa kitu ambacho ni critical. Unasema ulikuwa unafanya kazi ubalozini. Unamaanisha Rais Mwinyi hakutuma kikosi cha kuwarejesha nyumbani raia wake?
Mkuu nilielezwa na chazo cha uhakika kwamba hata kupanda ndege moja kwa Marais wa Burundi na Rwanda walishawishiwa na mtu unaeza kumuita "EXTREMELY INFLUENTIAL". Mtu mwenyewe ni Mtanzania ambae mpaka sasa hivi hakuna anaemzungumzia kua alikua na mkono kwenye machafuko yale na hatimaye kuingia madarakani RPF, ngoja niishie hapaWell spoken kiongozi. Na nikwambie kitu mara baada ya ndege ile kushambuliwa na kuuawa kwa marais hao mtutsi yeyote aliyekuwa ughaibuni alifanya sherehe kubwa au ndogo, kwa uwazi au kwa usiri kufurahia tukio hilo.
Wiki chache sana kabla ya tukio la ndege kutunguliwa kulikuwa na mkutano mkubwa sana pale jijini Mwanza uliowakutanisha watutsi wote kutoka kanda yote ya ziwa. Mkutano huo mkubwa na wa aina yake ulifanyika pale Vijana Social Hall jirani na uwanja wa mpira wa CCM Kirumba. Lango kuu kulikuwa na udhibiti mkubwa sana na walioruhusiwa kuingia ndani ni watutsi pekee yake.
Hata hivyo mimi nikiwa nje nilibahatika kuwaona watu fulani watutsi waliokuwa wakiishi Mwanza kipindi hicho kwa kivuli cha wafanyabiashara na wengine watumishi wa serikali waliokuwa na nyadhifa kubwa kubwa kwenye taasisi mbalimbali za serikali wakihudhuria mkutano huo ulioashiria kwamba kuna jambo kubwa walikuwa wanapanga kulitekeleza, wanataarifiwa au kuwekana sawa. Kiufupi hakuna mtutsi yeyote aliyekuwa na umri wa zaidi ya miaka 18 ambaye hakuhudhuria mkutano huo pasipokuwa na sababu maalumu maana kulikuwa na uhamasishaji sana ili wahudhurie bila kukosa.
Baada ya vifo vya marais hao wawili, mauaji ya kimbari yaliyofuatia na baadae watutsi wengi kurudi kwao Rwanda, wengi wa watu hao niliowafahamu waliokuwa katika mkutano huo walipata nyadhifa kubwa kubwa katika serikali ya Rwanda.
Hata baadhi ya watu nchini (watutsi) waliokamatwa kwa kudaiwa kufanya sherehe za waziwazi kutokana na furaha waliyokuwa nayo baada ya kuuawa kwa marais hao, baadae waliachiwa huru kwa amri kutoka mamlaka za juu. Ndiyo maana kuna speculations za hapa na pale kwamba hata TZ kuna upande ilikuwa ikipendelea kwenye yale majadiliano yaliyokuwa yakiendelea ili kuleta muafaka wa amani/kiuongozi.
Ni grenade mama sio grumeti. Grumeti ni mto upo Serengeti.
Duh yamekuwa hayo tena? Tatizo nini? Umeachika au hupati bwana?Grenade ni kiingereza chake. Grumeti ni tafsiri ya lugha mama. Acha utaahira.
Huyo kiumbe mbongo bado yupo bongo?!Mkuu nilielezwa na chazo cha uhakika kwamba hata kupanda ndege moja kwa Marais wa Burundi na Rwanda walishawishiwa na mtu unaeza kumuita "EXTREMELY INFLUENTIAL". Mtu mwenyewe ni Mtanzania ambae mpaka sasa hivi hakuna anaemzungumzia kua alikua na mkono kwenye machafuko yale na hatimaye kuingia madarakani RPF, ngoja niishie hapa