Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Ok then, sina hakika kama umeeleweka, ila Nakupenda Bure, You have the right mind and my God bless you.
Mkuu huwa napenda kulisemea kwani huwa nawashangaa watu wanaojiona keki wana kipi cha ziada
Ni kama maoni tu kwani lisipodhibitiwa lina nia ya kutugawa tu na si kutuunganisha...lina nia ovu...
Afterall ukishakua exposed na maisha unaelewa binadamu wote ni wale wale ni suala la watu wapewe exposure na nafasi to prove themselves....

mkoloni ndo kaleta maendeleo ya 'aina' flani ya 'kileo' africa
Hivyo waafrika wenyewe kwa wenyewe kujiona kuna classes ni uzwazwa...wa hali ya juu ...hakuna cha naturally gifted wala nini...wamevumbua nini kipya??..hapo ndo utaona ni advantage ya rule ya mkoloni ndo iliwaweka baadhi ya watu mbele kabla ya wengine sio kwamba wale wengine ni vilaza hamnaa ni fursa tuuu...ndo mana sikuhizi kabila zote wasomi na wafanya biashara wapo...it was just a matter of fursa!!

Kwa uelewa wangu mzungu hio ilikua ni strategy ya kutawala...divide and rule...watu anawavuruga weee huku ye anaendelea kupeta

ss shida ni pale alipoondoka
Ilipasea viongozi waweke sawa hio hali
Tanzania Nyerere alifanikiwa
Bila kuwadhibiti baadhi ya watu wangekua na nchi yao huku wakijiona wao ni elites...unadhani nini kingetokea iwapo ktk hio nchi wamemix na kabila ambalo sio elites kama wao?..by default wenye elimu ndo viongozi... hence kujiona keki ndo kunazaliwa hapo...wale waloachwa nyuma kidogo mfano wale 'wachunga ng'ombe' unadhani wangefanyaje kama sio kuwachabanga elites mapanga tu???!!!

nawasifu viongozi watanzania hasa nyerere ali'contain ukabila udini nk
Ndo mana hadi leo dini za kristo na islamzinapokezana vijiti urais hivyo kila mtu anajiskia anawakilishwa

likewise nyadhifa mbalimbali makabila yooote yapo kwa uchache tu
Magu Kanda ya Ziwa
Samia Zanzibar
Majaliwa kanda ya kusini
Baraza limemix watu kibao
Hivyo hakuna kabila linalojiskia wao wameachwa nyuma..likewise dini wanamix madhehebu yote

Shida Rwanda wachache tutsi bado serikali wanataka wengi wawe wao unafikiri wahutu wanafanyeje?....yanatokea yaliyotokeaa ndugu msomajii

Watu wakishakua exposed wanabadilika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes ni mtutsi pure kabisa wa western Uganda.
Tutsi wakiwa Rwanda na Burundi ila wakiwa Uganda ni Hima/Ankole, DRC ni Banyamulenge ama Hema/Bagegere.

So ni damu moja hao
Wakiwa Tanzania ni Wahangaza (Watusi + Wahutu wa Rwanda) na Waha (Watusi + Wahutu wa Burundi)
Japo pia kuna waha Asili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea kitu sahihi kabisa.

Mambo yaliyofanywa na interahamwe kule Rwanda ni sawa na yaliyofanywa na vijana wa imbonerakule pale Burundi.
Umenikumbusha buja nyuma ya makao ya cnddfdd (sien Dede efu dede) ipo hotel ya waziri mmoja kama sijakosea ni mwanamke nilifikia pale kipindi piere amekoswa kupinduliwa yupo jamaa alikuja pale tukawa tunakunywa nae alijitambulisha kwangu kama kiongozi wa Mbonerakure story zao zinatisha sana niwatu wasiokuwa na hofu ya kutoa uhai wa mtu hata kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachojua 100% ya rural areas Tz ni third world, nimeshatembea mikoa yote na bahati nzuri mimetembea nchi kadhaa za Ulimwengu wa Kwanza, ni kweli tuna safari ndefu, pengine kama mimi nimepata privilege jukumu langu ni kuinua wanaohitaji kuinuka walau wainuke, na si jiamini kuwa eti nipo Gifted, that's awkward, hata miji yetu 90% bado ni ulimwengu wa tatu sembuse vijijini?
Niseme tu, pasitokee mtu akajiona yeye au jamii yake ni Bora kuliko nyingine, hiyo ni dhana potofu na isiyo na mashiko, na ukiona mtu anaamini hivyo kwenye huu utandawazi basi tambua ako na some cognitive disorders,
Kwakweli umejikwaa kusema kuna jamii Gifted, inaonekana husomi vitabu, everyone is gifted.
Ni suala la Exposure tu kama alivyosema mkuu LadyRed
@LadyRed bwana, hili Jambo naona huwa unalizungumzia sana. Linakuumiza kwani? Ni kweli kuwa zipo jamii zilikuwa na privilege nyakati za mkoloni, ilà trust me nao walijiongeza sana tu, na wanazidi kujiongeza to-date. Zipo jamii hapa bongo hadi leo hii pamoja na fursa kuwa kwa kila mtu lakini bado they lag behind, hatuwezi kufanana na kuna watu naturally wapo gifted katika utafutaji na kusaidiana. Kuna sehemu leo hii ukienda vijijini japo ni afrika lakini hutaamini kuona palivyo, na kuna mahali ukienda unaweza kuishia kutoa machozi, ndani ya hii bongo.

So pamoja na privilege kuwepo kwa wote, kuna gifted hands, kuna watu wanabebana sanaaa, na wapo ambao hata dada mtu anaona wivu kwa mdogo mtu kuwin maisha.

Ya huko Rwanda siyajui sana, unaweza kuwa sahihi kwa analysis uliyofanya, ila kwa bongo mmmh.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachojua 100% ya rural areas Tz ni third world, nimeshatembea mikoa yote na bahati nzuri mimetembea nchi kadhaa za Ulimwengu wa Kwanza, ni kweli tuna safari ndefu, pengine kama mimi nimepata privilege jukumu langu ni kuinua wanaohitaji kuinuka walau wainuke, na si jiamini kuwa eti nipo Gifted, that's awkward, hata miji yetu 90% bado ni ulimwengu wa tatu sembuse vijijini?
Niseme tu, pasitokee mtu akajiona yeye au jamii yake ni Bora kuliko nyingine, hiyo ni dhana potofu na isiyo na mashiko, na ukiona mtu anaamini hivyo kwenye huu utandawazi basi tambua ako na some cognitive disorders,
Kwakweli umejikwaa kusema kuna jamii Gifted, inaonekana husomi vitabu, everyone is gifted.
Ni suala la Exposure tu kama alivyosema mkuu LadyRed

Sent using Jamii Forums mobile app
"Ako na some cognitive disorder"
Ndiyo nini hiyo "ako"!!!??? Acha ulimbukeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
shukrani sana ndugu. ..

ila ungejitahidi kujibu na maswali ya wadau ili tusibaki na kinyongo chchte
 
Pole sana Boss, tupo tayari kukuchangia ili mradi hii stori ifike mwisho. Pia nimegundua wewe ni mtu usiependa majivuno upo tofouti na watanzania wengi ambao wangepata exposure ulizopata wangekuwa na kauli za kejeli kwa baadhi ya member humu ndani pengine kususa kabisa kuleta muendelezo wa hii stori yako.

Hakika wewe ni mtanzania wa kipekee,tupo tayari kwa muendelezo, msalimie hapo shemeji.
Na tunamuheshimu sana shemeji yetu Happy womens day
 
Hii movie imetokana na story ya ukweli kabisa na wala siyo ya kutunga. Ingelikuwa ni ya kutunga starring asingemalizia kwa kushangaa kulia ubwabwa kwenye kikombe cha chai kwa mama ntilie. Badala yake angeliweka tukio kubwa la kusisimua sana ili kufurahisha genge. Tunamshukuru sana kwa kuwa mkweli na Mungu ambariki.
 
Ujinga wa hivi sisomi nimescroll hadi chini nashangaa kuona part 2 bofya link hii nikaachana nayo
 
Mkuu wale watu saba wenye Vumbi mpaka machoni kazi yao hasa unahisi ni nini?
Inaendelea...........

EeeeMRND ......eeeeee...MRND..eeeee..MRND ....eeeeee...MRnd.. ishaka rya banyarwanda , eeeee...eeee
Eeee MRN ishaka ryubumng'e na mahoro na majambele ya rubanda tweshe turagushigikie ...eeeeMRNd ikomera.×2

Huo hapo ni wimbo wa kinyarwanda wa chama tawala Cha MRND nikaona kabla hatujamalizana na rwanda wote muujue huu wimbo ,Kama nilivyosema mwanzoni kipindi hicho ulikuwa unapigwa redioni masaa 24 kwa siku hakuna kupumzika .nachotaka kusema hapa ni kwamba wimbo huo ulipigwa maksudi ili kuwakaririsha watu waamini kuwa hakuna chama kingine Cha kuwaletea maendeleo zaidi ya chama cha MRND na hakuna mbadala ,huu wimbo ulipigwa redioni Hadi wazungu wakawa wanaujua achilia mbali watoto ukabadilika ukawa Kama wimbo wa taifa yani unaweza kukamatwa na interahamwe ukalazimishwa uimbe huo wimbo Kama ukishimdwa unakula vibao vya kufaa mtu ikalazimika Sasa lazima kila mtu aukariri uujue angalau beti hiyo moja huwa si usahau Hadi Leo (matumiz mabaya ya redio yakawa yameniathiri ) haijalishi we ni mwenyeji au mgeni.imbaaa

Haya Sasa tumalize na Rwanda.......

Tukawa tumelala pale boda usiku asubuhi tukawa tunasogea kwenye kidirisha Ila uongo mbaya sikumbuki sawasawa Kama siku ile nililala usingizi au vipi huwa sina kumbukumbu sawasawa nilistukia tu kumekucha watu Wana nawa nyuso nami nikaenda kunawa uso tukawa foleni kugonga passports zetu kuwahi kupanda maroli upande wa pili ,taratibu zikakamilika

Saa mbili kamili nikawa tumeiacha ardhi ya Rwanda rasmi tunaingia ardhi ya Burundi nikasema ASANTE MUNGU ,safari ikaanza kwenda bujumbura safari ikaanza huku tukiwa na baadhi ya warundi tukawa tunapiga stori kuhusu zile maiti za mtoni usiku Ila wao wakawa wanasema zile maiti zimetoka mbali Sanaa vijiji vya mbali Burundi bado Hali sio mbaya Sanaa japo kulikuwa na tension kubwa rais wao nae alikuwa kwenye ndege iliyomuua rais wa Rwanda Habyarimana. nikajiapiza kuwa kamwe haitotokea Mimi nikanyage ardhi ya Rwanda Tena hadi nakufa hata Kama Vita itaisha nikaambiwa nirudi kazini tena ,hata ningeteuliwa kuwa balozi kamili na ndo ingekuwa mwisho wa hiyo kazi siko hiyo .( Ila miaka ya 2000' ) nilitembelea Kigali tena zaidi ya Mara mbili kibiashara lakini mwenyewe.)

tukaingia Burundi MAROLI yakaenda kupaki eneo la Gitega Kama sijakosea Ila ise nako kulikuwa na kituko ambacho kiliniacha hoi yani niliona magari kadhaa yanapishana mjini yakiwa na matundu ya risasi na polisi hawana time nayo magari ya raia tu nikawa nawaza hapaNapo sipo.tukalala asubuhi safari ikaanza rasmi kuelekea boda ya Tanzania tukavuka boda nikawa ndani ya motherland nikavuta pumzi ndefuu nikasema uuuuaaahhhhhh Asante mungu.
Kuna kitu sitaki kumaliza bila kukisema baada ya kumaliza kuvuka boada ya tanzania Kuna kamwendo kakutoka boda Hadi kuna sehemu madereva huwa wanakula na Kama kupumzika kunaitwa kwa MAMA SHILINGI Sina uhakika Kama bado kupo Kuna mgahawa hivi Sasa pale watu tukawa tunashuka ili kula nikakosa sahani ya kulia ya kuwekea ubwabwa ikabidi yule mama muuzaji anipe kikombe cha chai ili nitumie Kama Sahank na kweli nikachotewa ubwabwa nikawekewa nikawa na kula huwa nikikumbuka nachekaa sanaAaaaa...ubwabwa kwenye kikombe duuuhhh.

Nafikiri Sasa nikawa ndani ya Tanzania ..rasmi ya Rwanda yakawa yameishia hapo.

Sasa kwakuwa niliahidi kuwaletea stori yangu hadi kufika Tanzania,kuacha kazi,kujiingiza katika biashara ya chuma chakavu huko Zambia ,kufungwa jera Ndola n.k Basi niwaombe Kwanza nitengeneze simu yangu kwanza ikiwa imepona Basi ntaiendeleza Kama sehemu ya pili ya maisha yangu kujifunza tu.

Mwisho naomba niwashukuru wote kwa kunifuatilia,kunikumbisha,hata wale mliinidhihaki lakini mkawa mnanifuatilia Kiaina,Asante Sanaa..

Stori hii naamini itakuwa imewavutia wengi sio mbaya kuipeleka kokote Kama sehemu ya kujifunza lakini usisahau kutoa credit kwa Bossless mwenyewe ambae ndo mmiliki wake halali.

Asante kwa viewers na comments za kutosha. USIKU MWEMA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 1989 ma bus yalikua yanasafiri usiku mkuu,kuondoka dar ilikua ni kuanzia saa 10 jioni.
 
Back
Top Bottom