Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Haki vile nimecheka🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

I didn’t see this coming at all
You watch movies a lot, that’s a reason why🤣🤣🤣

Labda baada ya kujifanya kwamba hajui chochote kuhusu matumizi ya silaha za kivita baadae angeibuka ghafla na kushirikiana na wale makomandoo saba na hatimaye yeye kuwaua mainterahamwe kadhaa ikiwemo kiongozi wao aliyekuwa anakaribia kufyatua kombora la RPG kwa kiongozi wa makomandoo wetu. Baada ya hapo kwa kitendo hicho cha ujasiri kilichomfurahisha sana balozi wangekumbatiana, kubusiana nae balozi shavuni kisha kuagana kwa kupungiana mikono na wale watoto ili yeye aendelee na safari yake kurejea Dar huku balozi na wale watoto wawili wakibaki Burundi.
 
Nakumbuka mwaka 1994 baba yangu alikuwa na wenzie wakipeleka bidhaa Rwanda, alichelewa sana kurudi, ila siku aliporudi hakuwa na raha hata kidogo ila alirudi na pesa nyingi sana.

Huwa hataki kusikia mtu akisimulia tukio hili, yaani ilikuwa tukimuuliza ilikuwaje, mnamuona kainuka anaenda kulala, ila kuna siku alisema "Vita isikieni tu kwa wenzenu". Akainuka kwenda kulala.
Kwaiyo mzee mpaka leo ajatoa story
 
Nyerere alikuwa na wanajeshi wazuri sana! Sijui hawa wala vihepe wa sasa hivi tunaowaona huku mitaani.

Yani hapo unaweza kuta hiyo difenda ilitokea tz ikapita pori kwa pori hadi Rwanda

Sent using Jamii Forums mobile app

wewe nae unapumbazwa unaonekana zuzu unakubali tu.
hivi na akili zako timamu (japo zipo robo kilo) unaamini kwamba eti commando mmoja ni sawa na wanajeshi 100!!!

kwamba risasi ikimpiga kichwani hafi?
kwamba gari lao likitupiwa grumeti halilipuki?
 
Mkuu mshawishi mzee nae aje amwage yake hapa
Nakumbuka mwaka 1994 baba yangu alikuwa na wenzie wakipeleka bidhaa Rwanda, alichelewa sana kurudi, ila siku aliporudi hakuwa na raha hata kidogo ila alirudi na pesa nyingi sana.

Huwa hataki kusikia mtu akisimulia tukio hili, yaani ilikuwa tukimuuliza ilikuwaje, mnamuona kainuka anaenda kulala, ila kuna siku alisema "Vita isikieni tu kwa wenzenu". Akainuka kwenda kulala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaendelea...................... 49k viewers si mchezo.

Haya sasa tusonge mbele tarehe, saa, sekunde za malaika mtoa roho zikawadia 6/04/1994. Saa tisa usiku tukaashuhudia kitu kama kimondo kikishuka ardhini ila kikapotelea vichakani kwa mbali nje ya mji. kutokana na kishindo chake pale ubalozini kila mtu aliamka lakini hakuna aliejua hasa ni nini, tukachukulia kawaida tukajua ni yale yale kila siku si tumeshaanza kuzoea watu wakaendelea kuchapa usingizi nawanaume wakaendelea kulinda getini.
Asubuhi mapema tukashudia hali ya ajabu ambayo sijawahi kuiona katika maisha yangu, yani kukatokea kitu kama wingu hivi yanii mtu akisimama mitaa tano au kumi kutoka ulipo huwezi mtambua vizuri hadi awe karibu sanaa. Wenye redio wakafungulia redio zao kusikiliza , ikumbukwe kuwa kipindi chote wapiga mayowe wa propaganda redioni walikuwa hawaongee ulikuwa unapigwa tu muziki wa chama ila alfajiri ikasikika wimbo wa taifa ndo unapigwa watu wakabaki wanashangaa halafu unakuwa unajirudia .dalili ya kitu kibaya ikaanza kuhisiwa kigali yote kimyaa.....

Tukawa sasa tunaingia tarehe yenyewe 7/04/1994 harufu ya damu ikawa inasikika kigali nzima, makelele ya maumivu ya watu yakawa yanasikika kwa mbali kutoka hapo ubalozini ,balozi ndo akawa ametoka kututangazia kuwa sasa hali si nzuri rais habyarimana ameuawa ile kusema tu vile watu wote akili zilituruka wengine wakawa kama wanataka kukimbia hovyo wanaume ikabidi wafanye kazi ya ziada kwani kitendo cha kutoka nje ya ubalozi kingeleta maafa makubwa sanaa. Ila wote pale picha iliyotujia kichwani ni kwamba sasa tunakufa hakuna tena msalie mtume.

Swali likaja nani kamuua rais? Hakuna mwenye jibu. Aise kuna wimbo moja hivi ukiimbwa unakuwa kama vile unaomboleza unafanafana na ile ya Kimasai ukawekwa kwenye radio ukawa unapigwa huku unamtaja rais kuwa ameuliwa na Ng'otanyi(waasi wa kitusi) aisee vita ikawa imeanza rasmi hata balozi sasa akawa hatoki tena tukakaa wote mle ndani hakuna kutoka kufuata chakula wala nini.

Siku ya kwanza mitaa kelele kila upande, sasa interahamwe wakaanza kuvamia hadi balozi za jirani ambao walikuwa wameondoka walinzi wao wakakimbia watu wakazidi kuuawa. chakula pale kwa ni uji tu hakuna sukari wala nini, unajua kama upo vitani mara nyingi unakuwa husikii hamu ya kula na unajiona uko powa tu kumbe unazidi kuisha ( kama kuna mtu alipigana vita humu ya kagera atadhibitisha hilo) halafu unaweza shanga kumekucha ghafla kiza kimeingia ghafla usiku mnalala usingizi wenye wa mang'amung'amu tu.

Balozi zikawa zinaendelea kuvunjwa siku zinaenda magrounet yanarushwa hovyo hovyo risasi zinalia zikitulia labda nusu saa zinaanza tena,unajua rwanda ni milima sasa unaweza kaa usiku unaona roketi inarushwa kutoka upande moja kwenda upande mwingine vimulimuli tu vya moto hadi kuna kucha kelele na risasi zinaanza tena. Sasa ikawa dhahiri kuwa hakuna namna tumuachie mungu tu.

Lakini wakati huo balozi alikuwa kwenye chumba kimoja kati vile vyumba vya sili nilivyosema hapo awali sijui alikuwa anafanya nini , ikafika ya kumi sasa ikawa hakuna kitu tena njaa tupo katikati ya vita mjini umezungukwa na wanajeshi wanapigana live bila chenga jiona ya siku hiyo ndo wakaja wanajeshi wa rwanda ,na toka siku ile ndo niliwaona live wanajeshi wa rwanda majitu yamepanda sura ngumu macho mekundu wakaja na maroli yale 24 na ile defender nyeupe ila waliokuwa kwenye ile defender hawakushuka tukaitwa uwani ubalozini .balozi akatoa tamko akasema SAFARI YA KUWAONDOA KIGALI WATANZANIA NDO IMEFIKA NA KAMA HUNA PAPER ( PASSPORT ) TAFADHARI USIPANDE KWENYE ROLI UKIPANDA LIKALOKUTOKEA MBELE USILAUMU MTU. hii kauli aliitoa kwa uchungu na kwa msisitizo sanaa huwa siisahau maishani mwangu. .

Hapo sasa ndo ngoma ikawa ngumu kila mtu akamkimbilia balozi kuomba amsaidie mkewe na watoto wake, balozi akagoma kabisa wengine akawa anawajibu kama unampenda mkeo baki nae hapa aisee watu wakawa kama vile wamepagawa maroli yapo nje lakini unashindwa kwenda kulipanda paper huna , sasa kuna kisa kimoja kilichojitokeza sintokuja kukisahau.kuna mama wa kinyarwanda mtusi alikuwa na bwanake mtanzania amezaa nae ila yeye kipindi cha vita alikuwa ameleta mzigo tanzania ,hivyo ikabidi mama ajitoe mhanga akamuita balozi awachukue wale mabinti wake mapacha wawili walikuwa kama na miaka 14 hivi weupe pua za kitusi kabisa balozi akakubali mama akabaki ,sasa tutaona mbele walivyotaka kuleta kizaazaa nusu tuchapwe RPG kwa sababu yao.

Sasa tukawa tumejipakia kwenye roli wengine wasio na vibali wakawa wamebaki pale hapo ubalozini, hapo hakuna kusikitikiana mnapeana mkono wa kwaheri basi safari ikawa imeanza na escot ya wanajeshi wa rwanda ,vizuizi kibao tukifika kwenye vizuizi wanashuka wanaenda wanajeshi wenyewe wanavitoa tunapita ,cha ajabu vizuizi vingine vilikuwa havina hata watu sijui walikuwa wakajificha au vipi.

Sasa wakati vita imepamba moto Tanzania wakawa wamefunga mpaka wake na rwanda Ikatulazimu kupitia boda ya burundi sasa kimbembe ndo kikaanza hapo, kuna wilaya kama tatu inabidi upite ndo ufike boda ya Burundi na rwanda kama sijakosea kwa kutokea kigali lazima upitie province ya butare halafu ya Gitarama ya mwisho nimeisahau kitambo sanaa. Sasa province Butare (wenyewe wanaita) ili ufike lazima uvuke mto fulani mkubwa unaitwa Nyabarongo kuna daraja kubwa hivi linalounganisha kigali na hiyo wilaya hapo sasa ndo niliona mchezo wawale jamaa saba wa defender hapo tunaenda lakini magari yanakanyaga maiti barabarani maiti zimezaga kila kona. Ile tunashuka kilima kidogo inakaribia kuulifikia kama kilomita tatu hivi wale wanajeshi wa rwanda wakageuka na gari lao ghafla wakarudi nyuma moyo ukapiga paaahhh nikahisi kuna kitu si chakawaida unageuzaje gari ghafla unarudi kwanini usituache tuvuke ndo urudi aisee.

Mbele tena kidogo ile defenda ikasimama katika ya barabara hakuna gari kuendelea kupita magali yakawa yamesimama tu ile defenda ikawa inaendelea kusogea mbele sisi tumeambiwa tusimame hapo hapo hadi Difenda itakaporudi kutoruhusu tuendelee tukawa tu pale na madereva kila mtu kwenye Kibini wengine kwenye bodi nyuma kimyaaaaaa...


Kama lisaa hivi tukasikia risasi zinalindima vibaya Sanaaa yani ikawa dhahiri kama mbele yetu kama kilomita moja watu wanapigana lisasi live ila hatuoni tatizo la rwanda mapori na vichaka vingii ila risasi zikawa zinalia kama zipo chumbani nikasema sasa huu ndo mwisho wetu.

Mwisho lisasi zikakoma tumekaa kama nusu saa hivi defenda hairudi na risasi hazisikiki tena Mwisho balozi akaamuru tuendelee na safari bila defenda dahhh ile tunafika darajani maiti kibao zimelala hapo ila hakuna defenda tukawa tunaendelea na safari tu.

Sasa tukawa tunakaribia kuimaliza province ya Butare sasa hapo ndo kulitokea kizaazaa cha wale mabinti aise tulikuta bonge la kizuizi...... Na maenterahamwe mchanganyiko na wanajeshi wa rwanda aise........ Nikasema. Sasa tunakufa.................................

Itaendelea...........................................

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo maiti kibao ni kama ngapi na ilikuwa ni akinanani kwa mlivyo waona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uongo mkubwa + imani potofu.
kwamba commando akipigwa risasi ya kichwa hafi. Risasi inadunda!!!
Nani huyo kusema komando akipigwa risasi inadunda?
Mbona Tz tuna historia ya kupoteza makomando zaidi ya miwili kwenye mapambano i.e
Na yule Lima Tango tuliyempoteza Congo wakati tunapambana na MR21 sio komando?
Ni ipo hiyo imani potofu unayoiongelea wewe?
 
Nyerere alikuwa na wanajeshi wazuri sana! Sijui hawa wala vihepe wa sasa hivi tunaowaona huku mitaani.

Yani hapo unaweza kuta hiyo difenda ilitokea tz ikapita pori kwa pori hadi Rwanda

Sent using Jamii Forums mobile app
Mafunzo na yale yale mkuu na wanaiva na kufuzu mpaka kuona wamevaa zile badge za Military Special Unit.
l
 
Mkuu mshawishi mzee nae aje amwage yake hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani kama alishindwa kuisimulia familia yake aliyokumbana nayo huko Rwanda ndiyo atakuwa tayari kuja kukusimulia wewe mtu baki? Pia huwezi jua zile pesa nyingi alizorudi nazo alizipataje kati kati ya mauaji/vita maana kumbuka kutokana na simulizi ya babu hapo kipindi hicho ilikuwa ni biashara ya kubadilishana bidhaa kwa bidhaa na siyo bidhaa kwa pesa. Sasa huyo hizo pesa alizipata kwa kufanya biashara gani? Inabaki siri yake.
 
Nani huyo kusema komando akipigwa risasi inadunda?
Mbona Tz tuna historia ya kupoteza makomando zaidi ya miwili kwenye mapambano i.e
Na yule Lima Tango tuliyempoteza Congo wakati tunapambana na MR21 sio komando?
Ni ipo hiyo imani potofu unayoiongelea wewe?

sasa unapo shadadia kuwa eti commando mmoja ni sawa na wanajeshi 100 unakua na akili timamu kweli?
 
Nyerere alikuwa na wanajeshi wazuri sana! Sijui hawa wala vihepe wa sasa hivi tunaowaona huku mitaani.

Yani hapo unaweza kuta hiyo difenda ilitokea tz ikapita pori kwa pori hadi Rwanda

Sent using Jamii Forums mobile app
Wale walikua watu wa kazi wanarekebisha huku wanatungua huku. Hali ilishaeleweka mapema kipindi kile kwamba kitanuka huko ndo wakapelekwa wale kulinda mpaka na kupiga ile mambo yenu yaishie hapo msilete kwetu huku. Ukibisha tuna wewe
 
Hivi hakuna mtu amekumbana na Mtutu wa Charles Taylor
Taylor ni mzuri kwa hiyo fani bunduki sana.
ila kilichotokea Rwanda usipime. Jamaa wanasema usipoteze muda na risasi kata miwa tu fasta. Hapo ni mapanga shaa, jembe la kichwa, nyundo sekunde tu watu hao wamemaliza kazi wanaangalia next station. Unakuta wanapigiwa call inyenzi wako 200 shule flani nendeni kazini unaambiwa wakifika pale hamna maswali.
Kwa kweli watusi wana haki kuhate hao jamaa interahamwe.
Ile hata mjerumani alichofanya Auschwitz haifiki.siku 100 tu mtu milioni+ ziliondoka
 
Taylor ni mzuri kwa hiyo fani, ila kilichotokea Rwanda usipime. Jamaa wanasema usipoteze muda na risasi kata miwa tu fasta. Hapo ni mapanga shaa, jembe la kichwa, nyundo sekunde tu watu hao wamemaliza kazi wanaangalia next station.
Kwa kweli watusi wana haki kuhate hao jamaa interahamwe.
Unavosema watusi wana haki ya kuwachukia intarahamwe ambao ni wahutu, kumbuka watusi nao walikua wanawaua wahutu kwa kutumia vkundi vyao vikiongozwa na RPF.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kagame hakujipanga "msituni" bali alikua na back up ya serikali za kitutsi za Uganda na Burundi ambao pia baada ya kushika hatamu walimsaidia kuwateketeza wahutu waliokimbilia huko DRC.

Wahutu changamoto ni kwamba hawapo organized wala kimkakati kila mtu anapambana kivyake sasa ambacho wanaweza ni kutumia back up ya serikali za kihutu mfano Nkuruzinza na walitakiwa wahakikishe DRC anashinda mtu ambaye hayuko puppet wa Kagame!! Wamechelewa sana.

Maana kagame wakimvamia tu Museveni na Magu watamsaidia so watafeli!! Hapo bado DRC itawafukuza..... Ila kagame na watutsi walikua makini kabla ya uvamizi wanahakikisha serikali za jirani zipo mfukoni.

Hata alopovamia wahutu DRC alihakikisha ameshaongea na kaunda wa Zambia na Dos santos wa Angola kuwa wasiingilie vita. Sasa wahutu hawana ushawishi huo kwenye serikali zetu hivyo vita itakua ngumu sana

Fursa yao pekee ni kuhakikisha Nkuruzinza hatolewi kwa gharama yoyote lasihivyo ndio utakua mwisho wa ndoto zao kurudi Rwanda.
Hiv Burundi kuna wahutu Tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taylor ni mzuri kwa hiyo fani bunduki sana.
ila kilichotokea Rwanda usipime. Jamaa wanasema usipoteze muda na risasi kata miwa tu fasta. Hapo ni mapanga shaa, jembe la kichwa, nyundo sekunde tu watu hao wamemaliza kazi wanaangalia next station. Unakuta wanapigiwa call inyenzi wako 200 shule flani nendeni kazini unaambiwa wakifika pale hamna maswali.
Kwa kweli watusi wana haki kuhate hao jamaa interahamwe.
Ile hata mjerumani alichofanya Auschwitz haifiki.siku 100 tu mtu milioni+ ziliondoka
Ila kuua watu 500,000+ kwa panga, nyundo, rungu sio mchezo. Hawa jamaa walichafukwa na nini hivi? Hata kama propaganda zilikua za kiwango gani?

Hii unaweza ikawa rekodi ya dunia nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom