Barrier hazikuwa nyingi kihivyo zilikuwa mbili tu na maaskari walikuwa wanahangaika na malori kuliko hivyo vigari vidogo vya abiria.
Halafu napata mashaka kama kweli ulikuwa nimwanabarozi,kujua vizuizi vilivyopo kasumbalesa mpaka Lubumbashi kote huko ulifuata nini tena na gari wakati ubalozi upo kinshasa maelfu ya km kutoka mpaka wa Zaire(Kongo) na Zambia.
Mi nadhani useme ukweli tu kwamba wewe ni wa malori mwenzangu sio dhambi.
Na sisi watu wa malori tuna exposure kubwa zaidi kuliko wapanda ndege hivyo usione haya kusema wewe ni dereva.
Pia wakati wa machafuko nyie mnaojiita mabalozi mlijifungia ktk balozi zenu sisi baadhi yetu ndio tuliotekwa nyara tukazuiwa,bidhaa zikaibwa na baadhi ya nyakati tulishuhudia live watu wakiuawa. Na ukiruhusiwa kurudi kwenu unakuta maiti zimezagaa barabarani,mwanzoni tulikuwa tunazisogeza kwa kuzipa heshima ya kibinadamu lakini kwa jinsi zilivyokuwa nyingi tukawa tunazikanyaga tu.
Sent using
Jamii Forums mobile app