Kitu nimejifunza hadi sasa:
1. Kutajwa kwa Dar, Nairobi, Kampala, Kinshasa, Ufaransa, Ubeligiji na Marekani, ni dhahiri vita haikuwa ya watusi na wahutu peke yao. Majabari ya vita hiyo yalikuwa nje ya Rwanda.
2. Vita si ya kujaribu kabisa kwani shetani hufanya kazi mwenyewe badala ya kuwatuma wasaidizi wake.
3. Kwamba malori yalipita juu miili ilozagaa barabarani, ni ishara kuwa mapigano Rwanda yalifikia hatua ambayo pengine ulimwengu haukuelezwa ukweli wa kilichoendelea huko na hivyo kukosa usaidizi stahiki wakati muafaka.
4. Ubalozi wa Tanzania kuwa kimbilio, na kutoshambuliwa kama ilivyokuwa kwa balozi nyinginezo kunatia mashaka iwapo hatukuwa washirika muhimu katika vita hiyo.
5. Media, hasa redio ni chombo hatari mno kikishindwa kufuata misingi bora ya kiutendaji.
Mwisho kuliko vita ije hapa kwetu bora CCM watawale milele.
Sent using
Jamii Forums mobile app