Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Lakini ajabu dunia ilifahamu ikapuuza. Bikira Maria hadi alitokea kuonya kinachokuja lakini wale mabinti waliotokewa walipuuzwa! Ila yale mauaji ya Rwanda sijui nini kiliikumba dunia!

Sent using Jamii Forums mobile app
Bikra Marium aliwezaje kuwa bikra wakati alikiwasha jifungua mtoto Yesu apo tarehe 25 desemba? Na inasemekana Yesu alikuwa na wadogo zake pia..

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli angemtaja tu angalau tumpongeze ukizingatia kuwa huyo balozi alikuwa ni mwanamke na leo ni siku ya wanawake duniani. Huyo mwanamke ana ujasiri wa ajabu kupita hata wanaume wengi wa kutoka pande hizo tuliowazoea kuwaona na kuwasikia kwamba ni wapenda ulojo.
Mkuu ingia google utamjua tu

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Vita ya Rwanda,.nlikuwa kigoma at that time,nlipokuwa Ni karibu na mpaka waburundi,nlikuwa Kama na miaka sita hivi, origin ya waha wengi wa mipakani huwa na asili ya either tutsi au hutu.kwetu ilikuwa Ni tutsi nakumbuka mida ya jioni walikuwa wakifungulia redio kusikiliza BBC ilikuwa Kama wanafatilia matangazo ya mpira

ilikuwa ikitangazwa idadi ya wahutu waliokufa Ni wengi kuliko watutsi Basi nyumba nzima ilikuwa inaripuka kwa shangwe
miaka kadhaa baadaye ndio nakuja kujua kwamba ilikuwa Ni Vita ...nkaanza kupata picha halisi ya uadui uliokuwapo Kati ya mtutsi nA muhutu,...yani mtu anashangilia kifo Cha mwenzake Kama timu yake pendwa imepata goli
nmecheka kama mazuri
imagine ushabiki wa mpira ukawekwe kwenye maisha ya watu
dunia ina matukio ya kutisha sana
 
"....Wakati mambo yanaenda kombo kuna wajinga wa chama tawala ikiwemo watangazaji, viongozi wa dini na wazee wenye ushawishi walikuwa wanaitangazia dunia kupitia redio Rwanda ipo salama hakuna chochote kibaya kinachoendelea kwani amani imetawala kabisa....."

Sentensi hiyo inafikirisha kweli kweli.
Ndio kitu kilikuwa kinaasisiwa na Magufuli na genge lake kina sabaya, makonda, musiba, kheri James na wengine 🥺🥺

Hatari sana
 
huu wimbo ulipigwa redioni Hadi wazungu wakawa wanaujua achilia mbali watoto ukabadilika ukawa Kama wimbo wa taifa yani unaweza kukamatwa na interahamwe ukalazimishwa uimbe huo wimbo Kama ukishimdwa unakula vibao vya kufaa mtu ikalazimika Sasa lazima kila mtu aukariri uujue angalau beti hiyo moja huwa si usahau Hadi Leo (matumiz mabaya ya redio yakawa yameniathiri ) haijalishi we ni mwenyeji au mgeni, imbaa

Aisee, nimecheka sana mkuu. Kuna aina ya ujinga huwa unakuwepo kwa wanajeshi hasa vitani. Mpaka wazungu ikabidi waukariri wimbo wa MRND na ukute ulikuwa na melody mbaya kinoma 😄😄
 
Inaendelea .............

Tulipoishia Sasa tukawa tumefikia kuimaliza province ya Butare hapo ndio tukakuta kizuizi interahamwe kibao kama Mia mbili hivi na kila mtu na panga wengine wamebeba RPG wengine vibomu vya Mikono halafu pembeni Kuna maiti kibao, Sasa kilichonistua zaidi maeneo yale kulikuwa na maiti mbili za wazungu nahisi atakuwa mke na mume, Sasa nikajiuliza kama hawa wazungu wameuawa sisi ni akina nani tusiuawe. Ikawa Sasa magari yamesimamishwa .

Sasa nikawa nawaza hivi lile defender limeenda wapi na wale jamaa hapa siwangesaidia au katika mapigano Yale pale darajani limeangukia mto Nyabarongo. Sasa hapo ikawa ni kushuka wote hakuna Cha dereva wala utingo unazima gari chini maroli 24 yote watu tukawa chini jamaa wanaimba nyimbo zao za chama mapanga juu yanalia tu nguo zao zimejaa damu nikajisemea sasa tumekwisha ikabidi balozi atoke kwenye gari lake aje nyuma kwenye maroli.

Sasa ikawa tumepangwa kwenye mstari unanyanyua passport yako juu huna unakaa pembeni, Kama unakumbuka kuna watu nilisema wakati tunavuka daraja walikuwa wanapanda maroli ya nyuma nao walikuwa wanakimbia Kigali sasa ikaja kimbembe kumbe hawana karatasi (passport) Ila ni wanyarwanda aise wakawa wanawekwa pembeni tu haijalishi ni mtusi au ni mhutu

Sasa hapo likaja swali wakawa wanaulizwa wale jamaa kwanini mnakimbia wakati nyinyi ni wahutu kwanini msibaki mpambanie nchi yenu wakawa wanajitetea tu aise likatokea jamaa likamkata na panga moja wapo miongoni mwa wale eneo la shingoni damu ikaruka aise mwili wangu haujawahi kufa ganzi Kama siku ile (Kuna kitu nimejifunza na kimekuwa kikijadiriwa Sana humu binadamu anapokaribia kufa huwa hasikii maumivu yeyote huwa anakuwa Kama amepigwa na ganzi Kama tutaendelea kunifuatilia nitaelezea tukio lilonitokea nikiwa nikiwa jela Ndola-Zambia baadae sana, msistuke nimeshafungwa jela miaka mitatu kisa biashara za chuma chakavu) tuendelee...

Sasa Yule mtu aliepigwa panga akawa amedondoka anakoroma Kama mbuzi aise kwa kweli pale akili iliondoka kidogo nikawa kama nimehama ulimwenguni kwa sekunde kadhaa hapo wote passport zipo juu yaani unanyoosha Mikono na passports jamaa linapita linakagua aise ikawa huku Zoezi la kuwasurubu wale wahutu wengine likiendelea Sasa Kuna watu sijui ni ndugu wale nao walikuwa wamedandia roli wakawa chini pamoja nasi yule mkubwa akapewa panga amkate yule mdogo shingoni ikawa jamaa anasita sita wakasema Sasa tunawaua wote si hutaki, pale pale yule mkubwa akampa mpanga yule mdogo halafu alikuwa amevaa Sweta zile zenye kofia akaivua akakunja shingo akamwambia yule mdogo piga shingoni ikawa Kama anasita Ila Kaka mtu akamwambia piga yule dogo akapiga kweli damu ikaruka hadi nilipokuwa nimesimama Hadi matonetone yakawa yamechafua kidogo suruali niliyokuwa nimevaa aise jamaa kadondoka mzima mzima paaaa...

Sasa hapo balozi anaongea na lile jamaa lililoonekana Kama ndio kamanda lao Ila likawa Kama halina time nae vile nikajisemea Leo hatutoki, majamaa yanapanda kwenye maroli yanachukua kila kitu kilichokuwemo mikate, nguo, viredio, majiko na masufuria ya kupikia


Sasa hapo tukawa njia panda. Sasa wakati lile njembaa linakagua aise likafika kwenye gari ya balozi likawaona wale mabinti aise acha liwachomoe unaujua ile gari ya balozi Ilikuwa na tinted hivyo alivyoshuka aliwaacha, watoto wakachomolewa wakavutwa nywele Kama kuku vile unavyomtoa bandani ikawa Sasa mzozo kila interehamwe anataka awavute ikawa mzozo mabinti wale wakawa katika ya msitu wa wauaji

Mwanzoni nilisema Kuna matukio mawili ambayo Aliyafanya balozi Hadi nikamvulia kofia nimetaja la kwanza pale ubalozi, Sasa Hili ni la pili yule mama (balozi) alichomoka pale pale alipokuwa akaingia katikati ya msitu wa wale jamaa akawa anavutana nao yaani anawavuta wale watoto na wale interehamwe wanawavuta wale watoto sasa ikawa vurugu tupu ikabidi wale watoto wawe wamemuinamia balozi tumboni Kama vile kuku anae atamia, uongo mbaya siku ile ndio nilimchukia balozi wangu yani nilimuuona Hana maana kabisa yaani kwa kitendo kile alichokuwa amekifanya nilijua Sasa anaamsha hasira za interahamwe Sasa tunakufa wote. Dhana ya kuogopana ikawa imechukua nafasi tumefikia mwisho wa uharibifu kila mtu anatetea nafsi yake (nikaona Bora angeacha tu wauawe wale mabinti sisi tuendelee na safari yetu mungu anisamehe ila mawazo hayo yalikuwa Bora kuliko kitu chochote kwa wakati ule)

Mama kakomaa aise lile jamaa likawa limefika pale, balozi kishati chake kimechanwa imebaki sidiria tu na alivaa sketi mama kakomaa lile jamaa likatoa sauti kwa kinyarwanda REKAA hiyo sauti huwa siisahau (maanake nafikiri ni achaa) Sasa wakati anasema vile kuna tukio lilienda sambamba na ile sauti nusu tufe aise.

Unajua roketi ya mkono RPG ukiwa umeibeba lazima uelekeze juu Sasa Kuna interahamwe moja sijui Ilikuwa aje, unajua Hawa hawana mafunzo wameokotwa tu mitaani aliishika Kama vile kashika bunduki ya kawaida Sasa wakati wa vuta ni kuvute sijui lilishika kwenye triga chuma ikachomoka ikapita katika ya watu, ikapita katika ya roli na gari ya balozi tukasikia mripuko aise kila mtu pale alichanganyikiwa yanii ni moshi mtupu Sasa ikawa haijulikani imetokea wapi imerushwa au imekuwaje Tena?

Intetahamwe wakasambaa wengine wakawa wanakimbilia mabondeni, kama dakika kumi zikapita tukawa tumepowaa kidogo Ila kelele tupu lile jamaa likamsogelea balozi likamuuliza hao ni akina akasema wanangu unajua balozi alikuwa mweupe na wale watoto walikuwa weupe kwa struggle ile lile jamaa halikutia shaka tena, mwanamke kumpigania mtoto namna ile hata wewe huwezi kataa kuwa sio mwanae Sasa hapo tukawa tumetulia kidogo jamaa wakaturuhusu safari ikaanza hapo watanzania watupu wale wadandiaji wote walishushwa sijui kilichoendelea nyuma Sasa tukawa tunaingia province ya GITARAMA safari anaendelea upo kwenye kibini za maroli lakini unasikia dereva anaingiza gia Kama vile hataki kwackweli kwa lile tukio kila mtu alikataa tamaa kabisa....

Sasa tunaingia mji wa GITARAMA tunashuhudia Jambo ambalo linatuacha wote tumeduwaa na mi Domo wazi....Ila hakuna wakumuuliza mwenzake. ......jambo gani hilo?

Itaendelea......................................



( Ila kisimu Cha wife daa sijakizoea battan zake napata shida kweli kuandika)

Sent using Jamii Forums mobile app
Nisije nikaota ulichosimulia 😭😭😭
 
Back
Top Bottom