Inaendelea .............
Tulipoishia Sasa tukawa tumefikia kuimaliza province ya Butare hapo ndio tukakuta kizuizi interahamwe kibao kama Mia mbili hivi na kila mtu na panga wengine wamebeba RPG wengine vibomu vya Mikono halafu pembeni Kuna maiti kibao, Sasa kilichonistua zaidi maeneo yale kulikuwa na maiti mbili za wazungu nahisi atakuwa mke na mume, Sasa nikajiuliza kama hawa wazungu wameuawa sisi ni akina nani tusiuawe. Ikawa Sasa magari yamesimamishwa .
Sasa nikawa nawaza hivi lile defender limeenda wapi na wale jamaa hapa siwangesaidia au katika mapigano Yale pale darajani limeangukia mto Nyabarongo. Sasa hapo ikawa ni kushuka wote hakuna Cha dereva wala utingo unazima gari chini maroli 24 yote watu tukawa chini jamaa wanaimba nyimbo zao za chama mapanga juu yanalia tu nguo zao zimejaa damu nikajisemea sasa tumekwisha ikabidi balozi atoke kwenye gari lake aje nyuma kwenye maroli.
Sasa ikawa tumepangwa kwenye mstari unanyanyua passport yako juu huna unakaa pembeni, Kama unakumbuka kuna watu nilisema wakati tunavuka daraja walikuwa wanapanda maroli ya nyuma nao walikuwa wanakimbia Kigali sasa ikaja kimbembe kumbe hawana karatasi (passport) Ila ni wanyarwanda aise wakawa wanawekwa pembeni tu haijalishi ni mtusi au ni mhutu
Sasa hapo likaja swali wakawa wanaulizwa wale jamaa kwanini mnakimbia wakati nyinyi ni wahutu kwanini msibaki mpambanie nchi yenu wakawa wanajitetea tu aise likatokea jamaa likamkata na panga moja wapo miongoni mwa wale eneo la shingoni damu ikaruka aise mwili wangu haujawahi kufa ganzi Kama siku ile (Kuna kitu nimejifunza na kimekuwa kikijadiriwa Sana humu binadamu anapokaribia kufa huwa hasikii maumivu yeyote huwa anakuwa Kama amepigwa na ganzi Kama tutaendelea kunifuatilia nitaelezea tukio lilonitokea nikiwa nikiwa jela Ndola-Zambia baadae sana, msistuke nimeshafungwa jela miaka mitatu kisa biashara za chuma chakavu) tuendelee...
Sasa Yule mtu aliepigwa panga akawa amedondoka anakoroma Kama mbuzi aise kwa kweli pale akili iliondoka kidogo nikawa kama nimehama ulimwenguni kwa sekunde kadhaa hapo wote passport zipo juu yaani unanyoosha Mikono na passports jamaa linapita linakagua aise ikawa huku Zoezi la kuwasurubu wale wahutu wengine likiendelea Sasa Kuna watu sijui ni ndugu wale nao walikuwa wamedandia roli wakawa chini pamoja nasi yule mkubwa akapewa panga amkate yule mdogo shingoni ikawa jamaa anasita sita wakasema Sasa tunawaua wote si hutaki, pale pale yule mkubwa akampa mpanga yule mdogo halafu alikuwa amevaa Sweta zile zenye kofia akaivua akakunja shingo akamwambia yule mdogo piga shingoni ikawa Kama anasita Ila Kaka mtu akamwambia piga yule dogo akapiga kweli damu ikaruka hadi nilipokuwa nimesimama Hadi matonetone yakawa yamechafua kidogo suruali niliyokuwa nimevaa aise jamaa kadondoka mzima mzima paaaa...
Sasa hapo balozi anaongea na lile jamaa lililoonekana Kama ndio kamanda lao Ila likawa Kama halina time nae vile nikajisemea Leo hatutoki, majamaa yanapanda kwenye maroli yanachukua kila kitu kilichokuwemo mikate, nguo, viredio, majiko na masufuria ya kupikia
Sasa hapo tukawa njia panda. Sasa wakati lile njembaa linakagua aise likafika kwenye gari ya balozi likawaona wale mabinti aise acha liwachomoe unaujua ile gari ya balozi Ilikuwa na tinted hivyo alivyoshuka aliwaacha, watoto wakachomolewa wakavutwa nywele Kama kuku vile unavyomtoa bandani ikawa Sasa mzozo kila interehamwe anataka awavute ikawa mzozo mabinti wale wakawa katika ya msitu wa wauaji
Mwanzoni nilisema Kuna matukio mawili ambayo Aliyafanya balozi Hadi nikamvulia kofia nimetaja la kwanza pale ubalozi, Sasa Hili ni la pili yule mama (balozi) alichomoka pale pale alipokuwa akaingia katikati ya msitu wa wale jamaa akawa anavutana nao yaani anawavuta wale watoto na wale interehamwe wanawavuta wale watoto sasa ikawa vurugu tupu ikabidi wale watoto wawe wamemuinamia balozi tumboni Kama vile kuku anae atamia, uongo mbaya siku ile ndio nilimchukia balozi wangu yani nilimuuona Hana maana kabisa yaani kwa kitendo kile alichokuwa amekifanya nilijua Sasa anaamsha hasira za interahamwe Sasa tunakufa wote. Dhana ya kuogopana ikawa imechukua nafasi tumefikia mwisho wa uharibifu kila mtu anatetea nafsi yake (nikaona Bora angeacha tu wauawe wale mabinti sisi tuendelee na safari yetu mungu anisamehe ila mawazo hayo yalikuwa Bora kuliko kitu chochote kwa wakati ule)
Mama kakomaa aise lile jamaa likawa limefika pale, balozi kishati chake kimechanwa imebaki sidiria tu na alivaa sketi mama kakomaa lile jamaa likatoa sauti kwa kinyarwanda REKAA hiyo sauti huwa siisahau (maanake nafikiri ni achaa) Sasa wakati anasema vile kuna tukio lilienda sambamba na ile sauti nusu tufe aise.
Unajua roketi ya mkono RPG ukiwa umeibeba lazima uelekeze juu Sasa Kuna interahamwe moja sijui Ilikuwa aje, unajua Hawa hawana mafunzo wameokotwa tu mitaani aliishika Kama vile kashika bunduki ya kawaida Sasa wakati wa vuta ni kuvute sijui lilishika kwenye triga chuma ikachomoka ikapita katika ya watu, ikapita katika ya roli na gari ya balozi tukasikia mripuko aise kila mtu pale alichanganyikiwa yanii ni moshi mtupu Sasa ikawa haijulikani imetokea wapi imerushwa au imekuwaje Tena?
Intetahamwe wakasambaa wengine wakawa wanakimbilia mabondeni, kama dakika kumi zikapita tukawa tumepowaa kidogo Ila kelele tupu lile jamaa likamsogelea balozi likamuuliza hao ni akina akasema wanangu unajua balozi alikuwa mweupe na wale watoto walikuwa weupe kwa struggle ile lile jamaa halikutia shaka tena, mwanamke kumpigania mtoto namna ile hata wewe huwezi kataa kuwa sio mwanae Sasa hapo tukawa tumetulia kidogo jamaa wakaturuhusu safari ikaanza hapo watanzania watupu wale wadandiaji wote walishushwa sijui kilichoendelea nyuma Sasa tukawa tunaingia province ya GITARAMA safari anaendelea upo kwenye kibini za maroli lakini unasikia dereva anaingiza gia Kama vile hataki kwackweli kwa lile tukio kila mtu alikataa tamaa kabisa....
Sasa tunaingia mji wa GITARAMA tunashuhudia Jambo ambalo linatuacha wote tumeduwaa na mi Domo wazi....Ila hakuna wakumuuliza mwenzake. ......jambo gani hilo?
Itaendelea......................................
( Ila kisimu Cha wife daa sijakizoea battan zake napata shida kweli kuandika)
Sent using
Jamii Forums mobile app