Sio afya kwa serikali, Jeshi letu la Polisi linapotiliwa mashaka

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Kaka yangu Nape, mapema mwaka huu aliwahi kusema, kama serikali isipodhibiti matumizi ya nguvu dhidi ya raia, Siku moja wananchi watakikataa chama chetu.

Kila mtu anaweza kuwa na mtazamo wake juu ya hili, lakini mimi napenda kuwakumbusha viongozi wangu uchaguzi wa 2010 Mbeya mjini kati ya Sugu na mzee wangu Mpesya.

Tuwe wakweli na nafsi zetu, ukatili wa migambo wa jiji, haswa wakati wa kuwaondoa waliokuwa wafanyabiashara lilipokuwa soko la makungulu, kwakiasi kikubwa ndio uliochochea chuki za wananchi dhidi ya chama.

Matokea yaliyoripotiwa na utafiti wa Afro barometer, ingawa yalihusu kupima imani ya wananchi juu ya jeshi polisi, lakini huwezi kuyatenga na imani ya wananchi dhidi ya serikali.

Mzee Simbachawene alitoa mwelekeo mzuri sana alipokuwa waziri wa mambo ya ndani. Kwamba ifike mahali, wananchi wasifurahie polisi wetu kupata matatizo.

Lakini, haya mambo yanapojirudia rudia ya watu kulihusisha Jeshi letu la polisi na utekaji sio mazuri. Ni kweli hakuna ushahidi wa wazi unaothibitisha polisi kutenda hayo mambo, lakini huku mitaani tunakoishi maneno haya yanasemwa sana na wananchi wanayaamini.

Mimi nadhani, ipo haja ya Jeshi letu la polisi kuchukua hatua za kizalendo kuhakikisha mambo haya ya watu kutekwatekwatekwa yanakomeshwa. Sio sawa na tusizizoee kabisa kuzisikia taarifa kuwa Jeshi la Polisi linafuatia taarifa za mtu fulani anayedaiwa kutekwa.

Pia niwasihi wana CCM wenzangu kujiepusha na kauli zinazoshabikia uvunjifu wa haki za binadamu. Tusisahau kuwa uchaguzi unapofika ni sisi ndio wenye jukumu la kuwashawishi wananchi wenzetu kuendelea kuichagua CCM. Tusipoyakemea haya leo, kazi yetu ya kuwashawishi wananchi watuchague tena 2030 itakuwa ngumu sana.

Nimalize kwa kusema, ni wajibu wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, haswa Jeshi la Polisi kutafsiri kwa vitendo falsafa ya KAZI NA UTU ya Mh. Rais wetu, Dr. Samia Suluhu Hassan.
 
Kaka yangu Nape, mapema mwaka huu aliwahi kusema, kama serikali isipodhibiti matumizi ya nguvu dhidi ya raia, Siku moja wananchi watakikataa chama chetu.

Kila mtu anaweza kuwa na mtazamo wake juu ya hili, lakini mimi napenda kuwakumbusha viongozi wangu uchaguzi wa 2010 Mbeya mjini kati ya Sugu na mzee wangu Mpesya.

Tuwe wakweli na nafsi zetu, ukatili wa migambo wa jiji, haswa wakati wa kuwaondoa waliokuwa wafanyabiashara lilipokuwa soko la makungulu, kwakiasi kikubwa ndio uliochochea chuki za wananchi dhidi ya chama.

Matokea yaliyoripotia na utafiti wa Afro barometer, ingawa yalihusu kupima imani ya wananchi juu ya jeshi polisi, lakini huwezi kuyatenga na imani ya wananchi dhidi ya serikali.

Mzee Simbachawene alitoa mwelekeo mzuri sana alipokuwa waziri wa mambo ya ndani. Kwamba ifike mahali, wananchi wasifurahie polisi wetu kupata matatizo.

Lakini, haya mambo yanapojirudia rudia ya watu kulihusisha Jeshi letu la polisi na utekaji sio mazuri. Ni kweli hakuna ushahidi wa wazi unaothibitisha polisi kutenda hayo mambo, lakini huku mitaani tunakoishi maneno haya yanasemwa sana na wananchi wanayaamini.

Mimi nadhani, ipo haja ya Jeshi letu la polisi kuchukua hatua za kizalendo kuhakikisha mambo haya ya watu kutekwatekwatekwa yanakomeshwa. Sio sawa na tusizizoee kabisa kuzisikia taarifa kuwa Jeshi la Polisi linafuatia taarifa za mtu fulani anayedaiwa kutekwa.

Pia niwasihi wana CCM wenzangu kujiepusha na kauli zinazoshabikia uvunjifu wa haki za binadamu. Tusisahau kuwa uchaguzi unapofika ni sisi ndio wenye jukumu la kuwashawishi wananchi wenzetu kuendelea kuichagua CCM. Tusipoyakemea haya leo, kazi yetu ya kuwashawishi wananchi watuchague tena 2030 itakuwa ngumu sana.

Nimalize kwa kusema, ni wajibu wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, haswa Jeshi la Polisi kutafsiri kwa vitendo falsafa ya KAZI NA UTU ya Mh. Rais wetu, Dr. Samia Suluhu Hassan.
Mapaka mambo yavurugike hawatosimama
 
Back
Top Bottom