Sio kazi yako kuwa kila kitu kwa kila mtu.

Sio kazi yako kuwa kila kitu kwa kila mtu.

realMamy

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
3,925
Reaction score
8,853
Hapa sasa inatakiwa kuwa na Mipaka katika maisha yako.

Kila shughuli umo tu, Kila mtu akikosa mtu wa Muhimu anakutumia wewe sasa kuziba pengo.

Ukiitwa mahali kuna shughuli unaenda yani wewe hata kama ulikua unafanya kitu cha maana unaacha unakimbilia unakoitwa.

Mtoto anaumwa baba au mama unahitajika uwepo pale muda wote lakini ukipigiwa tu simu kuna bia za bure unaacha kila kitu unaenda.

Hilo ndilo kusudi lako uliloletwa nalo duniani?

Hata siku moja huwezi kusema uko busy na familia wewe ni kuyapa umuhimu tu mambo ya watu.
Hiyo siyo kazi yako.
Jipe umuhimu kwanza wewe na familia yako.
Huko kwingine utaenda hata baadaye.

Ukitaka kujua huna umuhimu huo pata shida uone kama utawaona hao uliokuwa unawaona wa muhimu.
 
20240725_075653.jpg
 
Back
Top Bottom