May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Leo asubuhi kupitia redioni nimesikia wakisoma moja ya Gazeti lenye kichwa cha habari kinachosema, vifuu, machicha, ungawa mbao n.k vinahitajika huko kwa wenzetu.
Sidhani kama hii ni fursa sahihi, kwa nini tusifikirie kwenye kuuza bidhaa tayari? hivi kweli bidhaa za nishati zinaweza kukosa soko hata hapa hapa nchini?
Wapi zile ndoto za kuwa Tanzania ya Viwanda?, au ndio imeshaenda na Mwendazake?
Kinachoenda kutokea ni sisi kuendelea kuwauzia Wenye nguvu malighafi wengine alafu wao watuuzie bidhaa zilizo tayari.
Badala ya sisi kuwasaidia Wajasiriamali wetu kuwa na viwanda vya kuandaa hizi nishati mbadala kupitia hivyo vifuu na mabaki/unga wa mbao eti tunataka ku export hizo malighafi... matokeo yake Wajasiriamali wetu watashindwa kupata malighafi kiurahisi na kubakiza matumizi ya mkaa yaendelee kwa fujo tuendelee kumaliza misitu yetu...na tukishamaliza misitu sasa tunakuwa Wateja wa mkaa unaotengenezwa Viwandani kwao.
Sijui ni bidhaa gani wanaenda kutengeneza lakini chondechonde tutumie hizi malighafi kutengenezea mkaa mbadala, Watu wetu wajiajiri sambamba na kupunguza kama sio kuondoa kabisa matumizi ya mkaa wa misitu.
Tutengeneze sisi hizo 'briquettes' tuzipaki kisha tuwauzie, la basi tuendelee kuwa Wanunuzi wakuu wa Dunia hii kwa kufikiri kila kitu kinafaa kuwa biashara angali ghafi.
Sio kila fursa ni fursa, haswa kwa vile visivyohitaji mtaji mkubwa kuvibadilisha bidhaa...hata zisipouzika nje bado hapa nyumbani wapo Watumiaji w kutosha.