KWELI Sio kila maji ya mvua ni salama, baadhi hayafai kwa kunywa

KWELI Sio kila maji ya mvua ni salama, baadhi hayafai kwa kunywa

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Salaam wakuu,

Rainwater.jpg

Wakati mikoa mingi nchini ikiendelea kupata mvua ya kutosha, kwa wengine imekuwa neema kwao kwani sasa wanaweza kuvuna maji ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, mifugo na hata mazao.

Sasa kwa matumizi ya nyumbani ni pamoja na kuyatumia kwa kunywa bila kuyafanyia treatment yoyote. Tokea nakua kumekuwa na kasumba na kuaminishana kuwa maji ya mvua ni bora kwa kunywa. Mvua ikinyesha tumekuwa tukiyakinga na kunywa moja kwa moja bila kujua madhara yake

Pamoja na kubeba vimelea vingi na kila aina ya takataka, pia kuna aina ya madini maji hayo hukosa kwa ajili ya afya ya binadamu.

Pia kuna jamii zinaamini kuwa maji ya mvua yanatibu magonjwa mbalimbali.

Maji ya mvua yanaweza kuwa safi lakini siyo salama.
 
Tunachokijua
Maji ni kitu muhimu kwenye maisha ya viumbehai, na karibia 60% ya mwili wa binadamu huundwa kwayo.

Hivyo, mwili wa binadamu hutoa maji kupitia takamwili zake kama vile jasho na mkojo na kunywa maji ya kutosha kila siku husaidia kuboresha afya ya mwili pamoja na kufidia kiasi kingine kinachopotea.

Vyanzo vya maji
Vyanzo vya maji ni jumla ya maeneo yote ambayo maji huanzia hapo kabla ya kusafiri Kwenda sehemu nyinginezo. Kwa mfano Mito, Maziwa, Visima, Chemichemi, Mabwawa nk. Kimsingi maji ndio kiini cha uhai wa viumbe hai vyote vilivyopo duniani. Iwe ni Binadamu, Wanyama na Mimea, vyote haviwezi kuishi bila ya uwepo wa maji safi na salama.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizojaliwa aina tofauti tofauti za vyanzo vya maji, ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, nk. na huyatumia maji haya kwa shughuli mbalimbali za kibinadamu pamoja na shughuli za kiuchumi.

Usalama wa maji ya mvua
Kukusanya na kutumia maji ya mvua inaweza kuwa njia nzuri ya kuhifadhi rasilimali. Watu wengine hutumia maji ya mvua kumwagilia mimea, kusafisha, kuoga, au kunywa. Hata hivyo, ni muhimu kuhakikisha kuwa mfumo wa ukusanyaji maji ya mvua unadumishwa ipasavyo ili kutunza ubora wa maji kwa ajili ya matumizi yaliyokusudiwa.

Ingawa ni muhimu kwa vitu vingi, maji ya mvua yanaweza yasiwe safi kama watu wengi wanavyofikiria, hivyo sio kila wakati hufaa kwa kunywa. Mvua inaweza kubeba aina tofauti za uchafu ndani ya maji unayokusanya (kwa mfano, kinyesi cha ndege kwenye paa lako kinaweza kuishia kwenye pipa lako la maji au tanki). Yanaweza kubeba bakteria, virusi pamoja na kemikali zingine zinazoweza kuwa hatari kwa afya yako.

Hatari ya kupata magonjwa kutokana na maji ya mvua inaweza kuwa tofauti kulingana na eneo lako, ni mara ngapi mvua inanyesha, msimu na jinsi unavyokusanya na kuhifadhi maji ya mvua. Vumbi, moshi na chembechembe kutoka angani zinaweza kuchafua maji ya mvua kabla ya kutua juu ya paa lako.

Hivyo, madai ya kuwa sio kila maji ya mvua ni salama yana ukweli.

Jikinge na magonjwa
Ili kupunguza hatari ya kuugua, zingatia kutumia maji ya mvua kwa matumizi tu kama vile kumwagilia mimea au kuosha vitu ambavyo havitumiki kwa kupikia au kula. Epuka kutumia maji ya mvua kwa ajili ya kunywa, kupikia, kupiga mswaki, au kuosha au mimea ambayo unakusudia kula.

Ikiwa una mfumo wa kinga dhaifu, unapaswa kuwa mwangalifu hasa wakati wa kuchagua chanzo chako cha maji ya kunywa.

Hata hivyo, sio maji yote ya mvua ni mabaya. Ikiwa umejiridhisha kuwa maji husika ni masafi unaweza kuyatumia kwenye shughuli zote zinazokuhusu, ikiwemo kunywa.
Bado Hujaweka Wazi Huo Usalama Unao yakosa Niupi Ukilinganisha Na Hayo Mengineyo
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Nina tank la lita 10,000 na 5000, hilo la lita 5000 kwa ajili ya kunywa tuu. Napenda maji ya mvua hayana chumvi haaaah basi bwana km yanamatatizo.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
haya maji ya mvua yamekuwepo kwa dahari na kimsingi kwa sisi wengine ndiyo yametukuza hadi hapa tulipo sasa. binafsi sijawahi kupata shida kwa kutumia maji haya.

Nayapenda ni maji laini na mororo sana.
Isijekuwa uhai & Co wameanza kampeni zao ili wauze bidhaa zao. Maana huwa wanaanza iviivi.
 
Hakuna maji yaliyo salama 100%, hata maji ya viwandani ni hatari kwa afya kutokana na kemikali zinazowekwa.

Maji yote tunayotumia yana changamoto zake
 
Salaam wakuu,


Wakati mikoa mingi nchini ikiendelea kupata mvua ya kutosha, kwa wengine imekuwa neema kwao kwani sasa wanaweza kuvuna maji ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, mifugo na hata mazao.

Sasa kwa matumizi ya nyumbani ni pamoja na kuyatumia kwa kunywa bila kuyafanyia treatment yoyote. Tokea nakua kumekuwa na kasumba na kuaminishana kuwa maji ya mvua ni bora kwa kunywa. Mvua ikinyesha tumekuwa tukiyakinga na kunywa moja kwa moja bila kujua madhara yake

Pamoja na kubeba vimelea vingi na kila aina ya takataka, pia kuna aina ya madini maji hayo hukosa kwa ajili ya afya ya binadamu.

Pia kuna jamii zinaamini kuwa maji ya mvua yanatibu magonjwa mbalimbali.

Maji ya mvua yanaweza kuwa safi lakini siyo salama.
Mtoto wa Maji ya Kilimanjaro kwenye ubora wako.Tutolee upuuzi wako,Mimi na familia yangu tumekuwa tukitumia Maji ya Mvua nahifadhi kwenye kisima kikubwa,na wakati mwingine vyura wanaingia,lakini Maji hayohayo,tunakunywa tena bila kuchemsha.Na hatujawahi kupata kasoro.Nenda kawahubirie hao watoto wenzio wa Maji ya Sekwa na Kilimanjaro.Acheni kudekeza miili yenu
 
Siku moja dar es salaamu mahali nilipo panga niliwahi kutoa wazo kuwa tutengeneze mfereji wa kukingia maji yanayotok kwenye bati , baada ya kuona maji mengi yanapotea nasis Tunapat tabu kunywa maji ya chumvi, au yale ya DAWASA. Dada mmoja na wenzake waliniambia maji ya mvua ni mabaya kiafya kutokana ya Anga hewa kukusanya moshi mchafu wa viwanda ,hivyo mvua inaponyesha huja na zile kemikali, Niliingiwa na shaka na sikuendelea na kampeni ya kutaka tuweke mfereji. Kwenu studio naomba ufafanuzi zaidi.
 
Maji ya mvua ukiyahifadhi kwa muda yanaweza kutoa viluwi luwi sometimes and kuna time yanatoa haruf and ile harufu huisha kabisa.. huwa siyaelewi ila siyaachi kuyakinga.. zawadi from God huwezi kuidharau... ila kuyatumia lazima kuyachemsha... madhara sijawai ona labda baada ya miaka 100 nadhani
 
Shule niliyosoma high school hapakuwa na chanzo kingine cha maji isipokuwa maji ya mvua yaliyovunwa. Tumetumia maji hayo kipindi chote cha advance bila shida
 
Back
Top Bottom