Sio kila mwenye mafanikio ana raha na mafanikio yake

Sio kila mwenye mafanikio ana raha na mafanikio yake

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
278
Reaction score
512
Usiumie, usilie wala usijipe unyonge kuona wengine wanapata mafanikio wakati wewe miaka nenda miaka rudi upo palepale.

Sikia nikwambie ndugu yangu, sio kila mwenye mafanikio ana raha na mafanikio yake. Kuna vilio vingi nyuma yao nje na haya ambayo tunayaona kwa macho.

Kuna watu wanacheka mbele za macho yetu lakini wakiwa chumbani wanalia kuona nyuso za wazazi wao au watoto wao kwenye chumba kisichofunguliwa na mtu yoyote.

Nyuma ya mafanikio yao tunayoyaona kuna ajali nyingi zisizotarajiwa zimetokea huko barabarani kama kafala kulipia gharama za mafanikio yao.

Kafala haziwapi furaha lakini hawana namna nyingine ya kufanya kwasababu wanaupenda utajiri na hawapo tayari kurudi kwenye umasikini na kutafuta vya halali.

Ndugu yangu, hata siku moja usije ukatamani mafanikio ya mtu ikiwa ujui amepita njia gani hadi kupata mafanikio hayo.

Kuna watu ni baba kwenye ndoa zao lakini nyuma ya panzia nao ni wanawake na wanatoa ndogo kwa maboss ili kumiliki majumba na magari ya kifahari hapa mjini.

Mafanikio ya aibu hayana raha hata kidogo. Katika utafutaji wako usithubutu hata siku moja kujaribu kutafuta kisicho cha halali kwani kitakufedhehesha mwisho wa safari.

Mwenyezi MUNGU anatoa riziki kwa kila mja kadri ya mapenzi yake na juhudi zako. Usichoke kupambana huku ukimuomba yeye akupe kile unachokipigania kila siku.

Usifuate njia za waovu, fuata njia ya wenye haki. Hata liziki zako zikichelewa amini ipo siku zitakufikia na utafanikiwa. Changamoto huna budi kuzikabili kwani kila mafanikio huja na mitihani yake.

Tuendelee kupambana 💪💪💪

#No_learnig_No_earning
So We Have To Learn.

Content By Mr George Francis
 
Utajiri ni siri

#hakuna utajiri wa kafara,majini... hizo ni myth tu kama upo thibitisha hapa.
 
Back
Top Bottom