Sio kwamba anakupenda, Anakuhitaji kwaajili ya kutimiza nahitaji yake

Sio kwamba anakupenda, Anakuhitaji kwaajili ya kutimiza nahitaji yake

kulagha nenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2026
Posts
690
Reaction score
1,375
Habari wadau, Haya mahusiano Yana Siri kubwa sana

1.Wakati wewe mwanaume unafikria kuwa umempata mke wa maisha mwanamke anafurahi kupata boya la kumaliza shida zake za kwao na kumsaidia ex wake mtaji.

2 Kuna mwanaume unamwona kama vile kakuzimia anatangaza na ndoa kabisa kumbe akili zake zote ni hilo tako TU yaani akikuvua tu hata habari za kwenda kwenu kujitambulisha anakupotezea na mwisho hata simu hapokei. Wakati wewe ulishajiaminisha kuwa huyo ndo bwana ukute ndo ulishawakataa wanaume kibao . Shukuru Mungu kama haja kuacha na mimba au mtoto.

3. Wapo waliouza mali zao nakutoa hata viungo vyao vya mwili kama vile Figo na damu kwaajili ya mapenzi mwisho WA siku wameachwa na hao waliofikri wanawapenda.

Hitimisho langu nikuwa
Tuishi TU katika mahusiano huku tukijua kuwa huna garantii ya kuishi au kuwa na mahusiano ya milele na huyo uliye nae kwasababu hujui ni kwanini yuko na wewe hapo.
Sababu za kuwafanya watu wawe na mahusiano ya kimapenzi huwezi kuzifafanua ni ngumu kuzijua, zina utata mwingi.

Kila mtu anasababu zake za kuwa na fulani

Ndo maana sio vizuri kuyatumia mahusiano ya watu wengine kufanya kama rejea unapotatua matatizo ya kimahusiano na ndoa.

Yale maneno, hamkuni vizuri, hatoi matumizi ana kiburi, ndo maana wameachana huwa ni stori za kufikirika TU.
 
Shida nipale tunapotanguliza matamanio na matrajio yetu bila kujua mwanamke au mwanaume amekukubalia au kaja kwenye maisha yako akiwa na mipango gani kichwani
 
Sasa tatizo ni nini?
Maana yake wewe unategemewa, na ndiyo maana ya mapenzi.
 
Back
Top Bottom