Sio lazima kila kitu kifanyike Arusha, semina na vikao serikalini, pia vifanyikie Lindi, Mtwara, Ruvuma, zimesahaulika

Nashauri uongozi mkuu utoe maelekezo maalum kwa taasisi na mashirika. Kama taasisi au shirika lina semina/ mafunzo/ vikao 10 kwa mwaka, kwa kuanzia, walau kikao/ semina moja ifanyikie katika mikoa hiyo.

Hii itasaidia kuiunganisha nchi kiuzalendo na mzunguko wa uchumi.

Mambo ya kupeleka kila kitu Arusha hayajengi uwiano wa kieneo kwa nchi
Chuki imekuwa la. Elimu elimu Elimu
 
Ungesema mtwara at least na ruvuma labda songea,lindi hiyo kumbi za kutosha vikao vya kiserikali hakuna kungekuwa na jam foleni lodges chache zenye ubora,watu matukio ya kitaifa wanachukua lodge mtwara na matukio yanafanyika lindi..its nonsense.
wajipange kwanza ndipo hizo fursa zije mjini lakini pamekaa kama kijijini bhana 🤣
cc: ndege JOHN
Mji umejaaa mam mamwinyi nani aje huko
 
  • Thanks
Reactions: apk
Ngoja nije kuwa Raise 2040.. Lindi, Mtwara na Ruvuma watainjoi sana..
Nitajenga SGR kutoka Dar, Lindi, Mtwara mpaka Mbababay
 
Fanyeni maendeleo huko ili pawe na vivutio watu ndio watapapenda maana huwezi kwenda kupeleka kongamano sehemu ambayo hata malazi hayakizi watu wenye nyazifa zajuu ,jengeni mahoteli makubwa
 
Nashauri uongozi mkuu utoe maelekezo maalum kwa taasisi na mashirika. Kama taasisi au shirika lina semina/ mafunzo/ vikao 10 kwa mwaka, kwa kuanzia, walau kikao/ semina moja ifanyikie katika mikoa hiyo.

Hii itasaidia kuiunganisha nchi kiuzalendo na mzunguko wa uchumi.

Mambo ya kupeleka kila kitu Arusha hayajengi uwiano wa kieneo kwa nchi
Naunga mkono hoja, sumbawanga pia na Kigoma, lakini tatizo "facilities", tuanze na hili kwanza kwa viongozi wetu wa mikoa kuchangamka nalo, waige mfano wa Makonda, hasa kuhusu ubunifu.
 
Ndio wafanye kugawanya sio kila siku sehemu moja tu ....Huu ni ujinga kabisa .
 
Shida ni hotel nzuri na kumbi nzuri za hadhi ya wanasemina

Guest House wengi Huwa hawapendi

Arusha hotel zenye hadhi ziko nyingi mno za viwango vya kimataifa

Huko Lindi,Mtwara na Ruvuma nitajie hoteli kumi tu mjini kwenye Kila mji zenye hadhi ya kimataifa Lindi,Mtwara.Ruvuma
 
Nashauri uongozi mkuu utoe maelekezo maalum kwa taasisi na mashirika. Kama taasisi au shirika lina semina/ mafunzo/ vikao 10 kwa mwaka, kwa kuanzia, walau kikao/ semina moja ifanyikie katika mikoa hiyo.

Hii itasaidia kuiunganisha nchi kiuzalendo na mzunguko wa uchumi.

Mambo ya kupeleka kila kitu Arusha hayajengi uwiano wa kieneo kwa nchi
Kwanini huulizi mbona kuna taasisi nyingi za Africa Mashariki na pia Africa pale Arusha? Usifananishe Arusha na miji mingine hata Dodoma na Dar hawana umuhimu kama Arusha linapokuja suala la mikutano.
 
Marehemu Ben alishindwa kubadili hiyo mikoa ndo bas .

Hawa akina goli la mkono hawana time
 
Nguvu ni lazima zitoke katika mipango ya viongozi waliopo ndani ya mkoa husika, mipango thabiti, nia za dhati, na tusisahau GOEGRAPHICAL POSITIONS!...
MFANO, Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro ameanza kuyaona haya vyema, yupo anapigana na Wawekezaji ili kuona wanajenga kumbi na hotel za hadhi ya juu, huu tunauita utendaji wa kujiongeza,sasa yuko mkuu wa mkoa kabisa hajiongezi yeye ni kupigana na senti za halmashauri na tozo mbalimbali, anasahau kushughulika na wawekezaji mbalimbali, mwishowe anadumaza eneo la mkoa wake, kuna Mkeka unatoka wa wakuu wa mikoa stay tune!, kuna wakuu wa mikoa ni mizigo!
 
Kulitakiwa kuwe na makao ya kikanda , mbona BOT wana tawi lao Mtwara? Serikali ndio imechemsha yenyewe kufanya distribution ya rseource hata ile gas waitaka kupeleka mikoa kuwaacha wazaw hawana kitu .
 
Ngoja nije kuwa Raise 2040.. Lindi, Mtwara na Ruvuma watainjoi sana..
Nitajenga SGR kutoka Dar, Lindi, Mtwara mpaka Mbababay
Hiyo iko kwenye plan usanifu umeshaanza ujenzi utaanza soon
 
Back
Top Bottom