Sio muda tutakua na Formula AI. Sijui utamu wa racing utakua hivi hivi au ndio ushavamiwa?

Sio muda tutakua na Formula AI. Sijui utamu wa racing utakua hivi hivi au ndio ushavamiwa?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Wakuu.

Kuna hii trend kwenye tasnia ya mashindano ya magari naona inaanza kuja, ya AI racing, ambapo magari yakiwa yanajiendesha yanashindana kama F1 mfano (Formula AI tuite)!
IMG_0899.jpeg

Mi naona car racing sio tu kuhusu ubora wa magari, ubora wa team na teknolojia zao, ila skills na endurance za dereva zina mchango wake kwenye kuongeza utamu.

Sasa recently naona wazungu wanazidi kupush racing za magari yanayojiendesha yenyewe. Sasa sijui ata tunakua tunaangalia nini? Like tunashindanisha teknolojia ya Honda na Mercedes na McLaren au tunashindanisha IT na developer wa izo team?

Mfano:
IMG_0897.jpeg

Kuanzia mwaka jana (2024) kulizinduliwa hii A2RL (Abu Dhabi Autonomous Racing League) ambayo ni racing ya magari kama Formula One Grand Prix ila hayana dereva.
IMG_0896.jpeg

It was terrible, yaani ilikua kichekesho nikajua itafeli, ila imeendelea na mwaka huu wametoa season 2. Sahivi ipo testing ila main racing itakua November 2025.
IMG_0894.jpeg

Wengine Roborace pia wameanza kitambo kufanya autonomous racing ikiwa assist na LiDAR, radar na vision.
IMG_0895.jpeg

Sina ubaya na Driver Agent mfano ya Google Cloud inayotumika kwenye Formula E. Hii AI inamsaidia tu dereva kua better kwa kumshtua kama kuna mahala amekosea kukata kona, amepiga breki mapema, etc so ni kama simulator za kawaida, na anazitumia wakati wa mazoezi tu.
IMG_0898.jpeg

Ila sasa hii magari yanakua yanajiendesha hafu watu mnashangilia hapana aisee.

Bado Premier League AI tu.
 
Technology inaenda Kwa Kasi Sana naona Ile ladha ya akina Hamilton haitakuwepo tena.
Sasa itakuaje kwenye ajira zao hao madereva wa formula 1? Mpaka sasa nashindwa kujua utofauti Kati ya formula one na formula E
 
magari ya formula 1 yanatumia mafuta, magari ya formula E (e kwa maana electric) yanatumia umeme tu, battery technology bado sio nzuri, hivyo wanarace kwa lap chache tu hawawezi kufika lap 50/60/70 kama magari ya mafuta f1, pia kuna f2, f3, f4

wacheni technology iendelee, kwanini mpoteze hamu ya kuangalia binadamu wanarace kisa tu AI, camera technology imeendelea na inachukua picha nzuri Sana, lakini bado wapo watu wengi wanapendelea kuchora picha zao wenyewe na kununua paintings zilizofanywa na binadamu
hayo magari ya AI yaje tu, ili tupate burudani zaidi, wafatiliaji na wapenda robotics and AI hii ndo watafurahia zaidi
 
Daaah!!!!!!aisee shukran Sana mkuu Kwa elimu hii nilikuwa sijui kabisa mambo hayo zaidi kuona watoto wangu wanaagalia kule DStv.
Wiki iliyopita haya mashindano yalikuwa yanafanyika ujerumani nilioona hiyo formula E nikawa sielewi kabisaa!!!!
 
Mbona zipo.. mashindano ya simulation games za f1
 
Back
Top Bottom