Sio offside Yanga walihujumiwa

Tueleze na Yale magoli ya mikono alipokuwa anafunga Tambwe yalikuwa Ni halali au hujuma
 
Nawapenda sana wachambuzi wasioegemea upande kama wewe. Kilicholetwa mezani ni "Uhalali au Uharamu" wa goli la Tambwe dhidi ya Mtibwa. Nakubaliana na wewe kwamba hakuna hujuma katika tukio lile, ila ni mwendelezo wa umbumbumbu wa waamuzi wetu. Hali hii inachagizwa na Bodi ya ligi kutochukua hatua kwa waamuzi wanaoboronga kama huyu mshika kibendera Na.1 wa mechi hiyo. Kama wangekuwa wanachukuliwa hatua wangekuwa makini na makosa yangepungua.
 
Hakika mkuu, waamuzi wetu wabovu tukubali hilo tuna waamuzi wenye beji za fifa lakini katika michuano ya caf(afcon) hatuna hata mmoja..

Tatizo wengi kwenye soka wanapenda ushabiki maandazi.
 
Vipi lile goli la Ajib kuifunga Yanga akiwa Simba lililokataliwa kwa offside?
Vipi lile goli la mkono la Tambwe?
vipi Simba kunyimwa point 3 za ubingwa na kupewa kagera licha ya kumchezesha mchezaji ambaye hakustahili kucheza?
 
Marefa waanza sasa kujitafakari kwann hata mmoja hajaitwa afcon

Hakuna refa wa Tanzania anayeweza kuchezesha AFCON...upo wakati refa wa TZ alikuwa msomali alichezesha AFCON...akachezesha dakika zaidi ya 100...yaani aliongeza karibu dakika 10 pale dk. tisini zilipoisha...kama kumbukumbu zangu ni sahihi hakuchezesha tena michuano hiyo..halafu nakumbuka kuna mechi Simba na Yanga alikuwa ndiye mwamuzi, madaraka Selemani (mzee wa kiminyio0 aka-control mpira kwa mkono na kufunga wakati huo kulikuwa hakuna TV...refa yule msomali alikuwa anabebwa na kiongozi mmoja aliyekuwa FAT (TFFnya wakati ule) ambaye naye alikuwa msomali...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…