Ndio maana soka letu haliendelei kwa sababu ya unywanywa kama huu, wa kulalamika kuhujumiwa, akuhujumu nani ww na kwa faida gani..
Tunapaswa tutambue vitu viwili
1. Refa ni binadamu si wakamilifu, hata wakina collina walikuwa wanakosea japo ni kwa uchache..
2. Marefa watz ni wabovu kupita maelezo, hawana umakini mchezoni wakati mwingine wanashindwa kuzitafsir sheria kwa haraka..
Utashangaa mpira umeinsha manara anakuja na tv analalamika, haya masuala ya kulalama lalama upate huruma ya watu ni upuuzi!!
Hakuna cha kuhujumiwa wala nini ni refa alitoa boko, na makosa ya namna hii ni mengi mnooo kwa waamuzi wetu, sheria ya offside inawalamba mnoo chenga, acheze yanga, acheze simba, iwe lipuli, ndanda sujui kote huko huwa naona makosa yale yale.