Sio offside Yanga walihujumiwa

Sio offside Yanga walihujumiwa

Ndio maana soka letu haliendelei kwa sababu ya unywanywa kama huu, wa kulalamika kuhujumiwa, akuhujumu nani ww na kwa faida gani..

Tunapaswa tutambue vitu viwili
1. Refa ni binadamu si wakamilifu, hata wakina collina walikuwa wanakosea japo ni kwa uchache..
2. Marefa watz ni wabovu kupita maelezo, hawana umakini mchezoni wakati mwingine wanashindwa kuzitafsir sheria kwa haraka..

Utashangaa mpira umeinsha manara anakuja na tv analalamika, haya masuala ya kulalama lalama upate huruma ya watu ni upuuzi!!

Hakuna cha kuhujumiwa wala nini ni refa alitoa boko, na makosa ya namna hii ni mengi mnooo kwa waamuzi wetu, sheria ya offside inawalamba mnoo chenga, acheze yanga, acheze simba, iwe lipuli, ndanda sujui kote huko huwa naona makosa yale yale.
Nawapenda sana wachambuzi wasioegemea upande kama wewe. Kilicholetwa mezani ni "Uhalali au Uharamu" wa goli la Tambwe dhidi ya Mtibwa. Nakubaliana na wewe kwamba hakuna hujuma katika tukio lile, ila ni mwendelezo wa umbumbumbu wa waamuzi wetu. Hali hii inachagizwa na Bodi ya ligi kutochukua hatua kwa waamuzi wanaoboronga kama huyu mshika kibendera Na.1 wa mechi hiyo. Kama wangekuwa wanachukuliwa hatua wangekuwa makini na makosa yangepungua.
 
Nawapenda sana wachambuzi wasioegemea upande kama wewe. Kilicholetwa mezani ni "Uhalali au Uharamu" wa goli la Tambwe dhidi ya Mtibwa. Nakubaliana na wewe kwamba hakuna hujuma katika tukio lile, ila ni mwendelezo wa umbumbumbu wa waamuzi wetu. Hali hii inachagizwa na Bodi ya ligi kutochukua hatua kwa waamuzi wanaoboronga kama huyu mshika kibendera Na.1 wa mechi hiyo. Kama wangekuwa wanachukuliwa hatua wangekuwa makini na makosa yangepungua.
Hakika mkuu, waamuzi wetu wabovu tukubali hilo tuna waamuzi wenye beji za fifa lakini katika michuano ya caf(afcon) hatuna hata mmoja..

Tatizo wengi kwenye soka wanapenda ushabiki maandazi.
 
SIO OFFSIDE [emoji119]Kwa mujibu wa Kipyenga cha mwisho cha Mwamuzi Mstaafu, Osman Kazi, kinachoruka Azam Sports 2 kila Alhamis Saa 3:30 usiku..... goli la AmissTambwe dhidi ya Mtibwa Sugar, HAIKUWA Offside. Lilikuwa goli halali lililokataliwa na mwamuzi msaidizi namba moja (Line One).
.
.
Kwa namna picha hiyo ilivyochorwa mstari wa mwisho kuonesha Offside, unakubaliana na Osman Kazi au hapana?...Toa maoni yako.
#tpl
#chombokwahewa
View attachment 1075964
Vipi lile goli la Ajib kuifunga Yanga akiwa Simba lililokataliwa kwa offside?
Vipi lile goli la mkono la Tambwe?
vipi Simba kunyimwa point 3 za ubingwa na kupewa kagera licha ya kumchezesha mchezaji ambaye hakustahili kucheza?
 
Marefa waanza sasa kujitafakari kwann hata mmoja hajaitwa afcon

Hakuna refa wa Tanzania anayeweza kuchezesha AFCON...upo wakati refa wa TZ alikuwa msomali alichezesha AFCON...akachezesha dakika zaidi ya 100...yaani aliongeza karibu dakika 10 pale dk. tisini zilipoisha...kama kumbukumbu zangu ni sahihi hakuchezesha tena michuano hiyo..halafu nakumbuka kuna mechi Simba na Yanga alikuwa ndiye mwamuzi, madaraka Selemani (mzee wa kiminyio0 aka-control mpira kwa mkono na kufunga wakati huo kulikuwa hakuna TV...refa yule msomali alikuwa anabebwa na kiongozi mmoja aliyekuwa FAT (TFFnya wakati ule) ambaye naye alikuwa msomali...
 
Back
Top Bottom