Sio sawa kwa wazazi wenye pesa kuwaficha watoto wao upande mgumu wa maisha

Sio sawa kwa wazazi wenye pesa kuwaficha watoto wao upande mgumu wa maisha

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Maisha magumu hayanaga hodi, ni vema mtu uwe walau una maandalizi yake maana lolote laweza tokea.

Kuna malezi haya ya dezo huwa naona ni hatari kwa watoto, ikitokea mara paap mzazi kafukuzwa kazi, biashara imeyumba, katoweka, n.k na hana ndugu wa kuendelea kumlea mtoto wake maisha ya dezo, basi mtoto atateseka sana.

malezi haya ni kama kumfanyia vitu hivi mtoto:

- kufuliwa nguo,
-kuoshewa vyombo
-kupewa vingi anavyoomba (hajui kunyimwa)
-kusamehewa makosa bila adhabu
-kutoweza kujitetea (wazazi kumkinga badala ya yeye kurudishia)
-kuwafungia sana ndani watoto wasicheze hata na watoto wa jirani (inaua sana communication skills)
 
Utasikia wanasema "mtoto wangu awezi kuishi maisha niliyoishi mimi.*

Unashindwa kujua yeye (Mzazi) muda wote anavuta kamba na kuwaacha watoto wanaangaika yote ni kwa sababu hawana experience na msoto.
 
Back
Top Bottom