Dodoma haitakaa iifikie mwanza jiji kwa ukubwa hizo ni ndoto za mchana, mkoa wa mwanza una wakazi million 4 na eneo lake ni dogo dodoma ni jiji lenye kmsq zaidi ya 2500 ina population ya watu laki 7 mwanza ukiihesabu kwa hizo kmsq inawatu zaidi ya 2m lakini pia mwanza imezungukwa na kanda ya ziwa yenye watu wengi zaidi nchini kwahio mingiliano ni mkubwa lakini dodoma ilipokaa ni eneo lisilo na watu ukienda km zaidi ya 120 mashariki ndio unakutana na kibaigwa nao ni mji mdogo ukienda magharibi ni mbali hadi uje ukutane na bahi au manyoni nayo ni miji midogo ukienda kaskazini hadi uje ukutane na kondoa karibu km 200 nao ni mji mdogo kwenya upande wa iringa mji mkubwa kule ni iringa km zaidi ya 250 iringa nao si mji wenye watu wengi unazidiwa hata na geita iringa kwa watu ni kama bunda tu kuja kwenye maendeleo mwanza ni ya 4 nyuma ya arusha na zanzibar na dodoma kuzifikia arusha na zanzibar pia ni ndoto imagine arusha kuna ghorofa 7000 dodoma zipo 2000 ghorofa zinaonyesha uwezo wa kiuchumi wa wakazi huwez kua maskini ukajenga ghorofa sasa kufikia huko sio leo ukumbuke dar es salaam kilichoifanya kuwa kubwa ni bandari mwingiliano wa biashara na wala sio kua makao makuu hata sasa hivi mji umeamia dodoma lakini foleni ni vile vile lakini kingine uboreshwaji wa miundominu kila kanda sasa hivi inhospitali kubwa miundominu sasa hivi sgr mtu ataweza kwenda mwanza na dar kwa haraka hata huduma kama interview sasa hivi watu wanafanya online sio lazima wawepo physically huduma makao makuu huduma kama mailing n.k sasa hivi zinafanywa kwa delivery sasa dodoma nje ya kua makao makuu haina pulling factors za kuchochea uchumi mbeya kuna madini na kilimo, mwanza kuna uvuvi, arusha & zanzibar kuna utalii dar kuna bandari dodoma kuna nini ambacho kipo competitive usinitajie kilimo tena kwavile kwenye ile big4 ya chakula dodoma haipo na ndio maana fika dodoma watu wanalalamika maisha ni magumu kwa mtu ambaye sio mwajiriwa au mtumishi wa serikali au mfanyabiashara mkubwa bado dodoma ni mji wa boom la udom na msimu wa bunge au mkutano wa ccm
Labda serikali iache mpango wake wa kukuza utalii ila kama lengo ni lile lile la watalii 5mi hadi hiyo 2039 arusha na zanzibar zitakua mbali sana
Kw hio msimamo kwa maendeleo utabaki kua Dar, zanzibar, arusha, mwanza na dodoma mtachuana hiyo namba 4😀
Ila ambalo hakuna mtu atapinga ni kuwa dodoma ndio utakua mji namba mbili kwa miundombinu bora zaidi nchini ila kwa uchumi sahau chief naiona mbeya iko na bright future kuliko dodoma sio kwa hali ya hewa, vivutio vya utalii, kilimo na resources wanachokosa ni plan tu maskini kwa vile hata mbeya ingehesabiwa kwa ukubwa wa kmsq 2500 ingekua na watu 700k kama dodoma au zaidi kwa sababu kwa kmsq 200 tu mbeya jiji inawatu zaidi ya laki5 ngoja tu serikali iamke kuutilize resources zote za huo mkoa dodoma ni majengo ya serikali tu yakamilike kwisha 😀 irudi kwenye nafasi yake ya 6
NB: Mimi ni mmoja wa watu nnaosapoti sana mpango wa dodoma kua makao makuu kwa vile imeongeza mpangilio mzuri kwenye eneo tabarare la dodoma ambalo ni katikati mwa nchi kuliko
Dar 👏 Ni mafanikio makubwa ya kujivunia kama nchi kwamba hadi 2039 tutakua na la kujivunia kwamba tunamji mmoja smart na uliopangika kisawasawa wa dodoma bila kuathiri ukuwaji wa miji mama ya mbeya, mwanza ,zanzibar, arusha na Daresalaam