Sio tu hajui kiingereza! Ali kiba hajui kujieleza

Usijifariji kutoangalia kinyesi chako wakati unaharisha kwamba itatoa ukweli kuwa unaharisha. Kujieleza kunaweza kuwa ni kipimo cha fikra za mtu,mfano niliona anaeleza kuwa kuna watu wanamfanyia figisu kwenye suala la views huko youtube wakati kiuhalisia ni tofauti kabisa.
 
kalisheshe, Dishless mtoa mada hajaongea vibaya kwaiyo hujui umuhimu wa kingereza au unaongea kishabiki ukishakuwa star kuna vitu vya msingi kujifunza hasa lugha ya kuwasiliana na wengine wasiojua lugha yako.

Yeye ni international musician kujifunza jinsi ya kuwasiliana na mashabiki wake vyombo vya habari ni Jambo la msingi sana diamond amefika pale siyo kwamba kamzidi kiba kuimba ila vitu vidogovidogo ambavyo ameviboresha ambavyo wasanii wengi wa bongo hawana na hawaoni umuhimu kujifunza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu vingine ni mtu tu anahamua kujua au kutokujua wachezaji wengi tu na wakubwa hawajui lugha ya Kiingereza na maisha yao yanaenda vizuri tu nachokiona ni Ali kiba ajataka tu kujua pia inaweza kuwa hiyo lugha sio muhimu sana kwake [emoji41]
Mkuu huwezi kumfananisha mesi ambaye hajui kingereza lakin kihispania ni lugha iliyoenea sehemu kubwa duniani na wazungumzaji ki kutoka mataifa yenye nguvu duniani tofauti na wachezaji wa nchi zetu au wanamziki wa nchi zetu tukumbuke nchi nyingi za ulaya ni first world countries Ata kama mtu hajui kingereza lugha ya nchi yake itambeba Wana vyombo vya habari vyenye nguvu ambavyo mtu kupata kazi inakuitaji ujue lugha zaidi ya tatu au nne za kimataifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shebeleza tuliicheza hapa hata maana hatujui...ngoma za kina awilo,Kofi olomide, defao Muziki una lugha yake peke yake wenyewe unajieleza kwa melodies taaaaamu siyo huo upuuzi wanaouwaza

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda nikwambie tu kuna sababu nyingi za kupenda kitu hasa mziki na sababu moja kubwa ni air time inayopata kwenye vyombo vya habari kipindi kile kulikuwa hakuna cm janja kama ivi lkin kumbuka Congo wengi wanazungumza kifaransa kitu ambacho ilikuwa rahisi kwao kupata nafasi ya kusikilizwa na wengi na kupendwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua ni nn hakuna kitu kibaya kama kuwa mtumwa wa lugha, Lugha hiyo hiyo unayojifunza na kutumia nguvu iliuijue watu wake ndio hao hao wanaokubagua kuna umuhimu gani sasa hapo wakuwajua hizi lugha zao wakati huo account ya Bank yangu inazaidi ya 100M maisha yanaenda vizuri tu.
 
Wewe kama ni mshauri wake basi haufai hata kidogo
kuongea ni kipaji mzee ndio maana watu huajiri hata wasemaji.

wewe unafurahi mond anapojibu kila analoulizwa kuhusu wazazi wenzie!!!!!mwisho hukwaza watu na kuonekana anadhalilisha wanawake.

but tunampenda/mnampenda sababu ya muziki wake mengine ni ubinadamu,so why not alikiba!!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hajui kujieleza kapataje watoto kibao vile? Au unataka kuniambia hao wakinadada aliwabaka?
 
Vitu vingine ni mtu tu anahamua kujua au kutokujua wachezaji wengi tu na wakubwa hawajui lugha ya Kiingereza na maisha yao yanaenda vizuri tu nachokiona ni Ali kiba ajataka tu kujua pia inaweza kuwa hiyo lugha sio muhimu sana kwake 😎

Kiingereza ni lugha yako rasmi ya kibiashara na kielimu..
Kutokuijua ni lazma ikucost tu asa itakuwaje kwa public figures !!!...

Kipindi kile cha MTV south alipopiga show na sauti sol hadi alitia huruma kwenye interviews hadi akasaidiwa. Ungekuwa wewe si ungeanza hata jitihada za kujifunza !!!!...

Ukishajiita internationa act lazma uwe kama global citizen. Miss mdee anajua lugha zaidi ya tatu ila kuna mmoja anajiskia uvivu kujifunza lugha moja kwelii !!!
 
Huu ni mtazamo watu tu tunasema lakini ukweli wa mambo hatujui ni nini kinacho mfanya asitake kujifunza lugha ya Kiingereza jamaa inawezekana anasababu zake za msingi yeye mwenye.

Lakini kuwa public figures sio lazima kujua Kingereza lakini kwa mfanyabiashara kuna umuhimu kama unataka kufanya biashara mpaka nje ya mipaka ya nchi ndio muhimu kujua lugha.
 
Uko sawa kabisa, mimi ni shabiki wa mziki wake sana ila linapokuja suala la interview huwa aibu naona mimi, jamaa hayuko organized, collected kabisa yani anachekacheka tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usifiche fiche mtoa uzi kwa kifupi ndugu yetu ni "NGUMBARU"
 

Niseme "LABDA" ana sababu zake muhimu

Lakini elewa pia kuwa public figure tayari ni brand na unakuwa bidhaa kama zilivyo tu soda ama bear. Hivyo Unapovuka border lazma ujiandae jinsi ya kuwa relevant na hiyo audience mpya ikiwemo lugha wanayoitumia

(kitu ambacho diamond alideal nacho mapema sana japo nae elimu ndogo)

Vinginevyo apate manager mwenye english clean awe kama translator. Kitu ambacho sijawahi kumuona akifanya
 
Ali anajua mwenye future ya muziki wake wapi unaelekea nandio maana kaona lugha sio muhimu kwake.
 
Point noted mkuu[emoji120]
 
Kingereza anajua bana mbona niliona anahojiwa Sibuka Tv akawa anachanganya na maneno ya kingereza!
 
Jamani issue hapa ni hajui KUJIELEZA mtoa mada ndio anasisitiza.Msitoke nje ya mda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…