Ulamaa Abagangaji
Member
- Oct 23, 2017
- 39
- 89
Habari wanajamvi na poleni kwa majukumu ya kujitafutia riziki ili kujenga nchi. Nawaombeni msome mwanzo hadi mwisho ili kuweza kunufaika na FURSA hii ya 'kusikiliza'.
Nijikite kwenye mada moja kwa moja
Sote tunafahamu kazi ya kiungo SIKIO ni kusikia,na ni miongoni mwa 'milango' ya fahamu ya mwanadamu. Kwa tafsiri rahisi na ya haraka haraka,KUSIKIA ni uwezo wa sikio kupitisha mawimbi ya sauti. Kwa tafsiri hiyo basi,kila binadamu anaouwezo wa kusikia labda kwa wale wenye matatizo ya masikio. Mfano ukikaa tu bila kushughulisha ubongo wako na kitu utakuwa unasikia mambo yote au mengi yanayoendelea kwenye mazingira yako ila hamna hata moja litalokushughulisha. Au ukiangalia tamthilia ya kichina wakiwa wanaongea kichina na we hukijui,kweli utakuwa unasikia ila ndo huambulii kitu.
KUSIKIA NI WAJIBU/LAZIMA NA SIO UAMUZI
KUSIKILIZA maana yake inaenda mbele zaidi ya neno kusikia, na hivyo tafsiri yake itakuwa ni uwezo wa sikio kupitisha mawimbi kuyapeleka kwenye ubongo na kupatiwa tafsiri na hatimaye kupatikana mrejesho….ambapo mrejesho huwa ni maamuzi. Mfano mama yupo nyumbani anasikia mtoto analia hivyo anasikiliza kuhakikisha ni sauti ya mtoto kweli na kufanya maamuzi ya kwenda kumchukua kujua kinachomliza.
KUSIKILIZA NI UAMUZI WA MTU NA SIO WAJIBU/LAZIMA
Ama KUSIKILIZIA maana yake ni kuambiwa taarifa ambayo tayari mtu ameishaifanyia kazi na kuitolea maamuzi,kwa kifupi kusikilizia ni hali ya kutumia sikio 'kulishwa' taarifa. Mfano mtu anakwambia kwenye hotuba ya waziri flani au mwanamziki flani pale aliposema hivi alimaanisha hivi,na wewe mhusika pasipo kujishughulisha kutaka kufatilia namna ilivyosemwa unakubaliana na hiyo taarifa. KUSIKILIZIA NI UZEMBE NA UVIVU WA KUSIKILIZA.
Hivyo basi SIO KILA ANAYESIKIA ANAUWEZO WA KUSIKILIZA WENGI WAO WANASIKILIZIA
Nalazimika kuandika haya kutokana na hali ya jamii yetu ilivyosasa hususani vijana kwa kuwa wengi wamekuwa watu wa 'kusikilizia' kiasi kwamba wote wanaishia katika matokeo yaleyale kwa sababu tu chanzo ni kimoja. Utaona ikitokea aina flani ya biashara basi wooooote wataishia kuifanya tena kwa namna sawa na hatimaye anguko huwa ni la pamoja na ndio maana neno 'trend' likawepo. Ikitokea fasheni, ikitokea usemaji,ikitokea simu,ikitokea modeli ya gari,ikitokea chochote kile basi wataigana kwa kuwa chanzo chao chote ni kusikilizia.
Mifano ni mingi sana juu ya vitu hivyo,tuchukulie mfano kwenye tasnia ya ufugaji,si mnayakumbuka mayai ya kware?,mnakumbuka ufugaji wa sungura?,ufugaji wa kuku wa kisasa wa broila je?,vyote hivyo viliibuka na kupotea au kupungua. Sio kwamba vilikuwa havilipi,HAPANA,ila wachache wachache wa mwanzo walisikiliza na wengine waliofuata walikuwa wanasikilizia.
Mpaka sasa mayai ya kware ni biashara,ufugaji wa sungura ni biashara tena kubwa na hata ufugaji wa kuku broila ni biashara ila vyote hivyo vimeondoka na mitaji ya watu na pengine hata kuwatoa watu barabarani kutokana na waliingia kwenye hizo tasnia kwa 'kusikilizia'. Na sisi vijana tunaomsemo siku hizi kwamba "kuna mchongo nauSIKILIZIA", na kweli utaendelea kuusikilizia mpaka unazeeka….mchongo unakuwa mchongoma.
Utaona vitu vinaibuka kwa kasi au wingi na vinapotea kwa kasi au vinapungua kwa kasi yote hiyo ni athari ya kusikilizia na watu hasa vijana wamejipa ukilema wa kusikiliza.
Fursa zote zipo kwenye kusikiliza na sio kusikilizia. Ambaye atasikiliza basi ataweza kuwa na mwanga mzuri wa kufanya maamuzi yake yawe ya kiuchumi, kijamii, kimapenzi, kifamilia, kikazi, kidini yoyote yale. Na ndio maana kuna ule msemo wa zamani ambapo kikitakiwa kuongelewa kitu cha maana chenye uzito, iwe kuelimisha au kuonya au kukataza utasikia wazee wa hekima wanasema "mwenye maskio na asikilize".
Hakuna gharama yoyote ile atayotozwa mtu kwa KUSIKILIZA na bahati nzuri viungo vyote vinavyohusika na usikilizaji navyo pia Mungu katupa bure kwa kila mtu….ambavyo ni SIKIO na UBONGO.
Lakini ili uwe msikilizaji mzuri,kuna tabia ambazo pia inabidi uwe nazo. Tabia hizo ni:
Jaribu kuangalia watu wote wenye kufanikiwa LAZIMA utawakuta wapo na hizo sifa mbili.
Kuwa na UTULIVU haimaanishi wewe ndio unakila kitu,maana watakuja watu kucomment 'unawezaje kuwa na utulivu wa nafsi na akili na wakati una stress za kodi mara ada ya watoto n.k?',jibu lake ni rahisi tu,utulivu ni hali ya kulielewa jambo kwa undani wake,umeshajuwa unakodi unadaiwa au una ada ya watoto unadaiwa,basi inatosha….namna ya kuzipata ni jambo lingine kwa maana huo mjadala ukiufungua ni mrefu mno.
Ufikiriaji ni changamoto sana,wengi wetu baada ya kukisikia kitu basi tunabaki tunakirudia rudia chenyewe au kulalamika au kulaumu badala ya kukitafakari namna ya kukifanyia kazi. Inaweza ikatokea ajali na ikaua watu kadhaa ama wote, wahusika watabaki wanalaumu ama kuiongelea namna ilivyotokea kana kwamba wanaouwezo wa kurudisha muda nyuma, chukulia kama kilichotokea kimeshatokea na ufikirie namna ya kuzuia kisijirudie tena kutokea kwa kadri ya uwezo wako.
Kufanya maamuzi ni matokeo na kusikiliza na ni hatua ya mwisho ya kuwa msikilizaji mzuri sana.Mara nyingi kama sio zote mtu aliyesikiliza huwa anauwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa sababu amesikia kwa utulivu na kutafakari.
Kwa kuhitimisha andiko langu,KUSIKILIZA NI FURSA lakini ili unufaike na fursa hii usiangukie kwenye mtego wa kusikilizia kama ilivyo kwa watu wengi,inabidi uwe na tabia ya utulivu,ufikiriaji na ufanyaji maamuzi.
Natumaini wanajamvi wote kuanzia sasa tutakuwa WASIKILIZAJI.
Naomba kuwasilisha.
Ulamaa Abagangaji.
sokony6@gmail.com

- UTULIVU (wa nafsi na akili).
- UFIKIRIAJI.
- KUFANYA MAAMUZI (kuwa na msimamo kwa vitendo)

Upvote
0