Nipo hapa kwenye kibanda umiza na jamaa wawili watatu tunatazama mpira wa Yanga na Lipuli. Kwa kweli Yanga ni tia maji tia maji. Mpaka sasa dakika ya 65 wana goli 1 tu.
Mpira umepoa sana,mtangazaji anajitahidi kupamba lakini wapi mpira mwingi hauonekana. Nimejikuta natafakari hivi kati ya hawa vijana wa Yanga wanaorukaruka humu kuna hata mmoja anayeweza kupata nafasi Club kubwa Simba SC?
Binafsi sioni iwe ni hawa wa ndani,benchi au hata jukwaani. Simba imejaa vipaji na wapambanaji. Hawa Yanga sijui wanachezaje hakuna mishe kabisa. Wapo vijana wawili watatu kama Yondani na Fei Toto wanajitahidi lakini bado sioni kama mtu wa kumweka benchi Simba.