Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 520
- 2,930
Uwanja mkubwa kuliko yote hapa nchini ni Uwanja wa Taifa (Uwanja wa Mkapa) ambao unachukua watazamaji 60,000.
Uwanja huu unamilikiwa na Serikali ulijengwa kwa ushirikiano na serikali ya China mwaka 2007.Unalingana na uwanja wa Kasarani wa Mathare Kenya ambao nao una uwezo sawa.
Kigoma huku uwanja wetu mkubwa ni huu uwanja wa Lake Tanganyika ndio ambao utachezwa mechi kati ya Simba na yanga tar 25 Julai hii 2021.
Nimeona hii video ikiwa ina sambaa na watu wakikosoa vikali maamuzi ya TFF kupanga mchezo huu kupigwa Kigoma sababu kwamba uwanja ni mdogo na ni mbovu .
Nadhani tathimini stahiki zifanyike kuona namna gani uwanja huu utaweza kutosha idadi ya watu siku hiyo bila kuleta athari yeyote na usalama wa watu ni Muhimu pia, kwetu sisi wakazi wa Kigoma mechi hii kuchezwa kwetu ni fursa kwetu kibiashara na mzunguko wa fedha kutokana na ujio wa wageni ingawa usalama ni jambo la msingi pia.
Lakini pia ni fursa kwa viongozi wa Serikali na viongozi wa soka waone namna viwanja vyetu vya mpira vinavyokufa , kuharibika na kuchakaa kwa kuendekeza kukumbatiwa na kumilikiwa na CCM bila kuwaza ubora wa viwanja vyetu na kuendelea kwa soka letu nchini.Uwanja wa Lake Tanganyika upo Kigoma mjini.Uwanja huu ulijengwa mwaka 1980 una uwezo wa kuchukua watu 15,000. Sasa hivi ndio unafanyiwa ukarabati ili uweze kuchukua watu 17000. Uwanja huu una milikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).
NI uwanja wa muda mrefu ila unaharibika kwa kukosa maboresho ,leo hii sababu ya mechi hii ndio unarekebishwa ,mimi sioni sababu ya viwanja vyetu kuendelea kumilikiwa na chama cha mapinduzi .
Kamati ya ulinzi na usalama mkoa waone namna bora zaidi ya kuhakikisha mchezo kati ya simba na yanga unakwenda vyema bila kuleta athari ya kiusalama sababu ya udogo na uchakavu wa uwanja wetu.
Ila hoja yangu ni ile ile sioni sababu viwanja vyetu kuendelea kumilikiwa na chama cha mapinduzi , viwanja hivi vimilikiwe na Serikali au taasisi binafsi.
Viwanja vingi vinakufa sababu ya umiliki wa CCM.
2.Uwanja wa Jamhuri Morogoro
Unamilikiwa CCM
ulijengwa mwaka 1978, una uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000.
3.Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine wa Mbeya ulijengwa mwaka 1977, una uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000 na unamilikiwa na CCM
4.Uwanja wa Jamhuri Dodoma . Endelea chini
Uwanja wa Jamhuri Dodoma . Ulijengwa mwaka 1978 una uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000.Unamilikiwa CCM.
5.Uwanja wa Majimaji
wa Songea mkoa wa Ruvuma.Una uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000, ulijengwa mwaka 1979.Unamilikiwa na CCM.
6.Uwanja wa Kirumba upo jijini Mwanza.Ulijengwa mwaka 1980, una uwezo wa kuchukua watazamaji 45,000.Kirumba ni uwanja wa pili kwa ukubwa Tanzania Bara.Una milikiwa na CCM.
7.Uwanja wa Kambarage, upo Shinyanga,unamilikiwa na CCM.Ulijengwa mwaka 1983, una uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000.
8.Uwanja wa Namfua upo Singida unamilikiwa na CCM. Uliejengwa mwaka 1982 una uwezo wa kuchukua watazamaji 10,000.
9.Uwanja wa Sheikh Amri Abeid upo Arusha.Ulijengwa mwaka 1957, unamilikiwa na CCM ,una uwezo wa kuingiza watazamaji 25,000.
10.Uwanja wa Mkwakwani,upo Tanga unamilikiwa na CCM, ulijengwa mwaka 1972 na unachukua watazamaji 15,000.
11.Uwanja wa Samora ulijengwa mwaka 1975, unamilikiwa na CCM, unachukua watu 25,000.
12.Uwanja wa Kaitaba,
Upo mkoa wa Kagera unimilikiwa na mali ya CCM . Ulijengwa mwaka 1976 unachukua watu 25,000
13.Uwanja wa Mandela,upo katika mkoa wa Rukwa unamilikiwa na CCM unachukua watu 15,000.
14.Uwanja wa Karume
upo Morogoro ulijengwa mwaka 1986 ,unamilikiwa na CCM unachukua watu 15,000.
15.Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.Unamilikiwa na CCM ,ulijengwa 1988 unachukua watazamaji 30,000.