Ukitaka kujua chama kimeshindwa kushindana, kila mara huja na sheria kandamizi. Huu ni baadhi ya mitazamo ya watu wenye kupenda kutunga sheria kandamizi ili kukidhi mahitaji ya muda mfupi. Jana ccm walikuwa na tamasha sijui onyesho hapa uwanja wa Taifa, ambalo nini kampeni ya wazi kabisa, lakini ikitokea na wapinzani nao wakafanya na wakapata mwitikio mkubwa, utakuja na ushauri huu kuwa kutungwe sheria kusiwe na matamasha mpaka kibali. Kwa mwenendo huu sintoshangaa ukitaka kuwe na sheria inayokataza kampeni za wazi, bali za ndani ili kuepusha nyomi.